Nakupenda Sana Lakini Ukiendelea Hivi Nakutema! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nakupenda Sana Lakini Ukiendelea Hivi Nakutema!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by The Analyst, Jun 10, 2011.

 1. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  We mwanamke vipi?
  Ulipotendwa na mpenzi wako wa awali mimi ndiyo nilikuwa faraja yako kuu....Usikatae!..Mwenyewe uliniambia, tena machozi yakikutoka...

  Hujawahi kuona mtu mwenye hekima kama mimi... ulisema. "Usijali!" nikakwambia.... Utapata mwingine tena bora kuliko yeye ukasema....Inshallah!

  Kila kitu ulinisimulia.... Usibishe!...Sikukuuliza wala kukuomba. Nilijua jamaa alikuchukulia for granted na kukupuuza kabla hajapata mwingine na kukuacha kwa dharau tena kubwa. Ukabakia mpweeeeeke... Dunia ikajua. Baadhi wakakupa pole na wengine kukudhihaki... Heheeeee...! Ulidhani atakuoa?.... Kamwacha JLo atakuoa wewe?

  Peke yangu nilihisi unavyoumia... nikaona ni vema nikutoe kwenye machungu...si kwa malove wala sex...nilitumia hekima kidogo niliyojaliwa....ikakuingia ukapata matumaini mapya...ukanishukuru....Taratibu ukanizoe, ukanithamini na ukanipenda...Ndiyo! mwenyewe ulinisimulia.

  Ulitaka kujua kwa nini sipendi kutoka na wewe nikasema siwezi!....kwa nini?....Sitoki peke yangu nitaweza vipi kutoka na wewe? Mimi ni selfish. I only care for myself. Ukabisha sana na kudai ningekuwa mbinafsi nisingekuonea huruma ulipokuwa unaumia kwa kupuuzwa na mshikaji wako. Hata hivyo tuliendelea kuzoeana....

  Baada ya mazoea kuzidi ukaipotezea soo na kuamua kusema nami.... Unanipenda sana na kama kuna uwezekano japo wa mie kuendelea kukujali kama unavyoona sasa basi upo tayari kufanya lolote ili tuwe pamoja romantically. Kwa ulivyowasilisha hoja niliona sawa. Kama ninayemlilia siku nyingi anajikweza na kuniringia kwa nini nisiwe na wewe (unayedai kunipenda)? Mmmh...! Mapenzi bana!

  Nikagundua ulivyo mwema na mzuri from the inside..... Nikakupenda zaidi hata ukajua na kudeka. Pamoja tukafurahi.
  "Sijawahi kupendwa kama unavyonipenda wewe...... Asante sana" Sikusema mimi!..... maneno yako hayo!

  >>>>>>>>>>>>Niombe nini zaidi?...Nikapropose nawe ukakubali. Ukataka shela na matarumbeta...nikasema nitajitahidi. Kumbe tumesahau! Mwenzangu dini yako tofauti. Kwa upole nikakuomba ujitolee japo kwa hilo nami nitakukumbuka daima.....ukasema no, labda mie ndo nibadili kukufuata nikasema ni ngumu kwa kuwa nilisoma kwa mchango wa waumini wa dini yangu so.... siwezi kuwakimbia kwa sasa japokuwa huwa sidharau dini ya mtu. (Moyoni mwangu Mungu kwanza kisha, watu halafu dini inafuata). Ikawa ngumu.

  Tukaibuka na mseto na kuanza maisha ya pamoja.

  Kila unaloamua hakuna anayeweza kukushauri tofauti. Hata mimi niliyekupenda ukanisifu leo hii siwezi kukubadili tena. Nahisi umeota mapembe. Upole uliokuwa nao awali wote umetoweka.....sina raha tena.

  Umeanza kutoka na wafanyakazi wenzako (ninapokuwa mbali ktk kutafuta riziki) hadi wake zao wanakushutumu...Nimekukanya weeeeh! ukasema huwezi kuacha kutoka na jamaa zako eti tu kwa kuwa mimi na weke zao tunakutaka uache......we mwanamke mbaya wewe...! Na mengine ya jeuri umeyasema nikakuangaliaaaaaaa........! nikasema poa. Sasa nimechoka na kuamua kukupuuza....! Sina cha kukwambia na sihitaji... After all bado hutanisikiliza wala kubadilika (eti kwa kuwa tu nimesema..) au siyo? Okey! Nakuachia nyumba.. mie huyoooo!

  Nashukuru Mungu, nimeamua kuendelea na yangu mambo... Cha ajabu sijui umetoswa na jamaa zako au vipi unaanza kurejea na kusisitiza ninavyopaswa kuwa.... Mara unakagua simu zangu,...mara unahoji kwa nini bado ninawasiliana na wa-zamani wakati ulinikataza, mara unataka niache kutumia Internet mara ooh! siku hizi sikupendi, mara mbona sina wivu, mara ooh inaelekea wanawake wenzako wamekuzidi....Nimekwambia hata hayo uyaache pia kwa kuwa hayasaidiii kuondoa vurugu uliyoanzisha mwenyewe kwa jeuri yako.... Bado unaendelea...

  Unajua nini?....Naudhika zaidi. Bora kuwa mpole na mnyenyekevu ili moyo urejee taratibu maana bahati uliyonayo ni kubwa bado sijampenda mwingine kufikia kiwango chako..Nahisi ukiendelea kunikera atapatikana.

  Unakumbuka siku uliyopokea simu yangu nilipopigiwa na binti wa kampuni ya simu ukaishia kutukanwa?... Ulipaswa ujifunze kuanzia hapo, lakini wapi! Juzi tunavuka barabara mie na mizigo wewe na watoto (2) nakwambia washike mikono ukakubali lakini ukaendelea kuchezea simu (kama mtoto wa shule). Kama si kasi yangu kutupa mizigo chini na kumuwahi last born pengine tusingekuwa naye leo maana, mtoto kakimbilia barabarani wakati dereva mmoja kakanyaga mafuta ya GX100 yake mpaka basi. Gari imechanachana mifuko mpaka hakuna cha kuokoa. Jambo la kusikitisha unanilaumu eti uoga wangu perfumes zako zimegongwa na gari. Bitch (Sorry..wakuu).. una laana.
  Nisiseme sana mwisho watu watajua siri zetu.

  Ninachokusudia kukwambia leo ni hivi. Inawezekana kweli ile roho ya kukupenda saaaaaaaana imekufa lakini ya kukupenda kuliko wengine bado ipo ndiyo maana sijakuacha. Sasa nasema next time nakwambia kitu cha msingi kama uhai wa mtoto unaniletea ubishi au mapozi. Sikufichi. That time nakutema hapo hapo na hutaamini maana hutakaa unishawishi chochote tena.

  Na mambo ya kujaribu kunidhibiti yananibore kishenzi! Mpaka sasa mademu wa nje sina, na sina mpango wa kutafuta. Unapoona sikujali ni kwa sababu jeuri yako hunikera kiasi cha kufanya nione kama mahusiano ya kijinsia ni vurugu tupu na hivyo kujikita kwenye utafutaji. Nitaendelea kutumia Internet na hutanilazimisha kuja kitandani kama sijisikii. Kimsingi hata mimi kwa sasa siwezi kufanya kila ukitakacho eti kwa kuwa tu umesema. He he he he heeeeeh! Inauma eeh...? Umeanza wewe mie namaliza.

  SITANII... UKIENDELEA NA UPUUZI NAKUACHA HATA KAMA ITANIGHARIMU....!
   
 2. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,339
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  hii ni hadithi ya bulicheka au abunuasi?
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,221
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Nimepotea....
   
 4. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,085
  Likes Received: 2,961
  Trophy Points: 280
  Mh!!Kazi kwelikweli!
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Jun 10, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,534
  Likes Received: 21,013
  Trophy Points: 280
  ahhhhhhhhhhhhhh
   
 6. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #6
  Jun 10, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,711
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160

  ...duuhhh, endelea tu kaka..."jipu hilo! kamua!....!"...nakusoma nikikusikiliza...
   
 7. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Mbona kawaida yako?

   
 8. jockey emmanuel

  jockey emmanuel JF-Expert Member

  #8
  Jun 10, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 330
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mapenzi mapenzi...ni kitu gani?endelea tu kaka...napenda kuckia zle ctor za 'mapenzi yanautesa moyo wee...'
   
 9. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #9
  Jun 10, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,221
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Huhhh?!
   
 10. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #10
  Jun 10, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Sijui kwa nini lakini natamani ungeandika mawazo yako kidogo zaidi ya hapo.
   
 11. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #11
  Jun 10, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Nipeni mawazo niandike hadithi mwenzenu!

   
 12. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #12
  Jun 10, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Imeandikwa na The Analyst.

   
 13. MUREFU

  MUREFU JF-Expert Member

  #13
  Jun 10, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,230
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  sijaelewa?
   
 14. MTAMBOKITAMBO

  MTAMBOKITAMBO Senior Member

  #14
  Jun 10, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  DAH!Kama ni kweli yamekutokea hayo,mh!Umeipangilia vizuri mno hapo,nahisi kuna ukweli umefichwa,ts too perfect to be true!Ni kama tamthilia,hakuna makosa,hii kweli ni stori(Isidingo).
  Kwa story unaweza kutunga mkuu,salute!
   
 15. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #15
  Jun 10, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Usishangae maana hata mimi sijaelewa kitu! Ninakusudia kuchokoza mjadala mrefu kwa kutoa malalamiko ya mshikaji katika format ya "Barua simulizi" Upo hapo? Bahati isiyo nzuri wengi wetu hatupendi kusoma threads ndefu so, nikaamua kuikatisha ili nipate maoni ya wadau kabla ya kuendelea. Wasipoitaka nitauchuna na kupoteza time kidogo Jukwaa la Siasa.

   
 16. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #16
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,774
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 180
  huo ni wimbo?
  Summarize kidogo maana ndefu hiyo kama mkataba wa madini. Lol.
   
 17. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #17
  Jun 11, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,641
  Likes Received: 562
  Trophy Points: 280
  Interesting but sijaelewa conclusion itakuwa amekucheat au ?
   
 18. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #18
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Pole my dear.
  I can only offer you the long one. Ndiyo majaaliwa. Yangu ndefu 'vo sa' n'tafanya n'. It's just the beggining of a very long discussion.

   
 19. Uda'a

  Uda'a JF-Expert Member

  #19
  Jun 11, 2011
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 221
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ehh hii kama ni story, bac una kipaj ndugu,,
  Nilivyomvivu kusoma eti nimesoma yote kha!

  Hapo kwenye 'ajali mhh umenigusa,,
   
 20. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #20
  Jun 11, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,041
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  mie ndo sioni kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
Loading...