nakupenda ila subiri nimalizane nae

mayenga

JF-Expert Member
Sep 6, 2009
4,118
1,966
Ni kijana mstaarabu,kakutana na binti mrembo wa haja,kwa vipimo vyake,anamuona kuwa aweza kuwa mke mtarajiwa.Kijana anamdokezea ombi lake,binti anasema hana pingamizi ila,anaye rafiki ila ni mkorofi na hana feelings nae,anaahidi kumpenda kijana huyu baada ya kumalizana na rafiki yake mkorofi.Ni sahihi kuwekwa pending usubiri watu wamalizane wewe ndo uingie?Eti wadau.
 
Choice ni ya wewe unaeambiwa subiri kama subra unayo na moyo wako ukotayari kumuamini hayo anayo kwambia...
 
Ni kijana mstaarabu,kakutana na binti mrembo wa haja,kwa vipimo vyake,anamuona kuwa aweza kuwa mke mtarajiwa.Kijana anamdokezea ombi lake,binti anasema hana pingamizi ila,anaye rafiki ila ni mkorofi na hana feelings nae,anaahidi kumpenda kijana huyu baada ya kumalizana na rafiki yake mkorofi.Ni sahihi kuwekwa pending usubiri watu wamalizane wewe ndo uingie?Eti wadau.

Mhhhhhhhmmmmmmm!!
 
changanya na zako, vp kama asipomalizana naye au akasema kamalizana kumbe bado wapo ktk mahusiano kisiri siri?
 
Ni kijana mstaarabu,kakutana na binti mrembo wa haja,kwa vipimo vyake,anamuona kuwa aweza kuwa mke mtarajiwa.Kijana anamdokezea ombi lake,binti anasema hana pingamizi ila,anaye rafiki ila ni mkorofi na hana feelings nae,anaahidi kumpenda kijana huyu baada ya kumalizana na rafiki yake mkorofi.Ni sahihi kuwekwa pending usubiri watu wamalizane wewe ndo uingie?Eti wadau.

Hizi tabia sisi kama waafrika huwa hatuna kabisa, ila siku hizi tunaiga iga za wenzetu ambazo kwao ni kitu cha kawaida. Nasikia kwa wenzetu pia watu huwa wanapeana hata likizo wakichokana na kila mtu anakuwa huru kufanya lolote analojisikia bila kubugudhiwa na mwenziwe mpaka ule muda unapoisha wanarudiana tena.

All in all, sidhani kama ni utaratibu sahihi, na huu naona kama ni uhuni tu sawa na uhuni mwingine.
 
Mambo yakuwekwa plan B au pending issue siyawezi when it comes to LOVE. Amalizane na hiyo relationship yake ndio amove on, ikiwa si si mke/mme wa ndoa sasa longolongo za nini. Amwage sera na sepe tu.
 
Halafu na wewe jiandae kuachwa in near future kwani ajaye nyuma yako ataambiwa kuwa asubiri amalizane na wewe....lol... twapokezana kama mbio za vijiti?? Usisahau kupima kabla au ndo ushaharibu tayari??
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom