Nakubaliana na Mange Kimambi kuhusu wasanii wa Bongo

matumbo

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
7,225
3,944
Leo kuna mtu kaniambia msome Mange kaongea kitu kizuri sana, nikampuuza ila aliponipa brief ikabidi niingie kumsoma.. Kwa kweli huyu mama uwa simkubali mpaka nakufa ila kaongea kitu cha msingi nimeona nikilete hapa ili wasanii wanaochungulia hapa ila wanajifanyaga huko JF siingiagi siasa tupu kumbe wana hadi Senior ids nao wapate darasa kwetu sisi tulio kando ya mchezo.

Mange kaongelea wasanii wa bongo fleva na kupwaya kwenye ubunifu, akimwongelea zaidi Ali Kiba na singo yake mpya...Ntakuwa namnukuu. Penye maandishi ya bluu ni yeye sio mimi

I like Ali Kiba's music but I think he needs to grow kimuziki. Mie naona toka arudi kwenye gemu nyimbo zake zimeshuka kiwango sio nzuri kama za zamani… Au labda tuseme yani nyimbo zake zote ni vile vile yani hazina tofauti.Yani they sound identical.Anabadilisha vitu vidogo vidogo sana

Hili nakubaliana na wewe Mange, Kiba wa sasa uwezi kumfananisha na wa Nakshinakshi au Cinderella.. Sasa hivi beef ndio linambeba sio quality ya muziki wake, mfano hii singo kiukweli kwa mtu anaejua muziki mzuri ata ajifanye kusema ni ngoma kali moyoni ukweli anaujua. Haya mambo ya kubebwa na beef yana mwisho wake. Ilimtokea Juma Necha, alibebwa sana na beef yake na kina chege akabweteka akaanza kutoa nyimbo chini ya kiwango sijui ndege tunduni sijui vitu gani. Ishu ikaja beef ilipokufa ikambidi awashawishi mashabiki na talent yake ikawa ndio mwisho wa Necha rasmi, tunaomba Kiba asifike huko.

hata besti ake Diamond pia nyimbo zake zimeanza kushuka kiwango…. Mie naona tatizo lipo hapa


Na Diamond nae nyimbo yake ya mwisho nitampata wapi haikuwa na viwango vya Diamond tunaemjua wa Mawazo, Ukimwona, Kesho nk.. Nafikiri Diamond kilichomwangusha ni ubize wa ratiba yake, hivyo kutulia kufanya kitu kizuri inakuwa ngumu pia presha ya ugomvi. Ila bado anaweza kufanya maajabu.

Mie naona ndo kama hawa vijana, wameshaandika all the best stuff they have sasa material zimekwisha inabidi wafanye tu ili mradi watoe new single…. Yani kwa Ali Kiba kwa jinsi alivyo under pressure sababu ya hiyo ya likinganishwa na Diamond naona hii new single imemwangusha kabisa yani na sasa ni dhahiri kuwa yeye ni number 2.

Presha ya mashabiki ni mbaya sana, wao wanataka kitu cha kupata kusema na kinaweza kisiwe kizuri ila wakakishabikia tu. Laakini unaweza kuicontrol kama mjanja ...Pia msanii inabidi uwe na kauli na wewe tatizo Ali kapata management mpya ila imekaa kizungu sana, mswahili bwana mpeleke kiswahili tu mambo ya kushutia video uzunguni wakati kisa cha uswazi wabongo utawazingua tu...ni sawa na hii video ya huu wimbo akafanyie kwenye mabarafu mbele.
VANESSA MDEE na JUMA JUX wanaface the same problem. Yani Vanessa na Juma Jux wana swaga za hatariiiiiiiii, yani wamekaa kimamtoni ile mbayaa ila tatizo ni nyimboooooooo, nyimbo hazina viwango vileeeee


Tatizo la Jux sio nyimbo Jux hana talent ya kuwa mwanamuziki star bali ana mikogo mingi ndio inambeba, Vanessa tatizo lake ni kuyumba na kutojua anataka nini ndio maana anaacha RnB anaanza kuimba kama Linah, Mwasiti, Recho ambao kiukweli wamechosha kusikilizwa sababu wadada wa THT wote ni kama wanaimba kitu kimoja na sababu kubwa mtunzi wao ni mmoja ambae Vanessa ameanza kumtumia asipoangalia ataishia njiani.. Radha za THT zimetosha ndio maana hata Ruge anataka kuifunga, ni kama imestuck.


Well, kunapokuwa na tatizo lazma tutafute na suluhisho… Tumeshajua tatizo sasa hivi ni uandishi wa nyimbo sio kwamba hawajui kuimba kama zamani. Talent zao zipo pale pale au hata labda zimeongezeka kutokana na experience ila problem is hawana tena material ya kuandika nyimbo



Hapa ndio pagumu kwenye muziki wa bongo, msanii atakubali kila kitu lakini sio kuandikiwa yaani wanaona kuandikiwa nyimbo ni aibu kubwa sana matokeo yake wanashindwa...Ila kiukweli wasanii inabidi wabadilike waanze kuandikiwa nyimbo mtu anasound vile vile miaka na miaka msikilize AY, MwanaFA, Benpol, TundaMan, TID, Dully nk akitoa wimbo mpya ni kama umeshawai kuusikia sababu kicwa kimeshachoka hakina jipya japo uwezo bado wanao.

Kuna wasanii wameandikiwa nawafahamu wakaja kama wapya mfano Shaa, Feruzi na kibodaboda, Aslay, hawa wote wanaandikiwa na Fela..Mama Ntilie Rayc na wale wapemba aliandika Adam Juma, zipo nyingi.


wasanii wetu ambao wameshajenga majina yao wasikubali kushuka kwa kung'ang'ana kuandika nyimbo zao wenyewe. Waanze kutumia professional writters ili waendelee kubaki kwenye gemu
…



Wasanii kukweli wawe profesheno, na hata maprodyuza wao wawe maprofesheno kuna nyimbo zina makosa mengi ila zinatoka sababu prodyuza hajui muziki anachojua ni kupiga mdundo baas, na wasanii wanakimbilia kwa awa maprodyuza underground sababu wanawarekodia bure..

Unasikiliza nyimbo ina kelele ila inapigwa daily redioni, big up kwa majani asingekuwa anajali profeshen yake huu muziki ungekuwa nyuma sana studio yake aliita wataalam kina bizman, kina raja wamsaidie mambo ya kimuziki wasanii wasio na talent ila walitaka kulazimisha fani kibabe aliwachapa sana ikawa kupitishwa na majani ni kama umefuzu hii ilisaidia kama screening flan ila kiukweli tunaitaji usiriaz ukiangalia muzki ni kama umefika kileleni unaanza kushuka watu wanaanza kukimbilia video wawe kama fulani ila muziki mbovu kama kina Temba sijui ndio nini kile wameimba..

Watu kama kina tundaman au nahreal sio waimbaji kabisa ila wasanii wangeheshimu watunzi wale jamaa wamngekuwa kwenye mastudio wanaandika tu. Kuna watu wapo kitaa na mishe zao zingine ila wana talent hatari maofisini huko wangefanya hii kama part time kulikwa kuwa na watu wale wale hakuna ubunifu..


Nawashukuru kwa kusoma gazeti langu ila linawahusu zaidi wasanii kama unalakuongzea welucamu kama huna potea usilete ushabiki wa maandazi mie nimemwaga facts tu sio ushabiki na unawausu wasanii zaidi..
 
Well said...mi ntaongezea hapo Kwenye kuandikiwa nyimbo...
Ujue wasanii wetu wakiwa wakubwa wanaona aibu swala la kuandikiwa wakati wenzao wa mbele wana music wakubwa mfano marehemu Michael Jackson alikuwa akiandikiwa nyimbo zake mpaka akawa na hit mno..
Ukija kwa Rihana most ya nyimbo zake zote anaandikiwa...
Nafikiri wasanii wetu wanatakiwa wapatiwe elimu kuhusu hayo mambo kwani ni professional tu.
 
Tanzania inachekesha!

Unawezaje kuwalipa ma professional kama industry ya muziki yenyewe haina dira!!!:confused::confused::confused: Kwa kifupi industry ya muziki inahitaji dira kwanza, hayo maushauri ya wadau kuhusu muziki siyo mbaya, ila inakuwa ni utoto na ujinga sometimes ukitoa ushauri kuhusu jambo flani na huku ukijua eneo hilo limekosa dira kabisa.

Hata diamond anajaribu that's why anaongea sana hata visivyo vya kuongea, kwa sababu muziki wetu hauna dira, ila big up wasanii wa bongo flavor, kwani wana lisogeza game.

Muziki wa Tanzania hauna dira, wasanii wanajitahidi kulisogeza game.
 
Jambo moja la msingi amezungumza, Ali kiba sasa anategemea bifu.
 
Vitu vingine mnaongea tu vile mnadhani/hisi.
Pressure kwa nani?? Kiba huyu huyu?
Anyways....ni mtazamo/fikra zako!

Wewe hujui ni jinsi gani mnawapa presha awa wasanii, kila kukicha mnalilia wimbo mpya. Mara oh umezidi kuzubaa atoe nyimbo mara kwa mara kama fulani ndio matokeo yake wanakuja na vitu havieleweki. Mtu uwezo wake ni kukaa miezi 6 ndio aje na kitu kingine ila sasa analazimika akae miezi miwili. Anafanya vitu under pressure.
 
Well said...mi ntaongezea hapo Kwenye kuandikiwa nyimbo...
Ujue wasanii wetu wakiwa wakubwa wanaona aibu swala la kuandikiwa wakati wenzao wa mbele wana music wakubwa mfano marehemu Michael Jackson alikuwa akiandikiwa nyimbo zake mpaka akawa na hit mno..
Ukija kwa Rihana most ya nyimbo zake zote anaandikiwa...
Nafikiri wasanii wetu wanatakiwa wapatiwe elimu kuhusu hayo mambo kwani ni professional tu.

Kweli kabisa mbele 99% ya nyimbo zinaandikwa na waandishi wengine....Sasa kibongobongo mtu anaona ataonekana hawezi, kumbe ishu sio kuweza unaweza ukajua kuandika mwenyewe ila unakuwa ushakinai.

Unaimba weee ila nyimbo tatu ni kama wimbo ule ule. Tizama nyimbo za Roma zinaboa tu siku hizi, ukichukua nyimbo zake uondoe chorus ni kama unasikiliza wimbo mmoja. Tena ata akisema kesho anatoa wimbo mpya unaweza kutabiri mistari ni escrow, waua albino, diamond na zari, magaidi wa amboni...Ubongo umefika kwenye limit yake anaitaji mtu wa kumleta upya.
 
Tanzania inachekesha!!! Unawezaje kuwalipa ma professional kama industry ya muziki yenyewe haina dira!!!:confused::confused::confused: Kwa kifupi industry ya muziki inahitaji dira kwanza, hayo maushauri ya wadau kuhusu muziki siyo mbaya, ila inakuwa ni utoto na ujinga sometimes ukitoa ushauri kuhusu jambo flani na huku ukijua eneo hilo limekosa dira kabisa. Hata diamond anajaribu that's why anaongea sana hata visivyo vya kuongea, kwa sababu muziki wetu hauna dira, ila big up wasanii wa bongo flavor, kwani wana lisogeza game. Muziki wa Tanzania hauna dira, wasanii wanajitahidi kulisogeza game.

Kibongobongo katika eneo la sanaa muziki kidogo ndio unaoonyesha uhai ndio maana unaona ata sponsors wameanza kuweka pesa zao.

Uwezi kufananisha na sanaa zingine zilizojifia kama muvi, ndondi, fashion, paintings nk. Sema ndio hivyo muziki umekosa creativity siku hizi hausikii wimbo ukabaki mdomo wazi kwamba huyu mtu kichwa chake kinawaza nini. Hela imekuwa nje nje ila waimbaji ndio hakuna matokeo yake muziki unakuwa kama one man show.

Kifupi naweza sema music bado haijapoteza dira ila kunaitajika innovation fulani kunyoosha industry. Kama mnakumbuka Salama enzi zake alikuja na mtindo wa kukosoa videos watu hawakumuelewa ila tuliona wasanii wakaanza kuimprove quality za video coz walikuwa wanapata lesson japo aliwaudhi.
 
Vingine sijaelewa nimeelewa vitu points mbili tu
1.ally kiba Wa Cinderella sio ally kiba Wa chekecha
2.Ally kiba anategemea bifu ili kubaki kwenye gemu
 
I like Ali Kiba's music but I think he needs to grow kimuziki. Mie naona toka arudi kwenye gemu nyimbo zake zimeshuka kiwango sio nzuri kama za zamani…
Au labda tuseme yani nyimbo zake zote ni vile vile yani hazina tofauti
.Yani they sound identical.Anabadilisha vitu vidogo vidogo san
a

Hapo kwenye red mark hapo bidada hata mimi naweza kukubaliana naye huu wimbo mpya wa Ali Kiba ni wimbo mzuri ila hamna jipya hata hit yake itakuwa sio ya muda mrefu.Nadhani Diamond kamfanya apanic kbs.Ila akirelax mbona talent anayo sana mimi sauti kwenye nyimbo zake ndio zinanivutia ila kwa nyimbo kama huu mpya bado hajanisababisha niseme waoooh.

 
Mtoto wa kiume kuwa na CHUKI towards MWANAUME mwenzako...

Mleta Uzi huwa "anajifanya" anaujua sana Mziki wa Bongo, lakin cha kushangaza Kashindwa kugundua kuwa hiyo paragraph ya kwanza aliyoiquote kuhusu "music and identity" ni ya "KIJINGA" sana..identity katika Music ni kitu cha kwanza ambacho msanii yoyote is ought to Consider!! ndo maana since 90's mpaka leo tones na flows za kina Jigga, Nas, Snoop Dogg, Robert kelly, Usher, DMX etc, Now kuna kina Pharrel, Breezy, Weezy, Tyga, Drake, John legend, Jason Derulo, katy perry, T.I, Nelly Etc wameshaEstablish they're own identity, kias kwamba ukiflow au ukipita mule wanapopita u're in Trouble...

but mtu anakuja hapa na kusupport kuwa Ali kiba's Music umekuwa so identical!!!

from Run It to Loyal, Breezy anachofanya ni kubadilika kulingana na soko linavyotaka, huwez kumpata breezy wa Gimme that sahiv, au huwez kumpata Robert kelly wa The world's greatest sahiv,( ngoma ya Robert kelly mpya mmeisikia)..

Watu wanaenda na soko sahiv linataka nn, dunia inataka kuskia nn, siku hiz Drake anauza sokon zaid ya Nas Escober, Kitu ambacho mabishoo wa hatari kina MASE walishindwa (kuyapita mauzo ya kina Nas kwa single na Albums kwenye Billboard)...music ni biashara sahiv, unataka kiba atoe MackMuga sahiv??? soko la Music sahiv linataka hivyo??? asilimia kubwa ya mashabiki wa bongoFeva ipo wapi???

M-bongo ukijaribu kupinga ngoma kama Wiggle ya Jason, Roar, ngoma za Rich Gang (kina Young thug and Co.) kuwa hazina maana yoyote, anaweza akashambulia kwa matusi, lakin yupo free kuponda ngoma za kina Diamond na Kiba au Barnaba au Weusi, kuna haja gani ya kuponda ngoma za kibongo kuwa hazina maana wakat, Alejandro ya LadyGaga ikipigwa Club unacheza???

Aim ya Kiba ipo katika BIASHARA, acha Kazi yake ya Mziki imlipe..Coz Music ni Biashara siku hizi..hicho kitu kila siku NIKKI WA PILI anakisema, kama umeamua kufanya Music biashara,fanya iwe Biashara kweli!!!
 
Afu ile "akadumba" ya Ney wa Mitego, mbona haikuandikiwa Barua???

Excuse, itakuwa Ali kiba ni msanii mkubwa na Mkongwe!!!! (piece of shit)...

3 WORDS "MUSIC NI BIASHARA"
 
MosDef naona wewe una tatizo binafsi na mimi ndio maana umeishia kunishambulia.
Ila ulichokiandika mantiki yake ni kama nilichokiandika mimi...Ndio maana ata maswali umeweza kujijibu mwenyewe.

Anyways huu ni mtazamo wangu ata kama hauupendi hauna jinsi ni mimi huyu utafanyaje sasa.

Nachoweza kukushauri ni kwamba unapokutana na watu wanajadili issues mihemko weka pembeni. Ushabiki hautokisaidia.
 
Last edited by a moderator:
Kichaa hawezi kupona ila anapata nafuu na hautakiwi kumuamini pia(Mange),nadhania hata lengo kuu la uzi liko wazi if u can read between the line bado nashangaa idadi ya makala zinavyoongezeka kisa kuna ngoma moja imetoka tena ya yule anaesemwa kaisha tunasahau kua kuna joints kibao zimemwagika tena za wakongwe hasa kama AY na hatukutaka kuziongelea mi nadhani ifike wakati tupunguze chuki za kipuuzi ili maisha yaendelee maana tunatoana akili tu.

MosDef nakubaliana na wewe kwenye ishu ya kuwa na identity iwe kwa mwanamuziki au mtayarishaji ni kitu muhimu jambo la msingi ni kuangalia mahitaji ya soko nashangaa kusikia watu wanataka kumsikia mwanamuziki akiwa kama yuleee haiwezekani leo Prof Jay apasuke kama chemsha bongo,TID apite kama Zeze na Nature wa Hili gemu au Fa wa Ingekua vipi ni mwehu pekee atabaki na fikra hasi narudia tena MosDef mara chache unazochangia unaacha alama sahihi bravo mkuu kwa hili.
Ukiona unachukiwa sana basi jua wanakuogopa au wanaanza kukupenda.
 
Last edited by a moderator:
Kichaa hawezi kupona ila anapata nafuu na hautakiwi kumuamini pia(Mange),nadhania hata lengo kuu la uzi liko wazi if u can read between the line bado nashangaa idadi ya makala zinavyoongezeka kisa kuna ngoma moja imetoka tena ya yule anaesemwa kaisha tunasahau kua kuna joints kibao zimemwagika tena za wakongwe hasa kama AY na hatukutaka kuziongelea mi nadhani ifike wakati tupunguze chuki za kipuuzi ili maisha yaendelee maana tunatoana akili tu.

MosDef nakubaliana na wewe kwenye ishu ya kuwa na identity iwe kwa mwanamuziki au mtayarishaji ni kitu muhimu jambo la msingi ni kuangalia mahitaji ya soko nashangaa kusikia watu wanataka kumsikia mwanamuziki akiwa kama yuleee haiwezekani leo Prof Jay apasuke kama chemsha bongo,TID apite kama Zeze na Nature wa Hili gemu au Fa wa Ingekua vipi ni mwehu pekee atabaki na fikra hasi narudia tena MosDef mara chache unazochangia unaacha alama sahihi bravo mkuu kwa hili.
Ukiona unachukiwa sana basi jua wanakuogopa au wanaanza kukupenda.

Kuwa na identity hakutoshi kumuuza msanii, lazima uwe na radha mpya. Wengi walioshindwa muziki sio kwamba wamepoteza identity ila imefikia hatua wamedumaa.
Huyu anaejiita mosdef anatoa mifano ya kina Snoopy sijui kama amemsikia Snoopy wa Dog Style na huyu Snoopy Lion? Kilichombeba mtu kama Pharell ni ubunifu pia anakuja mpya kila wakati toka enzi za Neptunes.

Whatsap man naona kama umepanic hivi...Mtu akishauri vitu vya msingi akili zenu zimeshalewa na ushabiki...
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom