"Nakuomba mke wangu,niwekee Limbwata"

"Nakuomba mke wangu,niwekee Limbwata"

Ralphryder

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2011
Posts
5,599
Reaction score
1,798
Alisikika rafiki yangu wa karibu kabisa akisema maneno hayo! Ni Mtu wa makamo tu kama miaka 35 hivi, Kasema yaani siku hizi anaweza akakaa hata mwezi na nusu au zaidi hana hamu ya ku do na mkewe isipokuwa hawara yake tu! Naye bado anampenda mke wake ishu inakuwa ngumu kufanya nae mapenzi sasa afanyeje? mi nimemwambi sio busara sijui wadau mnasemaje! No abusive language plz!
 
Ampe tu...ukilitafuta tatizo hutalikosa.
 
Naomba nikunong'oneze kidogo....akikupa nisaidie hio dawa na mimi kidogo nikampe my Wife aniwekee na mimi nimpende
 
Dah! ndo maajabu ya dunia unampenda mtu lakini hamu nae huna, amwambie tu maiwaifu wake! yanayojiri ila si kuhusu uhusiano mwingine then ampe kazi ya kulirudisha pendo at the same time na yeye ajue kuwa ni wajibu wake kurudisha upendo huo, so they have to work it together to solve the situation
 
Alisikika rafiki yangu wa karibu kabisa akisema maneno hayo! Ni Mtu wa makamo tu kama miaka 35 hivi, Kasema yaani siku hizi anaweza akakaa hata mwezi na nusu au zaidi hana hamu ya ku do na mkewe isipokuwa hawara yake tu! Naye bado anampenda mke wake ishu inakuwa ngumu kufanya nae mapenzi sasa afanyeje? mi nimemwambi sio busara sijui wadau mnasemaje! No abusive language plz!

Umenikumbusha jamaa yangu mmoja; yeye alisema mkewe akimuwekea limbwata haina shida kwani anapaswa kumpenda.
Anyway ushauri wangu, amtupie Mungu hilo swala lake halafu Mungu atadeal sio tu na ashiki zake bali na moyo wake kiujuma
 
Hawara atakua kesham-twist...
Aangalie asije akahamia huko moja kwa moja....
 
Bado anampenda mke wake afu bado ana hawara nje!!!!!!!mhhh that's soooo amazing mapenzi ya siku hizi hayapandi hata kwa arula nimeamini, Alikiba wa watu aljiimbia!!!!!!!!!!!!
 
Ya nyumba ndogo anaiona tamu sababu anaigharamia,ya nyumbani alishatoa mahari kitambo na akasahau ndio mana hajisikii.
 
Bado anampenda mke wake afu bado ana hawara nje!!!!!!!mhhh that's soooo amazing mapenzi ya siku hizi hayapandi hata kwa arula nimeamini, Alikiba wa watu aljiimbia!!!!!!!!!!!!

mdogo wangu Blue G usishangae kabisa. kwenye ulimwengu huu wenye tabu na dhiki ibilisi ametukuzwa sana. hivi sasa ibilisi amekuwa ndiye msimamizi wa familia hadi kazi za watu.

sasa hapa ibilisi kajiinua kwa mikono na miguu kaiingilia ndoa kaleta mapenzi ya nje ila maskini bado moyo wa mume uko kwa mkewe, hivyo akaona bora aekewe limbwata akasahau kwamba Yupo Mungu wa Israel na ipo Damu ya Yesu isiyoshindwa jambo.

imeandikwa hivi ''mwanangu usikasirike kuachwa na Bwana wala usishangae kurudiwa nae""
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana na maneno yako ya busara dada gfsonwin tuzidi kumwomba Mungu atusaidie nina imani shetani hawezi shindan na nguvu zake.

amen mamii. kumbuka kwaresma hii kusali zaid na kumbuka kutumikia kanisa. angalia wito wako uko wapi kama ni kwenye vyama vya kitume tumika na Mungu atakusaidia kama ni karismatiki tumika na Mungu atakuwa na wewe.

tuzidi kuombeana zaid huku tukikumbukana katika kutakiana baraka na napenda niwe wa kwanza kukutakia baraka za bwana wetu Yesu Kristo ziwe juu yako na juu ya familia yako. Mungu akuangazie nuru ya uso wake mchana na usiku na akubariki kila uingiapo na utokapo na kukupa amani yake. baraka hizi pia ziambatane na mpendwa wangu dada Kaunga popote pale alipo.
nawapenda sana sana
 
Last edited by a moderator:
Nashukuru dada yangu mpendwa na iwe hivyo kwako pia.
amen mamii. kumbuka kwaresma hii kusali zaid na kumbuka kutumikia kanisa. angalia wito wako uko wapi kama ni kwenye vyama vya kitume tumika na Mungu atakusaidia kama ni karismatiki tumika na Mungu atakuwa na wewe.

tuzidi kuombeana zaid huku tukikumbukana katika kutakiana baraka na napenda niwe wa kwanza kukutakia baraka za bwana wetu Yesu Kristo ziwe juu yako na juu ya familia yako. Mungu akuangazie nuru ya uso wake mchana na usiku na akubariki kila uingiapo na utokapo na kukupa amani yake. baraka hizi pia ziambatane na mpendwa wangu dada Kaunga popote pale alipo.
nawapenda sana sana
 
Wanaume wanakula vitu vingi sio siri

Hasa wenye wake zaidi ya mmoja, kila mwanamke huvutia kwake kwa kutafuta limbwata original lenye nguvu; ukichunguza sana wanaume hao huwa kama mazuzu kwa kuathiriwa na malimbwata.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom