Diwani
JF-Expert Member
- Oct 25, 2014
- 2,824
- 3,021
Hapa nazungumzia sana vijana ambao wanajitafuta kwa wakati huu; mara nyingi jamii inawapa msukumo wa kutafuta hela na inawathibitishia kwamba bila kuwa na pesa wao si kitu na hawana nafasi ya kimaamuzi au ushawishi wowote kwenye jamii na hata kwenye mahusiano.
Vijana (ME) kwa sababu ya fikra hii hujikuta wakitafsiri maisha kwenye mitazamo ya kifedha tu, bila kujali utu, mapenzi, haiba, mwenendo na hata heshima. Ikitokea ameingia kwenye mahusiano na amepata fedha, atakuwa akitafsiri kila anachofanyiwa hata kama ni kwa upendo kutoka kwa mwenza wake, ataona ni kwa sababu ya fedha alizo nazo.
Hata akihudumiwa kama mume au mwenza; tafsiri juu ya afanyavyo ni kwa sababu ya pesa alizonazo, jambo ambalo linamuondolea utu na kumtazama mwenza wake kama bidhaa, na wakati mwingine kumuondolea heshima kama binadamu; hii inatokana na mtazamo aliopandikizwa kuhusu fedha.
Kuna kundi kubwa la Wanawake wanavumilia mahusiano machungu, kwa sababu tu ya kuwa na Wanaume wenye fedha, na Wanaume hao wanahisi wana haki ya kuwafanya lolote kwa sababu ya fedha zao.
Endapo mitazamo hii inabadilika, haitaweza kumuathiri Mwanamume anapopata mpenzi; atazingatia upendo na heshima kwa Mwanamke kwa sababu ni msingi wa mahusiano yake naye, na si kwa sababu ya fedha zake lakini jambo hili linaanzia na kupewa heshima hata pale ambapo hana kitu.