We mwanamke vipi?
Ulipotendwa na mpenzi wako wa awali mimi ndiyo nilikuwa faraja yako kuu....Usikatae!..Mwenyewe uliniambia, tena machozi yakikutoka...
Hujawahi kuona mtu mwenye hekima kama mimi... ulisema. "Usijali!" nikakwambia.... Utapata mwingine tena bora kuliko yeye ukasema....Inshallah!
Kila kitu ulinisimulia.... Usibishe!...Sikukuuliza wala kukuomba. Nilijua jamaa alikuchukulia for granted na kukupuuza kabla hajapata mwingine na kukuacha kwa dharau tena kubwa. Ukabakia mpweeeeeke... Dunia ikajua. Baadhi wakakupa pole na wengine kukudhihaki... Heheeeee...! Ulidhani atakuoa?.... Kamwacha JLo atakuoa wewe?
Peke yangu nilihisi unavyoumia... nikaona ni vema nikutoe kwenye machungu...si kwa malove wala sex...nilitumia hekima kidogo niliyojaliwa....ikakuingia ukapata matumaini mapya...ukanishukuru....Taratibu ukanizoe, ukanithamini na ukanipenda...Ndiyo! mwenyewe ulinisimulia.
Ulitaka kujua kwa nini sipendi kutoka na wewe nikasema siwezi!....kwa nini?....Sitoki peke yangu nitaweza vipi kutoka na wewe? Mimi ni selfish. I only care for myself. Ukabisha sana na kudai ningekuwa mbinafsi nisingekuonea huruma ulipokuwa unaumia kwa kupuuzwa na mshikaji wako. Hata hivyo tuliendelea kuzoeana....
Baada ya mazoea kuzidi ukaipotezea soo na kuamua kusema nami.... Unanipenda sana na kama kuna uwezekano japo wa mie kuendelea kukujali kama unavyoona sasa basi upo tayari kufanya lolote ili tuwe pamoja romantically. Kwa ulivyowasilisha hoja niliona sawa. Kama ninayemlilia siku nyingi anajikweza na kuniringia kwa nini nisiwe na wewe (unayedai kunipenda)? Mmmh...! Mapenzi bana!
Nikagundua ulivyo mwema na mzuri from the inside..... Nikakupenda zaidi hata ukajua na kudeka. Pamoja tukafurahi.
"Sijawahi kupendwa kama unavyonipenda wewe...... Asante sana" Sikusema mimi!..... maneno yako hayo!
>>>>>>>>>>>>Niombe nini zaidi?...Nikapropose nawe ukakubali. Ukataka shela na matarumbeta...nikasema nitajitahidi. Kumbe tumesahau! Mwenzangu dini yako tofauti. Kwa upole nikakuomba ujitolee japo kwa hilo nami nitakukumbuka daima.....ukasema no, labda mie ndo nibadili kukufuata nikasema ni ngumu kwa kuwa nilisoma kwa mchango wa waumini wa dini yangu so.... siwezi kuwakimbia kwa sasa japokuwa huwa sidharau dini ya mtu. (Moyoni mwangu Mungu kwanza kisha, watu halafu dini inafuata). Ikawa ngumu.
Tukaibuka na mseto na kuanza maisha ya pamoja.
Kila unaloamua hakuna anayeweza kukushauri tofauti. Hata mimi niliyekupenda ukanisifu leo hii siwezi kukubadili tena. Nahisi umeota mapembe. Upole uliokuwa nao awali wote umetoweka.....sina raha tena.
Umeanza kutoka na wafanyakazi wenzako (ninapokuwa mbali ktk kutafuta riziki) hadi wake zao wanakushutumu...Nimekukanya weeeeh! ukasema huwezi kuacha kutoka na jamaa zako eti tu kwa kuwa mimi na weke zao tunakutaka uache......we mwanamke mbaya wewe...! Na mengine ya jeuri umeyasema nikakuangaliaaaaaaa........! nikasema poa. Sasa nimechoka na kuamua kukupuuza....! Sina cha kukwambia na sihitaji... After all bado hutanisikiliza wala kubadilika (eti kwa kuwa tu nimesema..) au siyo? Okey! Nakuachia nyumba.. mie huyoooo!
Nashukuru Mungu, nimeamua kuendelea na yangu mambo... Cha ajabu sijui umetoswa na jamaa zako au vipi unaanza kurejea na kusisitiza ninavyopaswa kuwa.... Mara unakagua simu zangu,...mara unahoji kwa nini bado ninawasiliana na wa-zamani wakati ulinikataza, mara unataka niache kutumia Internet mara ooh! siku hizi sikupendi, mara mbona sina wivu, mara ooh inaelekea wanawake wenzako wamekuzidi....Nimekwambia hata hayo uyaache pia kwa kuwa hayasaidiii kuondoa vurugu uliyoanzisha mwenyewe kwa jeuri yako.... Bado unaendelea...
Unajua nini?....Naudhika zaidi. Bora kuwa mpole na mnyenyekevu ili moyo urejee taratibu maana bahati uliyonayo ni kubwa bado sijampenda mwingine kufikia kiwango chako..Nahisi ukiendelea kunikera atapatikana.
Unakumbuka siku uliyopokea simu yangu nilipopigiwa na binti wa kampuni ya simu ukaishia kutukanwa?... Ulipaswa ujifunze kuanzia hapo, lakini wapi! Juzi tunavuka barabara mie na mizigo wewe na watoto (2) nakwambia washike mikono ukakubali lakini ukaendelea kuchezea simu (kama mtoto wa shule). Kama si kasi yangu kutupa mizigo chini na kumuwahi last born pengine tusingekuwa naye leo maana, mtoto kakimbilia barabarani wakati dereva mmoja kakanyaga mafuta ya GX100 yake mpaka basi. Gari imechanachana mifuko mpaka hakuna cha kuokoa. Jambo la kusikitisha unanilaumu eti uoga wangu perfumes zako zimegongwa na gari. Bitch (Sorry..wakuu).. una laana.
Nisiseme sana mwisho watu watajua siri zetu.
Ninachokusudia kukwambia leo ni hivi. Inawezekana kweli ile roho ya kukupenda saaaaaaaana imekufa lakini ya kukupenda kuliko wengine bado ipo ndiyo maana sijakuacha. Sasa nasema next time nakwambia kitu cha msingi kama uhai wa mtoto unaniletea ubishi au mapozi. Sikufichi. That time nakutema hapo hapo na hutaamini maana hutakaa unishawishi chochote tena.
Na mambo ya kujaribu kunidhibiti yananibore kishenzi! Mpaka sasa mademu wa nje sina, na sina mpango wa kutafuta. Unapoona sikujali ni kwa sababu jeuri yako hunikera kiasi cha kufanya nione kama mahusiano ya kijinsia ni vurugu tupu na hivyo kujikita kwenye utafutaji. Nitaendelea kutumia Internet na hutanilazimisha kuja kitandani kama sijisikii. Kimsingi hata mimi kwa sasa siwezi kufanya kila ukitakacho eti kwa kuwa tu umesema. He he he he heeeeeh! Inauma eeh...? Umeanza wewe mie namaliza.
SITANII... UKIENDELEA NA UPUUZI NAKUACHA HATA KAMA ITANIGHARIMU....!
hilo ndilo tatizo kutaka kumsidia mtu aliyetoswa na wenzako walishayaona hayo ndiio maana wakapiga chini
mie ndo sioni kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Maneno yako yanashangaza kweli...na wanaume wanaochwa sio KWA SABABU?!mkuu siku zote mwanamke anapoachwa na kidume mwenzio ni kwasababu..kaa mbali na hzo type
Show love to a woman you love in a three dimension fasion...Length X Height X Width=your love to her.kazi yako ni kucheza na variables tu..When L=2,H=I then W=10,KESHO L=50,H=0 then W=1000 nadhani majabu mnayo sasa.
Namaanisha siku zote anatakiwa aumize kichwa chake kwamba wewe ni mwanaume wa aina gani, yani ukichemsha hapo anakuweka kwenye kiganja.
Maneno yako yanashangaza kweli...na wanaume wanaochwa sio KWA SABABU?!
sasa sibora ungeiweka yote ili tunaoweza kusoma hzo thread ndefu tusome kuliko kukatisha alafu mtu unashindwa kuelewa so hapo tunashndwa kuelewa nini tukushaurUsishangae maana hata mimi sijaelewa kitu! Ninakusudia kuchokoza mjadala mrefu kwa kutoa malalamiko ya mshikaji katika format ya "Barua simulizi" Upo hapo? Bahati isiyo nzuri wengi wetu hatupendi kusoma threads ndefu so, nikaamua kuikatisha ili nipate maoni ya wadau kabla ya kuendelea. Wasipoitaka nitauchuna na kupoteza time kidogo Jukwaa la Siasa.
sasa sibora ungeiweka yote ili tunaoweza kusoma hzo thread ndefu tusome kuliko kukatisha alafu mtu unashindwa kuelewa so hapo tunashndwa kuelewa nini tukushaur
okay let me do that, what u want bro!Isome mwanzo wa Thread na utajua imefikia wapi. Ulipotea kwa muda .....(ID yako). Thanks anyways!
Kweli...binafsi hua napenda kujua kulichowaachanisha na sio nani kamuacha mwenzake.Hiyo sio muhimu kwasababu kila mtu na tabia yake na kwasababu tu alishindwa na yule haina maana wewe hutoweza kuishi nae.Ndio maana unakuta mmoja analalamika mpenzi wangu anaongea sana mpaka ananiboa siku wakiachana dada akaenda kwamwingine kaka wa pili anasifia mpenzi wangu ni mcheshi sana!So yote inategemea tabia ya walioachana na mpenzi mpya....Naamini ni kwa sababu pia, Honey! Unachopaswa kuchunguza, ukiwa mwanamke mjanja (kama unavyotafsirika kwa comment zako), ni kujua kama jamaa aliachwa kweli au yeye ndiye aliacha. Kwa uzoefu wangu mdogo najua kuna watu wanaojua zaidi kusema wameacha kuliko kuacha kwenyewe. Mfano ufuatao unahusika:-Mkaka kamchoka mdada eidha kwa tabia zake au sababu yoyote nyingine lakini, hawezi kumwambia hivyo kwa kuwa anaamini ni ukatili hivyo anachukua option ya kumkwepa. Hapokei simu, anajifanya bize na pengine anagundulika wazi kuwa kawa mkwepaji sana siku hizi. Nia yake ni kumwacha huyu mdada pasipo kumtamkia live. Sasa mdada akigundua hapendwi tena anaweza kutangaza amemwacha jamaa. Mfano huu unatukumbusha nini...? Tusiamini 1kwa1 mtu anaposema kamwacha mwandani wake na pasiopo kuchunguza tukamhukumu mwandani huyo (kwa aliachwa basi...) ana matatizo.
Mhhhh! Ndefu!
Kweli...binafsi hua napenda kujua kulichowaachanisha na sio nani kamuacha mwenzake.Hiyo sio muhimu kwasababu kila mtu na tabia yake na kwasababu tu alishindwa na yule haina maana wewe hutoweza kuishi nae.Ndio maana unakuta mmoja analalamika mpenzi wangu anaongea sana mpaka ananiboa siku wakiachana dada akaenda kwamwingine kaka wa pili anasifia mpenzi wangu ni mcheshi sana!So yote inategemea tabia ya walioachana na mpenzi mpya....
The Analyst,
Hiyo Analysis inakuhusu au Haikuhusu?
Yeyote inayomuhusu Pole zake. Jukumu linabaki kwake(kwako) Kusuka au Kunyoa. Neno la Mungu linasema ,"Mwananmke mpumbavu hubomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe",
Jenga( ajenge) nyumba Hiyo muda unaruhusu ,Kabla hamjaiharibu hiyo Familia, Wewe na yeye hamuwezi kuwa na hathari ila Watoto, Angalieni Future yao, Kukimbia nyumba siyo dawa.