SueIsmael
JF-Expert Member
- Dec 11, 2013
- 932
- 1,283
Matatizo mengi tunayoyapitia ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yametokana na mifumo tuliyonayo kama nchi na wananchi, pamoja na mifumo iliyojengwa "na dunia".
Bara la Afrika lilikuwa na mifumo yake ya uongozi, uchumi, ustaarabu, jamii, usalama, nk., kabla ya biashara za masafa marefu na kabla ya ukoloni. Tulikuwa na matatizo yetu ila tulikuwa na mifumo ya kutatua matatizo hayo, au hata kukabiliana nayo. Pasi na shaka ukoloni uliharibu sana mifumo hiyo, aidha ukifutilia mbali au kuigeuza iwanufaishe wao. Zaidi ya hapo walifanya jitihada kubwa sana kupoteza na kusahaulisha historia ya ustaarabu wa mwafrika. Baadhi ya maeneo walichochea chuki na mifarakano kwa makusudi ili kutawala kwa urahisi zaidi, kwa maana kundi moja lilipewa madaraka ya kiasi na hivyo kupunguza uwekezaji kwenye nguvu kazi. (Mfano, rejea matatizo ya Wahutu na Watutsi Rwanda).
Baada ya kupata uhuru kwa nchi za Afrika, mifumo hii haikubadilishwa. Iliasiliwa na wanasiasa kwa kuwa iliwapa nguvu ya kufanya mabadiliko kwa uharaka zaidi (haijalishi dhamira ya mabadiliko hayo) na hivyo nguvu waliyoipata wanasiasa ilikuwa mabaki ya nguvu waliyokuwa nayo wakoloni. Japo Tanzania iliandaa Katiba yake, ila kwa kiasi kikubwa ilibakiza mamlaka kwa wanasiasa (na baadhi ya watendaji) na siyo kwa taasisi. Kwa mfano, ukiangalia historia ya TPDF, utagundua kuwa siasa ilitawala uanzishwaji wa taasisi hii nyeti. Baada ya uasi wa baadhi ya wanajeshi wa Tanganyika Rifles, TPDF iliundwa kwa kusomesha na kuajiri vijana kutoka matawi ya TANU na Afro-Shiraz Party. Mfano mwingine, ni mamlaka aliyonayo Rais na uwezo wa kumwajibisha akiwa madarakani au hata akitoka.
Mifumo waliyoiacha wakoloni haikuhitaji wawajibike kwa yoyote zaidi ya makao makuu yao. Mpaka leo tukiangalia swala la uwajibikaji, tunagundua kuwa hatuna mifumo imara kwanzia ya kifikra hadi ya "kimamlaka" ndani ya nchi. Wananchi wana nafasi ya kuwajibisha wanasiasa kwenye sanduku la kura. Baada ya hapo, mifumo iliyopo "ina hiari" ya kumwajibisha mwanasiasa au la. Pale DPP anapoamua kumfutia mtu kesi, kwa mamlaka aliyopewa, kuna mfumo upi wa kumwajibisha ikiwa sheria inamruhusu? Tuna mifumo inayolinda mtu mmoja mmoja, na hili tumelirithi.
Ili kuwe na "checks and balance" lazima mifumo yote ya uongozi (kiuchumi, kisiasa, kijamii, kiusalama na kiutamaduni) iweze kuwajibika kwa usawa, na wananchi wawe na uwezo wa kuwajibisha kwa wakati. Kwa sasa "siasa" zimetawala mifumo yote kwa kiasi kwamba, tunategemea wanasiasa waendeshe na kusimamia nyanja zote. Mchango wa sekta nyingine ni kwa "ruhusa" ya wanasiasa.
Zaidi ya hapo, siasa zetu zina "umri" mfupi. Kila anayeingia kwenye madaraka ana miaka mitano hadi kumi ya kuamua anachotaka "kuifanyia" Tanzania. Mwanasiasa ndio anaamua dira ya Tanzania, sio mtanzania. Mara ya mwisho mtanzania kushirikishwa katika maaumuzi ya dira ya nchi yake ni katika zoezi la katiba mpya, na wengi wetu tunajua hilo zoezi liliishia wapi. Vyama vya siasa ndio vinaamua mustakabali wa nchi nzima kupitia manifesto zao, ambazo wanamaamuzi ya kuzifuata au la.
Tunahitaji mjadala wa kitaifa kuamua mustakabali wa taifa letu. Ila je, sote tuko tayari kwa hili? Ni nani atakayeongoza mjadala huu? Tuko tayari kubadili mifumo inayowapa baadhi nguvu kubwa na kuwaneemesha baadhi (hasa wanasiasa)? Kuna nia ya pamoja au hata utayari wa kukubali kuna haja ya mjadala huu?
Namna pekee ya kusonga mbele ni kubadili mifumo. Je wanasiasa watakubali kubadili mifumo inayowapa na kuwalindia mamlaka na nguvu wanayopata chini ya mifumo hiyo? Tukumbuke kuwa hatuwezi kusubiri nguvu ya nje kufanya mabadiliko haya, kwa maana hili litaleta hasara nyingine kubwa zaidi.