Namchukia sana huyu mama wa kambo

The unpaid Seller

JF-Expert Member
Oct 27, 2019
1,876
5,443
Peace be upon you all sons of Zion.

Baba alipomuoa huyu mwanamke na kua mama yetu wa kambo tangu mwanzo nilijua hana nia njema na sisi, kwa kumuangalia tu macho yake niliona kuna jambo haliko sawa na huyu mwanamama aliyependelea kuvalia mavazi ya gharama ila sauti ya upoleee.

Baba alipofariki ghafla eti akateuliwa kua msimamizi wa mirathi na mali za baba, hawa waliomteua kwa kufuata vipengele fulani vya sheria. Na hawa waliomteua walikua na mikwaruzano sana na baba ikisemekana walitamani kutapanya mali za baba ambazo kimsingi walirithishwa na babu.

Babu alikua mkali na daima alihimiza mali, milki na urithi vitunze mpaka kuwanufaisha wajukuu na vitukuu sasa baba nae alikua mkali kama babu ila hawa mabinamu siku zote wamekua wanazitolea macho mali zetu kwa hila mbaya.

Sasa baba alipokufa tu hawa mabinamu wakawa na ukaribu usio wa kawaida na huyu mama mke wa pili ma baba na mengi yakasikika ila hatimae tukaanza kujionea hila na mipango yao ovu.

Tukaja kusikia mama wa kambo kauza kwa siri zizi la mifugo lililokua Ngodongodo, tukasikia kauza na vifaa na vito vya thamani vya baba, akiba ya madini nk nk ila kilichotuuma zaidi mama huyu wa kambo tukasikia kauza uwanja wa wa mbele ya nyumba yetu eti mpaka baraza akauza looh

Nyumba tuliyoishi kwa kujivunia milki ya wazazi eti leo hata kupita kuingia ndani mpaka tuombe ruhusa kwa mmilike aliyenunua uwanja wa mbele na mpaka baraza yetu eti sasa ni mali ya mgeni ambae lugha yake hata akiongea hatumwelewi na hata mwandiko wake hausomeki.

Na hata alivyouza ni kwa usiri mkubwa, inasemekana aliwachukua ndugu wachache wakaenda huko wakanunuliwa soda na biskuti basi kila tukihoji kulikoni hawa ndugu walionunuliwa soda wanatukalipia eti tunyamaze mgeni aliyeuziwa uwanja na baraza yetu eti ni mtu mzuri na amenunua eti ili atusaidie !!

kweli nimeamini mama wa kambo sio mama japo baba alikua na mapungufu yake ila hakina alikua na nia ya dhati kuhakikisha mali ya familia inabaki kua ya familia, wapo wanaosema eti baba hakufa kifo cha kawaida kwamba alipumzishwa, sitaki kuamini haya maneno ila yanayotokea yananifanya kutafakari kwa kina.


hii ni simulizi ya kutunga "Mama wa Kambo" Sehemu ya 1 usikose sehemu ya 2
 
Back
Top Bottom