Subira the princess
JF-Expert Member
- Mar 3, 2018
- 4,465
- 4,613
Wasalaam.
Kama taifa ni kama tumepoteza dira na matumaini kwani miongoni mwetu tunaishi na manung'uniko, visasi, uhasama, dhulma, na kuombeana hata vifo na kupambikiana kesi za kipuuzi. Ukweli mchungu ni kwamba chama cha mapinduzi ndio kimetufikisha hapa tulipo na tunakaribia njia panda.
Nasema CCM ndio wametuchimbia shimo kubwa kwa sababu moja tu, wametunga sheria kandamizi dhidi ya raia ambazo zinatesa na kuleta upendeleo kwa maslahi ya kundi fulani ndani ya CCM. Mfano wa sheria kandamizi ni kama hii ya tozo kwenye simu na hii ya kodi ya jengo kwenye luku, maana hapa mpangaji ndo anaelipia mwenye nyumba.
ccm hawa ndo wametufikisha hapa.
CCM hawahawa wamezuia upatikanaji wa katiba ya wananchi kwani iliopo ni chama kimoja ambayo waliotunga hawafiki watu mia moja, na inawanufaisha viongoz walafi wa CCM ambao wamejiwekea kinga ya kutoshtakiwa milele hata wakiiba au kuua raia.
Hitimisho: Watanzania tunaangamia kwa kukosa maarifa na hakuna wakuokoa katika hili ila sisi wenyewe tutakaporudiwa na ufahamu, kwani ni kama tumezimia tumepoteza fahamu.