SoC02 Namna ya uwezeshwaji kwa vijana ili kujikwamua kiuchumi na kijamii

Stories of Change - 2022 Competition
Nov 9, 2015
15
15
Namna ya uwezeshwaji kwa vijana ili kujikwamua kiuchumi na kijamii.

Kwanza nitoe pole kwa wasomaji wenzangu hasa vijana hivyo nami nitakuwa miongoni mwa watoa makala za mashindano ya mabadiliko au mageuzi kwa ajili ya uwezeshwaji kwa vijana ili kujikwamua kiuchumi na kijamii. Makala hii imeshajieleza hapo juu lengo kuu ni namna ya uwezeshwaji kwa vijana ili kujikwamua kiuchumi na kijamii. Kwanza nitaongelea vijana kwa makundi makuu matatu kwa maana ya kwamba.

Kundi namba moja la vijana waliotoka katika familia duni (uchumi mdogo),kundi namba mbili la vijana waliotoka katika familia yenye unafuu na maisha (uchumi wa Kati ) na kundi namba tatu la vijana waliotoka katika familia yenye maisha Bora (uchumi mkubwa)

Kundi namba moja la vijana waliotoka katika familia duni (uchumi mdogo)

Tunapoongelea uchumi mdogo tunalenga familia zinazoishi chini ya dola moja kwa siku hivyo siyo rahisi kwa kijana kama huyu kufikia ndoto zake kirahisi kama walivyo vijana wengine waliotoka katika familia zenye uchumi wa Kati au uchumi mkubwa ni ngumu kwa sababu kumbukeni huyu kijana hana pakuanzia wala mtu wa kumsaidia angalau pesa au ushauri wa kujikwamua kiuchumi na kijamii. Hivyo basi kwa vijana wanaokumbwa na changamoto kama hizo nilizoziainisha kwa uchache ni bora pesa zinazokopeshwa Halmashauri za asilimia ( 10% ) wakopeshwe vijana (mmoja mmoja ) bila kujiunga kwenye vikundi vyovyote ,lengo kuu la hili ili vijana wajikwamue kiuchumi na kijamii,bila kutumia hii njia vijana waliotoka kwenye familia kama hizo kamwe haitatokea hata siku moja vijana wa kwenye hilo kundi namba 01 likajikwamua kiuchumi na kijamiii.

Hivyo makala yangu italenga kwa namna hiyo ili tujikwamue vijana tuliotoka kwenye hizo familia duni ,sharti bora na lenye unafuu kwa vijana inabidi tutumie mfumo huo kwa kuhimiza Bunge na Serikali kwa kubadirisha sheria za utoaji wa mikopo kwa Halmashauri zote nchini Kuwa mikopo itolewe kwa mtu mmoja mmoja mwenye uhitaji

Bunge na Serikali ikikubali hiyo sheria ipitishwe hapo ndo kutakuwa na mabadiliko au mageuzi ya kujikwamua kiuchumi na kijamii kwa vijana wanaotoka kwenye familia zenye uchumi duni au kipato kidogo, kupitia hizo mikopo za Halmashauri zitakazotolewa kwa kijana mmoja mmoja zitafanya vijana wengi wajiajiri hivyo tutapunguza changamoto za ajira nchini pia pato la taifa litaongezeka kwa namna hiyo tutakuwa tumeshaweza kumwezesha kijana au vijana kiuchumi na kijamii.Pia kupitia hiyo mikopo ya Halmashauri kote nchini masharti yawe nafuu ili kumuwezesha kijana au vijana aweze kukidhi vigezo vya kupata huo mkopo wenye masharti nafuu kwa kijana au vijana

Mfano wa mashariti yanayotakiwa apewe kipaumbele ili aweze kusaidiwa mkopo wa kujianzishia Biashara yoyote au Mradi wowote ni kama ifuatavyo :Awe mkazi wa kudumu wa hilo eneo husika, mdhamini wake awe mwenyekiti wa Kijiji/mtaa pamoja na kitongoji wa mtaa/Kijiji pia na mtendaji wa kijiji/mtaa. Hivyo ndo viwe vigezo vikuu vya kuwezeshwa Mkopo, hapo ndo tutakuwa tumemwezesha kijana au vijana kujikwamua kiuchumi na kijamii katika taifa letu pia tutakuwa tumepunguza changamoto za ajira kwa kiasi fulani.

Kwanini ninapendekeza au ninashauri Bunge au Serikali wapitishe sheria ya mikopo ya Halmashauri ya kijana mmoja mmoja ndo apewe mikopo kwa sababu kama zifuatazo mikopo ya vikundi kwa vijana haviwanufaishi moja kwa moja ila ndo chanzo cha kutengeneza migogoro ya vikundi kwa muda mrefu mwisho wa siku vinashindwa kuleta tija ambayo imelenga kuondoa umasikini wa mtu mmoja, kaya na taifa kiujumla mfano katika vikundi 05 vinavyoweza kuendelea na kuleta tija kwa wanakikundi ni kimoja tuu (01) kati ya vikundi 05 ndo maana nikaona ni bora hiyo mikopo apewe kijana pekee yake iweze kuleta tija kwa kijana na familia yake mwisho wa siku kuleta tija kwa taifa kwa ujumla.

Kutokana na kufanya utafiti mdogo kwa wilaya fulani kwa kuuliza vijana mbali mbali waliowahi kujiunga kwenye hivyo vikundi mbali mbali waliweza kuelezea changamoto za vikundi mbali mbali kwa mfano kutokuaminiana,kutokuwa wawazi baadhi ya viongozi wa vikundi hivo ,hivyo basi kutokana na hizo changamoto nilizoziainisha hapo Juu, vijana wanapendekeza kijana mwenye uhitaji apewe mkopo mwenyewe kuliko vikundi.

Kundi namba mbili la vijana waliotoka kwenye familia yenye uchumi nafuu (uchumi wa Kati )

Tunapoongelea uchumi wa kati tunalenga familia zinazoishi juu ya dola moja kwa siku nakuendelea hivyo kijana au vijana wanaotokea katika kaya kama hizo , kwao kutoka kimaisha au kuwezeshwa ili wajikwamue kiuchumi na kijamii ni rahisi kwa sababu wazazi au ndugu na jamaa wanauwezo wa kumuwezesha kifedha na mengineyo hivyo sitaongelea kwa upana zaidi kutokana kuwa hao vijana wa hizo familia wana wigo mpana wakuwezeshwa na ndugu na jamaa bila kupitia changamoto zozote wanazopitia kama vijana wa familia duni.

Kundi namba tatu la vijana waliotoka kwenye familia zenye uchumi bora (uchumi mkubwa).

Tunapoongelea uchumi bora tunalenga familia zinazoishi maisha ya juu kwa kila kitu ,hivyo kijana au Vijana wanaotoka kwenye familia bora wao kuwezeshwa kiuchumi na kijamii hapati changamoto zozote kama vijana wanaotokea katika familia duni, mfano kijana au Vijana akitaka kuwezeshwa kiuchumi na taasisi yoyote hapa nchini naamini kwa asilimia mia moja hata pata changamoto yoyote ya kuwezeshwa ,Mfano mdogo kijana wa Said Bakhresa na wengineo hivyo sitaongelea kwa upana zaidi.

Mwisho naomba kura yako.
 
umeandika ndugu yangu✊🏾😊
pia elimu. Kabla hawajapewa mitaji vijan inabidi waelezwe ukweli aise elimu na kujiamin kupitia Mungu wake..maisha Yamejaa siri nje ya PESA tunayoiangaikia kila siku


They tell us their secrets of success and doesn't involve spiritual power at All ☺💔 there's working power every second in our life ...be careful if you seek life with real purpose
 
Back
Top Bottom