Nakupenda Sana Lakini Ukiendelea Hivi Nakutema!

Thanx One and Only. Ni kweli wewe ni miongoni mwa wachache. Kwa jinsi ulivyonipa moyo hapa naanza kujiona na kijarida changu cha mara moja kwa mwezi kikiwa na maandishi makuuuubwa juu! The Analyst Monthly Magazine. Ndani full true stories .......! Just dreaming!

I can see shigongo in trouble, bonge la utunzi, ujumbe umeifikia hadhara bila vikwazo
 
Mkuu Mbu, ushauri wako umetulia sana, Thanx.
Jambo nililogundua mwanamke amegundua mema aliyoyafuja wakati ule na anachokikosa muda huu yanafanana kwa kila kitu. In brief she is more in love right now than ever before. Anatamani mshikaji ampende na kujali kama ilivyokuwa awali lakini mshikaji hana time hizo. Hajui amrejeshe vipi katika tabia zake za mwanzo ndiyo maana anafanya vituko vingine hata kuonekana chizi. Huwezi kuniamini nikisema hata mimi nafurahi Shem wangu anavyoteseka kwa sasa maana jeuri ilikuwa kubwa mno kwa jamaa. I know this guy so well na katika swala la utu anajali sana. Anapolalamika kwamba alimwonya na kumwambia madhara ya kiburi, jeuri na ukaidi wake naamini 1kwa1 maana hata tulipokuwa shule hakuwa mtu wa kuhukumu wenzake haraka kabla hajajaribu kuwaasa.
Unajua watu wengine wanafikiri anayependa na kujali sana ni mnyonge katika uhusiano na kumbe si lazima. Kuna watu marketability zao kwa watu wa opposite sex iko juu sana lakini huwakuti wakiwadharau wapenzi wao lakini cha ajabu unamkuta mpenzi wake, ambaye unaona wazi hata akitemwa hatapata mtu wa kujicommit kwake seriously kwa haraka, anamringia mtu wa aina hii na si kwa kuwa hampendi bali kwa kuwa anajua mshikaji anampenda sana na hasikii la mtu juu yake. Wanasema mambo hayo kwa mashost wao sometimes.
Jamaa mwenyewe anasema kungekuwa na mwanamke mwingine ambaye kamvutia basi (kwa kumkomoa mkewe) huu ndio ulikuwa wakati wa kujiacha wazi lakini anaseme kwa sasa anachofurahia zaidi ni kukua kwa shughuli zake za kiuchumi wakati anashuhudia ukuaji wa wanae. Siku nitakayozungumza na shem na kumshauri kutulia kwanza nitakujulisha hata ikiwa ni kwa PM.


...Ushauri wangu Bw Analyst, wawili hawa ni bora kuachana.

Mume keshageuka jiwe, na mke huyo alisha m discredit huyo mume siku nyingi.
Hapo kinachobembelezewa sio mume abadilike, bali awe mpole tena (mw'mke) aendelee na kujiliwaza kwake.

kama ulinisoma kwenye 'chupa mpya mvinyo ule ule' nimetoa changamoto watu tujiangalie nafsi zetu tunakosea wapi,
lkabla hatujaanza walaumu weza wetu.

Umeielezea vizuri sana mada hii, kiasi hata mimi nimejiona kumbe siko peke yangu na maswahiba haya,
lakini ukweli utabakia ukweli tu. Haiwezekani Mke akaanza visa na vituko iwapo tangia mwanzo uliweka msisitizo
mambo ambayo hayapendezi kufanyiana.

Haiwezekani Mke akaendelea na vituko, ila tu nawe unapojhikubalisha hali hiyo iendelee. Nimeandika hata mimi
nilipitia huko. Nilidhani kwa kumpa nafasi nyingine tena na tena baada ya kufanyiwa makosa makubwa ilikuwa sahihi
kwakuwa nilijifariji hakuna mkamilifu. Hivi leo nikikaa na kufikiria mke alitoa mimba ya mshkaji, halafu baada ya kupona akaanza uhusiano wa kimapenzi na dakitari huyo aliyemtoa mimba, ....kwakweli leo hii nikijifikiria najiona kweli nilimuamini kijinga.

Achana nae bana, Mwanaume ukisdhageuka jiwe ndio imekwisha hiyo. Kuishi na mtu for the sdake of children hainiingii akilini.
Tokea hapo mlishakuwa mna lack effective communication ndani ya ndoa, hilo jiwe na visasi moyoni mlipuko wake
hautokuwa mzuri hata kidogo. Mwanamke huyo (kama aliyekuwa wangu) keshazoea kutishiwa nyau....

Move on!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Tutatoka kwenye mada bure Honey! Nimeelezea mazingira ya kisa hiki katika baadhi ya post nilizofanikiwa kujibu hapo awali. Post yako hii inanitatiza kidogo maana, inaonekana unaamini kujua sana tabia za wanaume, kitu ambacho nitakubishia hadi naenda kaburini. Wanawake kama walivyo wanaume bado hawajaweza kuzijua tabia zote za opposite gender kiasi cha kumwelezea kila mmoja kwa urahisi kama unavyojaribu kusuggest wewe. Wanaume wote wangekuwa unavyosema wewe hii thread isingeandikwa. Kama unaamini mimi ndiye mwenye mke bado si tatizo lakini huoni kama bado inapingana na imani yako juu ya wanaume? Kama mhusika mkuu ni mimi ina maana tayari nimeweka wazi yaliyonisibu the same kwa mhusika mkuu kuwa rafiki yangu wa karibu. Vyovyote vile bado inaonekana huwa tunazungumzia hata yale unayoamini mwanaume hathubutu.

Kama ulikuwa hujui wanaume tunasimuliana zaidi mambo ya mahusiano kuliko wanawake pamoja na kuwapo misemo kama "Mwanamke Umbea" ukilinganisha na madada. Kama huamini fanya utafiti kidogo tu kitaani. I tell you, utaamini maneno yangu.
Uso umeumbwa na aibu umesimulia hapa kwa uwazi sababu hatukujui, unaweza wakalisha rafiki zako ukawasimulia the same face to face?
any way pole sana kwa masahibu
 
Pole sana the Analyst,nimependa style uliyotumia kupresent thread yako maana japo ni ndefu kidogo lakini haichoshi kusoma..,kudos.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom