Nakupenda Joy , ila usiwahi nisaliti.

Nakupenda Joy , ila usiwahi nisaliti.

mcTobby

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2018
Posts
7,569
Reaction score
21,837
Hayo ndiyo maneno yaliyoandikwa ukutani na Walter Kipkoech, mwenye umri wa miaka 23, ambaye ni mshukiwa wa mauaji. Aliandika ujumbe huo kwa kutumia damu ya mpenzi wake wa miaka 18, Joy Wangui, ambaye alikuwa mwanafunzi wa Kidato cha Nne.

Walter anadaiwa kumuua kikatili na kumkata kichwa Joy baada ya kumshuku kuwa alikuwa akimsaliti kimapenzi, kabla ya kutoroka katika eneo la tukio.
Kwa mujibu wa Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Kenya (DCI), mwili wa Joy ulipatikana ukiwa umelala ndani ya dimbwi la damu jikoni, huku kichwa chake kikigunduliwa kwenye korido karibu na bafu.

Baada ya operesheni ya pamoja iliyofanywa na wapelelezi pamoja na Crime Research and Intelligence Bureau, Kipkoech alikamatwa siku ya leo, Oktoba 6, 2026, kwenye maficho yake katika kijiji cha Lagwenda, huko Kuresoi North.
Kwa sasa anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Molo .😑😑😑😞
FB_IMG_1791287243020.jpg
 
Mrembo wa Tanzania anauawa kwa risasi ya kichwa, wakati huo mrembo wa Kenya anauawa kwa kutenganisha kichwa na kiwiliwili 🙌

Ni afya ya akili ama wenzetu wanapenda sana kuliko neno lenyewe lilivyo?

Wiki ya huzuni hii, Tanzania na Kenya kwa pamoja
 
Wanawake wanatakiwa kuheshimiwa sana jinsi walivyo na SIO KUAMINIWA....... ukimuheshimu mwanamke na madhaifu yake hakika hutokuja kumdhuru mwanamke hata kama atakuumiza kiasi gani.....Wanaume tunafanya kosa kubwa sana kuwaamini hawa viumbe......Na imani ndo inapelekea haya madhara.
 
Tafran kubwa sana hii, tena dogo wa 23 yrs..

Hii roho ya kikatili unatolea wapi kwa mfano
 
Hayo ndiyo maneno yaliyoandikwa ukutani na Walter Kipkoech, mwenye umri wa miaka 23, ambaye ni mshukiwa wa mauaji. Aliandika ujumbe huo kwa kutumia damu ya mpenzi wake wa miaka 18, Joy Wangui, ambaye alikuwa mwanafunzi wa Kidato cha Nne.

Walter anadaiwa kumuua kikatili na kumkata kichwa Joy baada ya kumshuku kuwa alikuwa akimsaliti kimapenzi, kabla ya kutoroka katika eneo la tukio.
Kwa mujibu wa Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Kenya (DCI), mwili wa Joy ulipatikana ukiwa umelala ndani ya dimbwi la damu jikoni, huku kichwa chake kikigunduliwa kwenye korido karibu na bafu.

Baada ya operesheni ya pamoja iliyofanywa na wapelelezi pamoja na Crime Research and Intelligence Bureau, Kipkoech alikamatwa siku ya leo, Oktoba 6, 2026, kwenye maficho yake katika kijiji cha Lagwenda, huko Kuresoi North.
Kwa sasa anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Molo .😑😑😑😞
View attachment 3685200
Kuna watu ni majangili alloow! kuna mda unaweza jiona mdhambi ila kunasehemu inafika unanyoosha mikono juu mpaka mtu anachkua kisu au panga anachinja binadamu mwenzi anakuwa ameingiliwa na kitu gani naamini sio akili ya kawaida hiyo.
 
Mapenzi +mental health issues ni kama maji na mafuta
 
Nowadays hii imekuwa common nadhani wizara hisika inabidi iwe na zile psychology centers ambapo watu wanakutana nakutoa ya moyoni.
Naona wanafanya sana mablack Americans na inawasaidia
 
Kiukweli wizara husika ingewekeza hasa kwa kuwaongelesha wanafunzi wa secondary na vyuoni kama sehemu ya counseling ingesaidia sana yaani
 
Back
Top Bottom