Nakumbuka zamani

zamani kulikuwa hakuna kona baa....

Sure....hata vitabu vyetu vya lugha vilikua na title kama hizi.....

Watoto wageuka Mawe
Tola alia gizani
Mwanangu pepe huna masikio
Sadiki na Sikiri
Twende Tukawinde
Musa Mtoto Shujaa
Msema kweli achaguliwa kuwa Diwani
Sizitaki mbichi hizi
Mwenge nk....

Zamani ilikuwa raaha sana...michezo kama kibaba baba na kima mama ilikuwa inakutambulisha kwenye Game....Kulikuwa na mchakamchaka kwenye kila shule......then JKT....full kulipenda taifa lako......siku hizi sasa..................................
 
hii bana nilikuwa naipenda sana kwakweli,natamani irudishwe tena,pia ile stayle ya kuamkia mwl huku mkono uko kwenye paji la uso
Zamani ukisikia wimbo wa Taifa unaimbwa hata kwenye redio, utasimama kikakamavu na hakuna kutingishika hadi wimbo uishe.

Zamani bendara ya Taifa ikiwa inashushwa, afande hupiga filimbi na wote hata wapita njia husimama mpaka bendera ishushwe yote.
 
Nakumbuka zamani.............,zamani kwakweli ilikuwa raha sana na heshima tele,zamani
1.Marufuku kupita makaburini na ikitokea umepita basi ni mwendo wa haraka tena bila kuangalia nyuma wala kungea,lkn siku hizi makaburi yamegeuzwa gesti.

2.zamani mvua kama hizi zinazoendelea kunyesha Dar watu wako busy na kukinga maji na watoto kuoga kabisa,tena maji hayo yanakuwa salam kwa kunywa lkn siku hizi watu ni ma dispenser na maji ya chupa kwa sana.

3.Zamani mtu mzima akipita kwanza unampokea mzigo na kumfikishia kule aendako,lkn siku hizi watu wanawapiga mpaka vikumbo na salamu si lazima.

4.Zamani hasa kwetu Tv tulikuwa tunaangalia taharifa ya habari tu,au bada ya kumaliza kazi za shule tena jumamosi na jumapili tu,siku hizi watoto wanajua ratib zote za vipindi.

5.Zamani mgeni akifika kwako unampokea,anaingia ndani mnataniana hili na lile alafu salamu inafuata lakini siku hizi ukiskia hodi tu na salamu inatolewa hapo hapo utasema huyo mgeni haingii ndani.

6.Zamani hatukuangaika na vitafunio vya chai maana mihogo,viazi,magimbi vipolo vya ugali na wali asb ni kupasha na kula tu lkn siku hizi mara mkate ,sausage,mayai .

7.Zamani msiba unaheshimika lkn siku hizi msibani watu wamegeuza sehemu za kupata wachumba,kujipodoa na kuoneshana vitu tofauti tofauti.

8.Zamani hasa jioni nilipenda sana hadithi za bibi maana zilinifunza mambo mengi na ya kunijenga,hata michezo ya zamani hasa rede,kombolela,lakini sasa hakuna michezo hiyo.

NAJUA DUNIA YA SASA NI KIJIJI LKN KIJIJI HIKI MMMH WALA HAKIFANANI NA KILE CHA KWETU MAANA KIJIJINI KWETU WATU WALIISHI KWA UPENDO,AMANI NA UMOJA.

WEWE ZAMANI UNAKUMBUKA NINI?

Hapo kwenye red banaaaaaa! TV haikuwepo zamani zile!!!

- Mimi nakumbuka kulikuwa na matunda fulani tulikuwa tunayachuma kwenye miti fulani ya miiba tukiyaita mapumbu ya paka, yalikuwa matamu hayooo....acheni tu jamani zamanii!!
 
mafisadi walikuwa nazo huenda alikuwa mtoto wa fisadi!
 
Zamani kwenye mpira tulikuwa tunashabikia timu kama LIPULI, TUKUYU STARS, MECCO, NYOTA NYEKUNDU, AFRICAN SPORTS lakini siku hizi watu mara MANCHESTER, ARSENAL, BARCELONA, CHELSEA
 
ah ah ah umenikumbusha jamaa mmoja alivaa chupi zile za VIP,wakati anacheza ghafla ikaachia mi niliona kitu kimeruka juu kama kishada
Zamani kwenye mpira tulikuwa tunashabikia timu kama LIPULI, TUKUYU STARS, MECCO, NYOTA NYEKUNDU, AFRICAN SPORTS lakini siku hizi watu mara MANCHESTER, ARSENAL, BARCELONA, CHELSEA
 
huamini au?VIP ilikuwa noma jamaa anacheza mpira mara kitu kiko juu usawa wa kifua mara,pyuuuuuuuuuuuuuuu kikaruka juu utasema mpira unataka kuingia golin lol
HA HA HA HA Weeee pearl banaaa
 
Zamani kwenye mpira tulikuwa tunashabikia timu kama LIPULI, TUKUYU STARS, MECCO, NYOTA NYEKUNDU, AFRICAN SPORTS lakini siku hizi watu mara MANCHESTER, ARSENAL, BARCELONA, CHELSEA

enzi za kadenge na mpira kadenge na mpira kashuti goooooo
 
Mh, Pearl, kweli zamani kulikuwa na TV?? Sikumbuki kuziona zamani, ila mara 2 hivi kwa mwaka kulikuwa kunakujaga sinema watu woooooooooteeeeeeeee tunakwenda kuangalia. Zamani ilikuwa raha sana, watu wakubwa wote walikuwa wazazi wangu, siku hizi subutuuuu! Unamfundisha mtoto asiseme na mtu yeyote njiani anapokwenda shule na akisemeshwa atimue mbio! Duh! Kweli umenikumbusha zamani za raha, hakuna hofu zamani. Ila hapo kwenye TV sielewi, maana nimeziona nikiwa mkubwa nimeshajitegemea, kwetu kulikuwa na redio National bendi 4 tena ilikuwa ndiyo redio kweli kweli na majambazi walikuwa wakijua unayo unavunjiwa mlango na fatuma wanaitaka. Ilikuwa inatumia betrii za National. Heheheheh! Zamani.... mengi sana mazuri.....
 
Mme sahau hizi zifuatazo
>>> Zamani Wachungaji na Mapadri wenye kanzu nyeupe wakija nyumba tunafikiri ni Mungu au Malaika
>>> Zamani tulikuwa tunaambiwa sadaka zakanisani zinapandishwa mbguni kwa Mungu kwa ngazi tunaamini
>>> Zamani ukikosea alafu mtu mzima akakutishia nitakukata masikio basi utalia wewee mpaka..au kama akikuona akakutishia kukukata masikio huku akionyesha ishara kama anataka kukukimbiza basi utakimbia wee bila kungalia nyuma huku unalia mpaka mvunguni mwa kitanda. Na huko hutoki mpaka utafutwe!
>>> Zamani Mvua ikianza kunyesha tulikuwa tunaimba MVUA njoo KATARINA usije.
>>> Zamani Shuleni hamuuingii darasani bila kupiga gwaride kwanza.
>>> Zamani Mshabiki wa Simba akipita na Nguo Nyekunde kwenye washabiki wa Yanga au wa yanga akapita na Nguo za njano kwenye washabiki wa simba anaweza kuvunjwa mbavu!
 
Nakumbuka siku ya mechi ya Simba na Yanga wenye redio zao kubwa na maspika ya muziki huyafungua na kuweka nje ili hata mtu aliyeko mbali kiasi gani na majukumu yake asikie matangazo. Siku hizi aahhh!!! wapi, English Premier Leaguee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
dah zamaniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii ............................... tangazo la ukimwi unalia mdundo ...ndunudu.... ukimwi unaua acha ngono lakini siku hizi unabembelezwa ......... kuwa mwangalifu fanya ngono salama
 
Nakumbuka zamani ukienda saloon unayoa nywele unatoa zako shilingi 500 umemaliza unaondoka zako, siku hizi mara scrubbing, sijui facial, mara black mara mask ukitoka hapo unalipa 10,000 au 15,000
 
mmmmh acha urongo sh 500 kwani ni zamani?zamani ni zama zile ukitaka kunyoa unaensa kwa mtu kakaa zake chini ya mti na redio ananyoa watu taratiiiibu

Ahsante sanaaa!!!! Ila ungemuuliza zamani yake ni lini?? Maana kuna wengine zamani yao ni mwaka 2005 atiii!!!!

Ninachojua mie kwenye saluni zamani ilikuwa ni chini ya miti na kiwembe alafu chenyewe ni kimoja kinaweza kula vichwa 20 kijijini!!!!
 
Nakumbuka zamani.............,zamani kwakweli ilikuwa raha sana na heshima tele,zamani
1.Marufuku kupita makaburini na ikitokea umepita basi ni mwendo wa haraka tena bila kuangalia nyuma wala kungea,lkn siku hizi makaburi yamegeuzwa gesti.

2.zamani mvua kama hizi zinazoendelea kunyesha Dar watu wako busy na kukinga maji na watoto kuoga kabisa,tena maji hayo yanakuwa salam kwa kunywa lkn siku hizi watu ni ma dispenser na maji ya chupa kwa sana.

3.Zamani mtu mzima akipita kwanza unampokea mzigo na kumfikishia kule aendako,lkn siku hizi watu wanawapiga mpaka vikumbo na salamu si lazima.

4.Zamani hasa kwetu Tv tulikuwa tunaangalia taharifa ya habari tu,au bada ya kumaliza kazi za shule tena jumamosi na jumapili tu,siku hizi watoto wanajua ratib zote za vipindi.

5.Zamani mgeni akifika kwako unampokea,anaingia ndani mnataniana hili na lile alafu salamu inafuata lakini siku hizi ukiskia hodi tu na salamu inatolewa hapo hapo utasema huyo mgeni haingii ndani.

6.Zamani hatukuangaika na vitafunio vya chai maana mihogo,viazi,magimbi vipolo vya ugali na wali asb ni kupasha na kula tu lkn siku hizi mara mkate ,sausage,mayai .

7.Zamani msiba unaheshimika lkn siku hizi msibani watu wamegeuza sehemu za kupata wachumba,kujipodoa na kuoneshana vitu tofauti tofauti.

8.Zamani hasa jioni nilipenda sana hadithi za bibi maana zilinifunza mambo mengi na ya kunijenga,hata michezo ya zamani hasa rede,kombolela,lakini sasa hakuna michezo hiyo.

NAJUA DUNIA YA SASA NI KIJIJI LKN KIJIJI HIKI MMMH WALA HAKIFANANI NA KILE CHA KWETU MAANA KIJIJINI KWETU WATU WALIISHI KWA UPENDO,AMANI NA UMOJA.

WEWE ZAMANI UNAKUMBUKA NINI?

zamani nilikuwa nasikiliza kipindi cha redio Tanzania tu hadithi za mama na mwana baada ya hapo ..ni kitabu na kumsaidia mama kazi za jikoni.
Siku hizi mtoto kakaa sebuleni mama unapika ukimuita kumuagiza kitunguu mtoto ananuna huyo adabu imeota pembe
 
Nakumbuka zamani.............,zamani kwakweli ilikuwa raha sana na heshima tele,zamani
1.Marufuku kupita makaburini na ikitokea umepita basi ni mwendo wa haraka tena bila kuangalia nyuma wala kungea,lkn siku hizi makaburi yamegeuzwa gesti.

2.zamani mvua kama hizi zinazoendelea kunyesha Dar watu wako busy na kukinga maji na watoto kuoga kabisa,tena maji hayo yanakuwa salam kwa kunywa lkn siku hizi watu ni ma dispenser na maji ya chupa kwa sana.

3.Zamani mtu mzima akipita kwanza unampokea mzigo na kumfikishia kule aendako,lkn siku hizi watu wanawapiga mpaka vikumbo na salamu si lazima.

4.Zamani hasa kwetu Tv tulikuwa tunaangalia taharifa ya habari tu,au bada ya kumaliza kazi za shule tena jumamosi na jumapili tu,siku hizi watoto wanajua ratib zote za vipindi.

5.Zamani mgeni akifika kwako unampokea,anaingia ndani mnataniana hili na lile alafu salamu inafuata lakini siku hizi ukiskia hodi tu na salamu inatolewa hapo hapo utasema huyo mgeni haingii ndani.

6.Zamani hatukuangaika na vitafunio vya chai maana mihogo,viazi,magimbi vipolo vya ugali na wali asb ni kupasha na kula tu lkn siku hizi mara mkate ,sausage,mayai .

7.Zamani msiba unaheshimika lkn siku hizi msibani watu wamegeuza sehemu za kupata wachumba,kujipodoa na kuoneshana vitu tofauti tofauti.

8.Zamani hasa jioni nilipenda sana hadithi za bibi maana zilinifunza mambo mengi na ya kunijenga,hata michezo ya zamani hasa rede,kombolela,lakini sasa hakuna michezo hiyo.

NAJUA DUNIA YA SASA NI KIJIJI LKN KIJIJI HIKI MMMH WALA HAKIFANANI NA KILE CHA KWETU MAANA KIJIJINI KWETU WATU WALIISHI KWA UPENDO,AMANI NA UMOJA.

WEWE ZAMANI UNAKUMBUKA NINI?

hapo kwenye red, labda wewe ni mtoto wa George Kahama. Zamani hatukuwa na TV, ila radio ya mbao - dudu proof special kwa ajili ya kusikiliza hotuba za Nyeyere, mpira wa yanga na simba, majira na mazungumzo baada ya habari ya Paul Sozigwa na brain washers wengine.
 
Back
Top Bottom