Namna ya kutafuta 'alama yako' kiroho

Namna ya kutafuta 'alama yako' kiroho

View attachment 581171mafuvu ni alama maarufu inayotumiwa na wengi... Wengine wanajua maana yake na wengine ni kuiga tu.. Fuvu na mifupa miwili ni alama ya kufisha na uharibifu
Watu hupenda kuwa na alama mbalimbali za kujitambulisha, hata hapa JF kuna watu hutumia alama kwenye avatar zao
Kuwa makini na alama unayotumia kwakuwa kiroho hukutmbulisha hivyo na kuipa nguvu ya kutenda katika ulimwengu halisi
Unatafuta vipi alama yako halisi? Fanya hivi
1. Tafuta sehemu iliyokuwa kimya na tulivu
2. Kaa katika mkao wa tahajudi kwa utulivu
3. Vuta hisia za ngazi... Yaani tengeneza ngazi akilini mwako
4. Weka nia ya kuipata alama yako juu mwisho wa ngazi
5. Vuta hisia halisi za kuanza kupanda ngazi yako
6. Panda kihisia mpaka juu kabisa
7. Cha kwanza utakachokiona mawazoni mwako juu mwisho wa ngazi ndio alama yako kiroho... Itumie hiyo kwa mambo yako... Unaweza ichapa kwenye vitu vyako, kuitumia kama avatar, kuitumia kwenye manuizi na viapo! Wengine hujichora tattoo ya alama zao
Ukiweza kuipatia alama yako kwa usahihi utakuwa umezalisha roho yenye nguvu hata kwenye mambo ya kulaani na ushirikina hivyo kuwa mwangalifu sana
Njia ya tahaduji ni ngumu hivyo baadhi hutumia bangi kupata imagination husika ama ulozi lakini hizi ni njia bandia na zenye madhara mengi

Sent using Jamii Forums mobile app
Inaonekana hii ni aina fulani ya ramli ya kujipigia mwenyewe! Kuna mtu aliniambia,ramli nyingi siku hizi zinashindikana kutokana na watu wengi kuwa na msongo wa mawazo ya maisha,hakuna utulivu wa akili ambayo ndiyo sifa kubwa ya kufanikisha ramli. Vipi hapo?
 
Sahihi kabisa ukiweza kuishi ndani ya nafsi yako mwenyewe na kuondoa taka taka zote za msongo wa maisha (mapenzi, kazi, umaarufu, cheo na utajiri ) na kufanya akili yako ifanye jambo moja tu kwa wakati mmoja unaweza kuwa hata nabii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sahihi kabisa ukiweza kuishi ndani ya nafsi yako mwenyewe na kuondoa taka taka zote za msongo wa maisha (mapenzi, kazi, umaarufu, cheo na utajiri ) na kufanya akili yako ifanye jambo moja tu kwa wakati mmoja unaweza kuwa hata nabii

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa Mshana Jr,mapenzi, kazi, umaarufu, cheo na utajiri ndiyo style ya maisha na haviepukiki! Kwa maana hiyo,bado ninaona kuna ugumu kufikia unachosema. Otherwise,utupe mbinu ya kuviondoa vitu hivyo ndani ya nafsi zetu. Mf,mapenzi (lazima umfikirie mke wako kimapenzi,na haitoki kichwani),kazi (ajira ni ngumu na muda wote ni kufikiri namna ya kupata kazi), umaarufu ( wachungaji,maaskofu,watawala,hata fukara wa kawaida siku hizi ni kutafuta kiki za umaarufu), cheo na utajiri (hii ndo basi tena na waganga woote wanaosifika ni kwa kuwaletea wateja vyeo na utajiri).
 
Ni sawa lakini usiwe mtumwa wa hivyo vitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmmh ngumu kuamini kutokana na imani yangu, ila alama za kwenye nguo au vitu huwa najitahidi kuepukana nazo hasa makopo ya vinywaji najua ni alama za nguvu za giza, sasa pia kupata alama hii sitajaribu, tena wengine wanasema utafute sijui rangi yako yaani full stress, Mungu ninayemwamini anisaidie tu

Sent using Jamii Forums mobile app
amina!
 
Kitu TAHAJUDI huwa sikielewi ni nini hasa....!!

Sent using Jamii Forums mobile app
meditation
yaani namna gani unavyoweza kurushu mwili na akili vifanye communication na nafsi ambapo sasa unaipa nasfi uhuru wa kutumia nguvu yake kukuwezasha kuona yaliojificha katika ulimwengu mwingine ila kitu hii meditation imegawanyika sana na inatengemea nini unataka kufanya na ni aina gani ya meditation unataka kutumia
 
Meditation ni muhimu kwani hata mimi nilitafakari kwa kina mpaka nikapata jibu langu mwenyewe kuwa "dini zimesukwa na wajanja, Mungu wangu namjua mwenyewe. "samahani nimetoka nje ya mada unisamehe bure .Nimejihami mapema kwani Mshana unasuka hoja zako kwa ufundi wa hali ya juu

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji817] [emoji115] [emoji115] [emoji781] [emoji779]

Jr[emoji769]
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom