Namna ya kuandaa video ya muziki ya kiubunifu

Jun 26, 2015
55
61
Kufaidi keki iliyoko kwenye tasnia ya burudani, Music video ni uma mzuri, ukiutumia kibunifu unaweza ukachoma mapande yenye faida.

Kwanini?

Music video producers wapo wachache?
Hapana bali wengi wanapuuzia utaratibu wa kuandaa video kali ya muziki.

"Sio wote wanapuuzia kwa kupenda". Wapo wanao onekana wanapuuzia, lakini ukweli ni kwamba hawajui hizi njia. Wapo wanaopuuzia tu kwa kupenda kwao. Wapo wanaopuuzia kwasababu za kibajeti au udogo wa msanii.

Lakini mimi nakwambia usikubali bajeti au udogo wa msanii ukakufanya upuuzie utaratibu.

Video kuwa Kali, kuna mambo mengi. Lakini nimejaribu kuvi lundika lundika na nimepata viwili; Ubora wa picha na ubunifu. Sasa kwa asilimia kubwa tatizo ni ubora wa picha, kwasababu hapa utahitaji kamera za hadhi ya juu (ukodi au ununue) na vifaa vingine vingi ambavyo itabidi ukodi au ununue. Hili ni tatizo kwasababu linahusisha pesa na kama bajeti ni ndogo, huwezi kuvipata hivi vyote.

Kuhusu ubunifu niswala hasa la kuumiza tu kichwa na wala sio mifuko.

Sasa miujiza hua inatokea pale ambapo, una bajeti yakusaza na ubunifu ni life style yako.
Usiogope! ili uonekane wewe ni noma, huitaji mavifaa ya gharama unaitaji ubunifu tu!

Kama unataka kuingia kwenye utengenezaji wa video, hivi ndivyo unavyoweza kuandaa video ya kuzingatia ubunifu zaidi.

SIKILIZA NGOMA MARA NYINGI UWEZAVYO

SIKILIZA Unapofua, unapopika, Kula, kulala...huwezi jua Idea kali itatokea wapi. Lakini pia tenga muda wa kusikiliza kwa utulivu mstari kwa mstari. Usije kusahau pia kuna umuhimu wakusikiliza instrumental au Biti ya nyimbo.

Kufanya haya yote kutakufanya kujua na kuelewa nyimbo, na kutakuongoza kwenye hatua inayofwata. Itakusaidia kuamua namna ya kushuti na kuediti hio video.
Unavyosikiliza tafakari hisia unazo pata wakati huo; huzuni, furaha, kicheko, kilio, hasira, majivuno n.k. hizi hisia lazima utatakiwa kuziwasilisha kwa njia ya picha.
Unaona nini ukisikiliza nyimbo?

Ukimalizana na hili. Sikiliza tena na tena na tena. Wataalamu wa saikolojia nao watakubaliana na mimi kwenye umuhimu wa kusikiliza.

ANDAA STORY

kwa kusikiliza Mara NYINGI utakua umeshajua na kuielewa nyimbo. Na umeshapata taswira ya namna gani picha ya nyimbo itakavyo kua.

Sasa unaandika story ambayo utaisimulia moja kwa moja kwenye video. Japo unaweza pia usisimulie story ya nyimbo kwenye video (binafsi napenda sana hii). Lakini kama utaisimulia tuendelee.

Mfano, Nyimbo inaweza ikiwa inahusu mtu aliye tupwa na mama yake kisa ni mlemavu:
Unaweza ukashindwa kusimulia kisa hicho, kwasababu bajeti yenu hairuhusu lakini hio ni fursa ya kua mbunifu zaidi.

Unaweza ukaonesha namna mama alivyo mtupa mtoto... lakini hii haitokua ya kibunifu zaidi kulinganisha na; Ukionesha mtoto anaetupwa anaimba... Hii itakua noma zaidi.
Swala ni kwamba uumize sana kichwa kusimulia Hadithi kwa njia ambayo sio ya kawaida. Mtu akimaliza kutazama video yako anatoka na hisia gani? Usikubali mtu aseme "hii video kali" . Kwasababu hio haitoshi, inabidi mtu aweze kuirudia tena na tena, na aweze kushirikisha wengine waitazame.

Tujibu swali hilo la; Mtu akimaliza kutazama video yako anatoka na hisia gani? Huzuni, furaha, kicheko, mshangao, mshtuko (hiki nini tena) n.k

ANDIKA SCREEN PLAY

Screen play ni namna gani video itaonekana kwenye screen. Kwahio hapa unalazimika kuandaa namna kila sekunde ya video itakavyoonekana. Yaani sekunde ya 2 hadi ya 5 kutakua na kipande Cha mama akimshusha mwanae kwenye shimo la choo. Au Sekunde ya dakika ya 2 hadi dakika ya 2.5 itapita picha ya msanii akiimba kwa majonzi katikati ya njia ya mtaani.

Ni muhimu kuandika hivi, kwasababu nyimbo moja ina vipande vingi, vipande vya mistari au intrumental, na kila kipande kuna namna ambayo ukiiwakilisha kitaleta maana au tuseme kitaleta mguso wa kipekee Sana.
Ukifanya hivi utakua umeanza kuedit video kabla hata hujaiingiza kwenye program. Na hii itakurahisishia hata ukiiweka kwenye program unakua unafwatisha tu.

KUSHUTI

Hii inakua kazi rahisi sana, kwasababu tayari unayo screen play. Unajua kabisa unaenda kushuti nini. Japo mambo yanaweza badilika, si vibaya kuendana nayo kama haya haribu picha uliyonayo kichwani.

Ukimaliza kushuti vitu kulingana na screenplay yako, Sasa unaweza kuanza kushuti vitu vingine ambavyo hukuandika hivi vitakusaidia kujazia sehemu ambazo clips zimepungua.

Go and make your dream music video.
 
Back
Top Bottom