Namna ya kutatua tatizo la ajira Tanzania

Tumtepe95

New Member
Jul 17, 2021
2
1
Naomba niongee kuhusu vijana wanaomaliza kidato cha sita na kupangiwa kwenda mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria, sikatai ni kweli wanaenda kufundishwa mafunzo ya awali ya ulinzi na usalama pamoja, uzalendo na uzalishaji mali lakini tija ya maarifa wanayoyapata vijana hawa imeshindwa kabisa kutatua tatizo la ajira Tanzania.

USHAURI WANGU

Ningependa kuishauri serikali kuwa pindi vijana wale wanapomaliza kidato cha sita wakiwa wanasubiri matokeo, ingekua na matokeo chanya sana kama wakati wachache wamepangwa kwenda JKT bhasi wengine wengi wangepelekwa VETA na kwenye taasisi nyingine za UFUNDI, USUSI, UVUVI, UFUGAJI NA KILIMO pamoja na tassisi zingine nyingi kwa kufanya hivi tungejikuta tunatengeneza taifa lenye vijana wenye maarifa tofauti tofauti na mwisho wa siku wanapohitimu vyuo vikuu wakaweze kujiajiri wao na kuajiri wenzao kutokana na maarifa walioyapata kipindi wapo VETA na kwenye taasisi nyingine nyingi walizokua wamepangiwa kuliko kupanga kwenda JKT tu ambapo kwa miaka miki toka kuanzishwa kwa mfumo huu pameshindwa kikubwa kuwapa vijana maarifa ya kutosha ili kutatua tatizo la ajira.

Nawasilisha

20210718_064718.jpg
 
View attachment 1857743
Wazo zuri sana,ila Veta wangeshirikiana ns J.K.T,kuwa pamoja kuwashughulikia vijana katika fani mbalimbali wakiwa kambini.
 
Naunga mkono hoja. Nafikiri huko huko JKT wangeanzisha kozi mbalimbali za kuwajengea vijana uwezo wa kujiajiri.

Vyuo pia vibadilishe/vianzishe mitaala itayokwenda na wakati wa sasa. Waanzishe Kozi za kuwawezesha vijana hata wakimaliza masomo yao wawe na ujasiri wa kujiajiri na si kutegemea kuajiriwa peke yake.
 
Tatizo la ukosefu wa ajira tanzania sio vijana kukosa elimu, tatizo la ajira tanzania linasabishwa na vijana wengi kutokuwa na uthubutu na kuridhika na umaskini uliopo kwenye jamii
 
Naunga mkono hoja. Nafikiri huko huko JKT wangeanzisha kozi mbalimbali za kuwajengea vijana uwezo wa kujiajiri.

Vyuo pia vibadilishe/vianzishe mitaala itayokwenda na wakati wa sasa. Waanzishe Kozi za kuwawezesha vijana hata wakimaliza masomo yao wawe na ujasiri wa kujiajiri na si kutegemea kuajiriwa peke yake.
Exactly broo
 
Back
Top Bottom