Mwanajamii ushauri wangu ni huu.
Jaribu kuchunguza yafuatayo ndo kiini cha gogolo hilo.
1.FINANCIAL FACTOR
2.BED ROOM FACTOR
3.RELATIVES FACTOR.
Ndoa nyingi matatizo yanaanzia hapo juu.
kwanini unahic kwamba mwenzako hakuhitaji tena? na yeye labda anahic hivyo hivyo ndio mana mnategeana nani wa kumwanza mwenzie, mmeshawahi kuongelea tofauti zenu? unajua unaelezea ki juu juu mami chanzo cha haya yote mpaka kufikia huku ni nini?
Nyamayao maisha haya yataka moyo (nimekuPM) dada huenda ukaelewa vema.
Bwana Fidel
Factors kubwa hapa financial and bedroom factor. Ukikuta mwanaume au mwanamke wanagombana hadi kuachana kwa sababu ya hizi factor mbili husishangae. Ila ukikuta wapenzi wanagombana hadi kuachana kwa factor ya relatives then wao wenyewe wana weakness kubwa kwenye mifumo yao ya maisha na utatuzi wa migogoro. Sociologically in conflict theory perspective mara nyingi ugomvi wa kimapenzi ni hulka ya mpenzi mmoja kutoridhika na kitu au jambo kutoka kwa mwenzake. Suala la mtu wa tatu kwenye theory hii linachukuliwa kama minor case kutokana na nguvu ya mapenzi ambayo hata Functional theory inazungumzia mapenzi kama sehemu muhimu sana ya kufanya muunganiko wa watu wawili au familia mbili au makabila mawili au mataifa mawili ambayo kamwe hayakuwahi kuwa na fununu za kuungana.
Kwa suala la mwenzetu hapa inabidi aangalie hizo factors mbili kama hiyo ya tatu ya relatives imeshaanza kuwa kikwazo basi hapo kuna tatizo kubwa sana zaidi ya mapenzi yenyewe, ogopa sana kuchukiwa na ndugu wa upande mmoja.
mtu ukishafikia maamuzi hayo ni kwamba ni kweli umechoshwa na hutakiwi kugeuka nyuma milele....kama kitu kimekushinda/kuchosha kwanini ung'ang'ane tu?
Mpwa bado nipo nipo kwanza ila hii through books and research.
Nyamayao maisha haya yataka moyo (nimekuPM) dada huenda ukaelewa vema.
Dada nyamayao husiseme hivyo bana (milele kabisa) unaondoa hata ule uwezekano wa EX-BF na EX-GL kujikumbushia jamani. Nway sometimes inahitaji msimamo kama huu lakini its very hard kama aliyepita alikuwa anakwea hadi juu ya mlima lakini the present anahishia upenuni mwa mlima.
Habari
Leo naungana na dada yangu Mwasity katika kile alichokiimba.....
Leo nalivua pendo, nililopenda zamani
Nabadili wangu mwendo, nami niwe furahani
Nimechoshwa na vitendo, visa na purukushani
Kweli mapenzi uvundo, apendwapo hathamini (By Mwasiti)
Hivi unapofikia hatua kama hii
1. Nini cha kufanya ili uendelee kuwa strong?
2. What to do ili isikusumbue (the quilty concious)
3. Ufanyeje ikusahaulishe mapema
Nauliza tu ndugu zangu maana...................mh
Pole MJ1, hayo ndo mapenzi,
ila kukaa mwenyewe itakugharimu sana, pumzika kidogo, kisha chukua muda kusoma mwanaume unayemtaka awe ana kupa kampani, la sivyo kila siku utakua mtu wa mawazo, that is life " Some lessons are learned through pain.Vision clears only after eyes are washed with tears.At times we have to be hurt to be stronger for life and for love"..pole ila usisononeka sana maana kusononeka ni sababu mojawapo ya kukikaribisha kifo chako
Kifaru
Aksante ndugu yangu.
Kuanza mwanzo naamini nitaweza ingawa itaniumiza sana tatizo ni moyo unauma kumwachia huyu ingawa nimefika kikomo! Najiuliza kweli nitawezamsahau kiasi cha kujikuta siku moja namkumbuka kwa maovu yake (ambayo ni mengi)?. Kusema kweli am using a lot of energy to love him, to be with him utafikiri naishi na yai bichi jinsi unavyolitunza lisidondoke au glass ya champaign siku ya arusi...... maana hutaaford kuiangusha uivunje-utapata wapi nyingine?!
Hatujatengana kwa sababu mwenzangu hajatamka hilo ila actions zake tu zainadhihirisha kuwa hanihitaji tena.
Tuko pamoja kama vile tunategeana nani aanze ili lawama ziwe juu yake.
Cha moto nakiona .... ndo maana nafikiria bora tu niamue mimi potelea mbali lawama ili nisiendelee kuteseka
Aksante Mbu maneno yako mazito ila duh ngoja nijaribu maana sina tena nguvu wala uvumilivu....mj1, "you've got to get the mind cleared out before you put the truth in it" aliyatamka hayo Louis Farrakhan.
hayo matendo unayoyaona na kuyahisi ni dhana tu! dhana humpeleka mtu motoni akaja jijutia baadae,... tafadhali clear off hiyo suspicious mind kwanza...
...unaona sasa? yeye amekutamkia au mmetamkiana "anza wewe!" ? No, ni dhana yako tu hiyo inayokupelekea huko, acha!
...hakuna cha moto wala nini, unajitia kiwewe tu kwa kuogopa kivuli! usijitishe na 'mawazo machafu' katika kipindi hiki cha gharika na mawimbi makali,.... sote tumepitia humo humo...
Ushawahi kusikia wimbo nahodha kajitosa baharini? well, hilo unalofikiria la potelea mbali 'bora ujitose baharini' liachie huko huko mawazoni, usilitende tafadhali. Madhara yake ni mazito kuliko unavyofikiri.
Unaacha usalama wa chombo unajitosa baharini kwenye papa na nyangumi? malenga wetu walisema "pupwe lina msisimo kwenye kondoo wenye manyoya haba!"... jivishe gamba la kobe! kama hakutaki mwache yeye ndiye akutamkie!
Halafu hayo mateso, au kuendelea kuteseka ni mambo ya kujitakia!
Epukana na mazoea,... "a bird in hand" ndugu yangu, kuwa mwangalifu.
Mnapitia kwenye dhoruba tu za mapenzi, usiachie nanga!
...Kuanza mwanzo naamini nitaweza ingawa itaniumiza sana tatizo ni moyo unauma kumwachia huyu ingawa nimefika kikomo! Najiuliza kweli nitawezamsahau kiasi cha kujikuta siku moja namkumbuka kwa maovu yake (ambayo ni mengi)?. Kusema kweli am using a lot of energy to love him, to be with him utafikiri naishi na yai bichi jinsi unavyolitunza lisidondoke au glass ya champaign siku ya arusi...... maana hutaaford kuiangusha uivunje-utapata wapi nyingine?!
Aksante Mbu maneno yako mazito ila duh ngoja nijaribu maana sina tena nguvu wala uvumilivu.