Namna mzee Mapanga alivyouwawa kwa mapanga!

Namna mzee Mapanga alivyouwawa kwa mapanga!

galatia

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2016
Posts
342
Reaction score
829
Hicho ni kisa cha kweli kbsa!

Mzee huyu alikuwa anaitwa Hasani Masatu kabla ya kuitwa Mapanga Melele!

Ilikuwa hivi;
Mzee Hasani Masatu alikuwa injinia wa barabara miaka kuanzia arobaini mpaka miaka ya themanini...
Alikuwa ni mwanaume strong, alipo yeye hakutaka kuonekana ameshindwa jambo..Tabia hiyo ilimpelekea kuogopwa na wafanyakazi waliokuwa chini yake..
Maagizo yake yalifanya kazi bila kupindishwa..

Akiwa anasimamia ujenzi wa barabara ya Itigi mpaka mbeya kupitia Makongolosi aliwahimiza wafanyakazi kubebe mapanga kila waendapo site..

Alisikika akiseme Mapanga milele...kauli hii ilipelekea wafanyakazi wamwite Mapanga Melele kwa sababu ya matamshi yake.

Mzee Hasani alilikubali lile jina jipya na Kwa makusudi akaamua kuliua jina lake la Hassan Masatu....ktk hili pia alifanikiwa kwa 100%

Hata sasa ukienda maeneo ya manyoni na Itigi ukalizia kwa jina la Hassan Masatu huwezi kumpata lkn ukisema Mapanga Melele ni rahisi kujulishwa alikuwa ni nani..

...hata ukigoole Mapanga Melele utaona matokeo yake.

Mzee Mapanga Melele alikuwa ni mtu asiyependa kushindwa , Mwenye nguvu, jasiri , mkali na asiyeogopa kitu..

Tabia zake hizo zilifanya jamiii inayomzunguka kumuogopa na kumuheshimu sana..

Kwasababu ya bidii ktk kazi mzee yule alikuwa tajiri sana ...pamoja nakuwa ni muajiriwa wa serikali lkn pia alikuwa mkulima na mfugaji mkubwa sana wa ng'ombe na mbuzi...

Mzee Mapanga baada ya kukubali kubadirishwa jina alibadirisha pia majina ya pili ya watoto wak wote.

Mtoto wa kwanza wa Mzee Mapanga aliitwa Juma Mapanga Melele, wapili Aliitwa Ally Mapanga Melele....na wengine hivyo hivyo.

Mapanga Melele alikuwa na bidii ya kuoa na kuacha pia ..alipo muacha mama wa akina Juma, Ally na Milaji alimuoa mwanamke mwngine ambaye nae alizaa nae watoto wawili...

Alipoacha na huyo mke wa pili alimuoa mwanamke mwngine wakigogo , yule mwanamke alipoona hazai alimuomba mumewe amuoe na mdogo wake ili amzalie watoto maana yeye likuwa hazai..bila shaka Mzee Mapanga alikubali na akawaoa mtu na Dada yake.
Mdogo mtu akazaa watoto wa nne.

Mzee Mapanga alikuwa mkorofi anayejua kupiga mke vizuri sana, mmoja wa wake zake aliwahi kupigwa na kung'olewa nywele kisa alikwenda kusuka bila kuomba ruksa kwa mumewe.

Mzee huyu alithamini sana elimu pamoja na nakuwa alikuwa na tabia za kizamani....hivyo alijitahidi kusomesha watoto wake kwa kadri alivyoweza..

Mtoto wake wa kwanza Juma Mapanga alichaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Makerere kwa bahati mbaya aliugua kichaa ugonjwa uliomfanya akatishe masomo yake. Na aliendelea kuwa kichaa mpaka kifo kilipomkuta kwa uzee miaka ya 2010+(R.I.P)

Mdogo wake Ali Mapanga Melele alibahati kusoma huko makerere na baadae ulaya kisha akaajiriwa na Tanzania harbour's Authority kipindi hicho akiwa kama principal public relation officer nafasi ambayo alitumikia mpaka mwaka 2006 Mungu alipoamua kumchukua (R.I.P)

Mtoto wake mwengine nae alisoma na akaangukia kuwa manager wa National Milling Corporation (NMC.
Huyu nae alishatangulia mbele za haki.(R.I.P)

Watoto wengine sitasema kitu juu yao maana bado wapo hai

Mzee Mapanga baada ya kustaafu kazi yake alibakia kuendelea na ufugaji na kilimo..alikuwa ni mfugaji mkubwa ambaye alikuwa na ng'ombe zaid ya 200.
Akiwa anaishi na wake zake hawa wawili yaani mtu na Dada yake siku moja aliamua kwenda kuchunga ng'ombe zake mwenyewe..

Kwa mujibu wa msimuliaji asema ilikua asubh kuna mbwa alikwenda maeneo lilipo zizi lake la ng'ombe ,yule mbwa hakuwa wa pale wala hakuna aliyemjua, akanunusa pale zizini na kutokomea uelekeo ambao ndipo wanapochungiaga.

Bahati mzuri palikuwa na mgeni pale kwa yule mzee , yule mgeni alikuwa ni mzee kuliko mzee Mapanga mwenyewe.
Yule mgeni akamtahadharisha Mzee Mapanga kwamba asiende kuchungia upande ule ambao yule mbwa ameelekea kwa madai yakuwa yule mbwa hakuja kwa uzuri.

Mzee Mapanga akajibu kwa dharau kubwa," na kwenda huko huko hakuna watakachonifanya"

Mzee Mapanga kwa jeuri akachukua gobole lake na binti yake wa kwanza kwa yule mkewe wa mwisho wakaelekea machungajini.

Majira ya mchana yule binti mwenye umri wa miaka 8 akarudi mbio na kutoa taarifa kuwa baba yake alivamiwa na majambazi na wamemkatata kwa mapanga.

Makelele yakuomba msaada yakapigwa watu wakaingia porini kutafuta mwili wa mzee Mapanga..

Baada ya muda mzee Mapanga akapatikana akiwa amekatwa mapanga kichwa huko damu nyingi zikimvuja wakati huo akiwa hana fahamu...
................
Nini kiliendelea je mzee Mapanga alipona? Ng'ombe zake zilipatikana ?/na je kina nani wali husika na tukio hilo usikose sehemu ijayo .
 
Na mdogo wake huyo mgonjwa wa akili yupo nafikiri
we unawajua au umehadithiwa tu?
Mimi nipo bandari namjua vzr sana , huyo mgonjwa wa aliki hakuwa mdogo wake yule alikuwa ni kaka yake lkn kwa bahati mbaya nayeye pia alishatangulia mbele za haki
 
Back
Top Bottom