Namkumbuka Sana Mkapa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Namkumbuka Sana Mkapa!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Buchanan, Aug 21, 2011.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Aug 21, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  1. Ali-maintain inflation tangu aingie Ikulu mpaka anatoka,
  2. Aliwezesha nchi kujenga barabara kwa fedha za ndani,
  3. Makusanyo ya kodi yalipanda kwa kasi sana,
  4. Heshima ya Serikali ilirudi,
  5. Alitujengea uwanja mpya wa soka,
  6. Alijenga daraja la Mkapa lililoshindikana tangu uhuru,
  7. Alianzisha mpango wa MMEM na MMES ili kuinua Elimu ya Msingi na Sekondari,
  8. Alianza kujenga Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),
  9. Alikuwa ni mtu wa msimamo,
  10. Nk.
  Hongera sana Ben, wenzako tunaumia sana kwa kuwa hatuna kiongozi kwa sasa, tunajiongoza wenyewe, lakini Historia itakukumbuka kwa mazuri uliyoifanyia nchi yetu, japokuwa wengi wetu hukumbuka mabaya kuliko mazuri, mimi nimeamua kukumbuka mazuri tu!
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ukitrace mwalimu alikuwa okey lafu tukadorola alpokuja mwinyi then tukapanda enzi za mkapa sasa kaja uyu ndugu yetu kila kitu FYONGO
  Ila trend analysis inaonesha atakaekuja atakuwa okey pia ivyo tuwe wavumilivu!
   
 3. I

  ITSNOTOK Member

  #3
  Aug 21, 2011
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  alijitahidi sana kama ulivyosema, mapato, inflation kudhibitiwa, tulisamehewa madeni kwa kufanya vizuri n.k.
  Lakini kuna watu wanamlaumu kwa ubabe, kuficha taarifa, mikataba mibovu, kulinda wezi, rada, ndege ya raisi hata kama wananchi wanakufa kwa njaa lazima ndege inunuliwe, majambazi yaliyokithiri, zanzibar 1995? ............. masuala ya akin zmbe, majita...............!
   
 4. N

  Nonda JF-Expert Member

  #4
  Aug 21, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Naongezea orodha yako

  - EPA
  - Aliimarisha ATCL
  - Umeme wa dharura, emergency generators
  - Ubinafsishaji wa NBC na takataka nyengine ikiwemi KIWIRA
  - Kuwawezesha wazawa kumiliki nguzo za uchumi wa nchi
  - Uhuru zaidi kwa vyombo vya habari
  - Kunyanyua kipato cha kila kaya na mafao ya jamii(social benefits)
  - Kaondosha uchangiaji wa wananchi katika huduma za jamii
  - kuimarisha kilimo na mifugo
  - kuendelea kupokea 3% katika machimbo ya madini
  - Lakini kubwa na zuri kuliko yote, kuhakikisha mwanaccm Kikwete anakuwa Rais atakayemrithi ili kuendelea kuiletea maendeleo Tanzania.

  Yes, tumpongeze kwa mission accomplished! Maisha bora kwa kila mtanzania.
   
 5. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #5
  Aug 22, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Alifuta kodi ya kichwa. Wakati anaingia madarakani alikuta nchi ipo katika hali mbaya, wananchi wanalipia hadi baiskeli. Listi ya kulipia kodi ilikuwa ni lazima utembee nayo utafikiri unatembea na kitambulisho cha taifa. Mkapa is a hero, alirahisisha sana maisha ya watanzania.

  Tuombe Mungu atakayekuja awe Mkristo, labda atairudisha nchi kwenye hadhi yake. Wakichukua tena waislamu, hapo lazima tupige nchi mnada. Maana kwa takwimu jinsi zilivyo ni kwamba kila nchi inapokuwa mikononi mwa Mwislamu mambo yanakwenda hovyo sana.
   
 6. N

  Nonda JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu
  naheshimu mawazo yako lakini naona kuna twist kali na mbaya katika hoja yako.

  Viongozi waliongoza nchi hii wote ni wanaccm. Na CCM wana sera zao. sasa hapa ukristo na uislamu unaingiaje?
  Kiongozi wa CCM ,akiwa mkristo au muislamu huwa wana tofauti ipi?

  Tusitumie imani za dini katika uongozi wa nchi. Nchi tayari iko shaghala baghala, tokea Nyerere hadi leo kikwete , tunaahidiwa maisha bora kwa kila mtanzania. Tunaishi kwa matumaini na ahadi hewa. Tukiingiza dini na imani za dini, tutazidi kuibomoa nchi hii na kubomoa ni rahisi na wepesi kuliko kuijenga.

  Tuchague viongozi kutokana na sera zao na sio imani zao za dini. Tukishawachagua tuhakikishe wanawajibika na tunawawajibisha.

  Tusiende njia ya imani za dini katika nchi yenye watu wa imani tofauti. Imani za dini ni time bomb. Tuonyane, tusiende huko.
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  mkapa hakujenga UDOM

  weka facts zako vizuri....
  ndo maana chadema ilani yao ya 2005 walisema dodoma iwe kitivo cha elimu
  na chamwino iwe chuo kikuu
  kikwete alipofanikisha hilo wakasema kawaaibia ilani yao...
   
 8. K

  KAMALELA JF-Expert Member

  #8
  Aug 22, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 213
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Acha mambo ya udini wewe, JK ni akili yake mbovu na wala sio dini yake si tabia nzuri kumuhukumu mtu kwa dini yake. Hao walikosea ni kwasababu ya mapungufu yao ya kibinadamu na wala si kwasababu ya dini yao, na hata Mkapa unayemsifia aliweza kwa juhudi zake binafusi na pengine washauri wazuri aliokuwa nao wakatio ule. Hivi unawazungumziaje akina Edward Lowassa, Andrew Chenge, Liumba, Balali nawengine ambao wamefanya ovyo? je wameyafanya hayo kwasababu ya dini yao? BADILIKA NDUGU YANGU.
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Aug 22, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hivi ujenzi wa UDOM ulikuwemo kwenye ilani ya CCM? Au ilikuwa mojawapo ya kauli mbiu za maisha bora kwa kila Mtanzania? Just asking!
   
 10. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #10
  Aug 22, 2011
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Jamani tuwe waungwana na tusweke Dini kama kitengo cha kumjua nani raisi bora. Mimi ni mkristo mwenye siasa kali sana lakini kipenzi changu ni kikwete kwa sababu ya malezi mazuri ya vijana wenye vipaji vyao. Namsifia sana mkapa kwa mazuri, yote yaliyotajwa hapo juu. Kikwete kapeleka sana vijana secondari. Ile hali ya vijana wa kimasikini kurudia rudia dalasa la saba mara zaidi ya moja imekwisha sasa. Elimu ya secondari na ya vyuo vikuu kugawiwa kwa walio wengi wengi ni hatua kubwa sana ya kimaendeleo.

  haya mambo ya bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu yangekuwa tangia tunapata uhuru, leo hii tungekuwa wapi kimaendeleo? Kenya, Nigeria na Uganda tungewafunika kirahisi sana. Ndio maana nawapenda sana hawa maraisi. Baada ya miaka kama 20 hivi, shule zetu za misingi zitakuwa na walimu waliofuzu chuo kikuu na sio tena vyuo vya ualimu.
  Nchi siku zote hujengwa na wasomi, haya ndio mafanikio makubwa ya marekani katika kuitawala dunia.

  Halafu utaona Mkapa aliyachunia sana matatitizo ya nchi za africa na aliweka mkazo sana kuyajua matatitizo sugu yetu na matokeo yake ni kama jinsi alivyosifiwa hapo juu kolamu ya kwanza! Nafurahigi sana kama mazuri ya mkapa yanatambuliwa!
   
 11. I

  ITSNOTOK Member

  #11
  Aug 22, 2011
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli alifuta kodi ya kichwa, aliikuta nchi kwenye hali mbaya, wananchi wanalipa hadi baiskeli- nakumbuka nilikamatwa siku moja. Ingawa bado ninafikiria sana kumwita hero. Sina haja ya kuchallenge ufutaji wa kodi hizo, ingawa kama utakumbuka hii ilikuwa ni hoja nadhani ya NCCR kwa muda huo kipindi cha kampeni. Wakati huo chama cha mkapa kilikuwa kinaeneza kuwa wapinzani waache uongo kwa kuwa ni lazima kodi hizo zikusanywe ili kuendesha nchi, ingawa baadae walikubali kufuta- napongeza kwa hatua hiyo sipo kinyume na maendeleo, na ningependa waendelee wengine hivyo.
  Lakini umeona hoja zilizotajwa na wachangiaji hapa, na wewe hebu endelea kufuatilia zaidi ya kodi za kichwa na baiskeli- ni vizuri ndiyo, lakini siyo kila kitu.

  Ila kwa mawazo yangu, ulipoingia kwenye udini umenipoteza kabisa, ninashauri, tusitaje maswala ya udini kwa upande hasi, si nzuri kabisa katika maendeleo yetu wenyewe.
   
Loading...