Naliona anguko la Kibanda

Everyday, now & then, we said here JF, most journalists including this one, are stupid, waganga njaa, illeterate, arrogant & ignorant too,
it doesn't matter how long he has been writting articles, he thinks using his foolish, idiot mind can convince or persuade all of us kwa issue
ya UWIZI MKUBWA wa wazi kama wa DOWANS, as i said ni ujinga wake unamsumbua, he is dirty to discuss him, Prostitution of journalism, hana lolote
hana uzalendo ( Patriotism)
 
Kuna Mzungu mmoja alishawahi sema kuwa ukitaka kumwibia au kumtia mtu mweusi matatani basi uweke mambo kwenye maandishi maana wana uvivu wa kusoma wanapenda vitu vya mkato visivyohitaji kutumia akili na kutafakari. Nikiangalia comments za watu hapa ina-justfy usemi huo. Watu wengi wanapenda ready made kutumia mda kudadasua hawataki,na hii inatokana na uvivu wa watu walio wengi kutokuwa na tabia ya kusoma vitabu. Iwe na vyuoni ni madesa tu mpaka humu kwenye JF wanaendeleza uchovu wao. Ndiyo maana hata wakuu wetu wanasaini mikataba bila hata ya kuisoma na mwishowe tunatiwa matatani. Mtu kusoma page 2 tu mchovu anataka apewe summary, kazi kweli kweli na Poleni sana.
 
Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Absalom Kibanda, anafanya kazi part-time kwenye magazine inayomilikiwa na Edward Lowassa inaitwa UMOJA. Pia Kibanda amekuwa anatoa habari za kumbeba Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge kwenye Tanzania Daima mara nyingi. Kwa kupokea maagizo na malipo kutoka kwa Lowassa na Rostam Aziz, Kibanda pia amekuwa akiandika habari na makala nyingi za kuwakashifu Samuel Sitta, Harisson Mwakyembe, Bernard Membe na John Magufuli.

Tanzania Daima ni moja ya magazeti yanayotumiwa na fisadi Rostam Aziz kutetea ufisadi mbalimbali, ikiwemo malipo kwa Dowans kwa nguvu zote. Wanaitumia Tanzania Daima kwa kuwa gazeti linaaminika kuwa ni huru na ni rahisi ku-brain wash watu kuliko kutumia Mtanzania/Rai ambayo Watanzania hawayasomi tena sasa baada ya kugundua kuwa yanamilikiwa na Rostam.

Cha kushangaza ni kuwa mmiliki wa Tanzania Daima, Freeman Mbowe, anaachia tu gazeti lake litumiwe na mafisadi kupitia kwa Kibanda kuangamiza nchi.
 
Mh nina wasiwasi ,mi ni msomaji wa Makala za Kibanda sioni dalili za kuchakuchuliwa!kama ndivyo basi Tnzania DAIMA YOTE!ALICHOJADILI mhariri ni kuhusu msimamo wa Sitta ,kwamba kama anajibainisha kuwa ni mpambanaji kwa nini yupo katika hilo kundi !na alisema kama yeye angekuwa ni Rais/waziri mkuu angemfukuza kazi,Kumbukeni anasema aangekuwa ni Kikwete au Pinda na kwa mazingira ya leo!Nani asiye jua kuwa watu wadilifu wanapoona wameingia sehemu isiyofaa hutoka haraka.inawezekana bwana mhariri anlitumia lugha kali !lakini ujumbe wake ni muafaka.Kumbekeni ni mojawapo wa waandishi aliyesimama thabiti kwa uwazi na hakutetereka kuonesha kuwa Kiwete alaikuwa anapewa sifa asizo stahili na alionesha kutofaa kwake kuwa mkuu wetu!aliyoondika leo kuna mtu atayabishia !
 
cha msingi sitta ni mtu safi lakini yuko katika chama kibaya
 
Sitta kasema hakuna baraza la mawaziri lililokaa na kuamua dowans alipwe, asa collective responsibility ipo wapi hapa? utamfukuzaje waziri alietoa maoni yake? Absolom kachemka, inaelekea kweli yupo ndani ya payroll ya Rostam, yeye ndo anafaa atimuliwe Tanzania Daima.
 

Kibanda ameshapotea njia muda mrefu,

siku hizi amekuwa mpiga filimbi wa Lowasa, Rostam, Karamagi & co. wakati huo huo yuko busy kuwakashifu na kuwaandika vibaya Mzee Sita , Mwakyembe & co.

Kama Mmmiliki wa tanzania daima hatochukua hatua za haraka na za makusudi kumuondoa kibanda(sijui ni cha nyasi ama makuti) basi ajue kwamba tanzania daima litaanza kupoteza wasomaji na kubakia kama magazeti ya fisadi "habari corp".

Vinginevyo basi na yeye atakuwa amejiandaa kutoa ruzuku kwa ajili ya uendeshaji wa gazeti lake litakavyokosa soko na kudoda vibandani.
 
Mhariri anakuwaje msemaji wa watanzania? Mtu kuwa muandishi wa habari haikupi mamlaka ya kuwa muamuzi kwa niaba ya wengine. Kibanda amekosea kumshambulia Sitta.

Kuhusu wachangiaji wanaolalamika kuhusu mada kuwa ndefu kuna mada fupi kwenye forum ya 'jokes'. Pia kuna mada zinazovutia kwenye forum ya 'mapenzi'.
 
Tatizo nililoliona siyo urefu bali font ndogo kiasi cha kuumiza macho.

 


Kama hajachakachuliwa, mbona siku hizi yuko busy kutuandikia habari za Lowasa?? hata gazeti la uhuru halimpi coverage yoyote Lowasa lakini Kibanda siku hizi imekuwa bandika bandua Lowasa hakosi kwenye front page.

Ni dhahiri kwamba kibanda ameshachakachuliwa, na siku zake zinahesabika, yuko njiani kuelekea kwa bosi wake muya fisadi papa

si umeona kuna mhariri mmoja tayari ameshachoropoka na kuingia zizini?
 
Nimeisoma Makala yako hii ndefu na kugundua kwamba ina weledi wa hali ya juu na ni nzuri sana. Sasa nimemuelewa vema kibanda-na kikoba chake alichokabidhiwa! DOWANS HAKUNA KUKUBALI mpaka kieleweke. BIG up 6, usikate tamaa, najua mafisadi watalipa watu wengi sana kujitakasa wakiwemo wanasheria wawapigie debe kama BOMANI! Lakini mwisho wa habari-DAMU YA WATANZANIA ITAWASUTA HATA MKIWA KABURINI!!!
 

Umesema yote kamanda.
Ang'olewe tu Tz Daima, aende rasmi kwa Rostam na Lowassa au kwa Ridhiwani (Jambo Leo) ili awe wazi. Kama vp aende Uhuru au Habari Leo.
Vinginevyo anakuwa anaharibu from within.
Credibility ya magazeti ya mafisadi ni ndogo ndiyo sababu wanatafuta wahariri wa magazeti mengine. Lets be vigilant!

Mambo ya kuwasifia Rostam, Lowassa, Chenge na kuwakashifu Sitta, Dk Magufuli, Dk Mwakyembe na Membe sanasana yanamuonyesha muandika makala hizo jinsi alivyonunuliwa.

Kuhusu hiyo makala, si ndefu kiasi cha kumfanya msomaji makini achoke. Tuwe na utamaduni wa kusoma na kujisomea!
 
bandikeni alichoandika Kibanda la sivyo acheni ngojera humu

Tatizo kubwa letu hatupendi kufanya tafiti hilo gazeti nami nililisoma na kustaajabika sana kuhusu huyo kibanda na sasa nanyi mwashindwa elewa au hamkununua gazeti hilo okay me ninalo kesho ntali post hapa maana mwenzenu kachukua kwa ufupi tu na kutupa dondoo zake na alicho kisema ni kweli huyo mhariri Kibanda alichemka kubwa pamoja na ni mawazo yake ila yameendea kushoto sana

 
Sitta si safi na kama safi angeruhusu mjadala wa Richmond uendelee mpaka kuparta muafaka bungeni na kwa hesabu tu marupurupu ya Spika yanazidi ya Uwaziri alionao ndo maana anakurupuka.
Sikatai anasema jambo jema lakini wasiwasi wetu wananchi ni kwamba hizi ni hasira za kuukosa uspika.
Kama safi ahame chama maana kinanuka
 
laiti kama sitta angeruhusu kifikiwa kwa maazimio ya bunge leo hii tusingekuwa na dowans,kwa kuogopa kwake hawezi kamwe kukwepa dhambi hii....tafakari
 
SITTA SHUJAA WA WATANZANIA.

Nampongeza sana kwa kuwa ndiye mtu pekee anayesimamia ukweli mpaka sasa. Najua fika kuwa sita analijua suala la DOWANS vizuri

kuliko mtu yeyote. DOWANS ni mafisadi wapo hapa hapa na pengine wapo ikulu. Ipo siku watachomwa moto kule mbinguni mana

mungu kasikia kilio chetu cha kulala gizani ana watoto wetu wanakufa kwa ajili ya joto la dar.
 
Kibanda, Kibanda wait and see lakini ameshanunuliwa
 
watu wanachoka kusoma summarize

Mkuu kwani wewe unamsemea nani hapa? Sema umechoka kusoma usiseme tumechoka, wewe na nani? Au ndo hivyo unajaribu kufanya kazi uliyotumwa kuifanya? "Motion neutralizer"?.

Huyu mwandishi naona ameamua kumpiga nyoka Kibanda kichwa ili kummaliza kabisa wala hakupiga mkia hata kidogo. Kina Kibanda ndio waandishi uchwara wanaotetea upumbavu katika nchi hii eti kwa kuwa wamekatiwa kitu kidogo. Hata wakifanya nini malipo hayo hayatafanyika. Ngoja tusubiri kauli ya JK juu ya hili.

Tiba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…