Nakosa cha kuongea na mpenzi

Barriz

Member
Nov 29, 2015
21
3
Habari zenu wana jamvi. Mimi ni kijana wa miaka 25 nina mpenzi natarajia kumwoa mwakani. Sasa Iko hivi huwa nikikutana na huyu mpenzi wangu huwa nakosa cha kuzungumza nae tunaweza tukae hata dk 5 bila kusemeshana. Na ukizingatia mimi kwenye mapenzi nimeanza kujihusisha hivi karibuni baaada ya kumaliza chuo. Hivi wadau huwa mnazungumza nini na wapenzi wenu? Maana naona Ataanza kunichoka sasa.
 
hamna mapenzi hapo... mkipendana story huwa haziishi, mtaongea hata ujinga imladi mmeongea tu!!!

sa dak 5 zote mpo kimya kila mtu anawaza mchepuko wake...
 
Habari zenu wana jamvi. Mimi ni kijana wa miaka 25 nina mpenzi natarajia kumwoa mwakani. Sasa Iko hivi huwa nikikutana na huyu mpenzi wangu huwa nakosa cha kuzungumza nae tunaweza tukae hata dk 5 bila kusemeshana. Na ukizingatia mimi kwenye mapenzi nimeanza kujihusisha hivi karibuni baaada ya kumaliza chuo. Hivi wadau huwa mnazungumza nini na wapenzi wenu? Maana naona Ataanza kunichoka sasa.

Ulimtongoza au ulitongozewa na kama ulimtongoza ulimtongozaje ?
 
Pata bia mbili tatu maneno yatakuwa mengi mno mpaka ya lugha iliyopanda pipa utazungumza
 
we acha mambo ya ajabu... ukose cha kuongea na mpenzi wako..?
basi siku mkikutana muulize anapenda nyimbo?akijibu muulize aina gani ya nyimbo? akijibu muulize anajua kuimba? yaani anachojibu ndio kinazaa swali jingine.
mpe nafasi naye akuulize swali kwa kuinesha kutoridhika na jibu lake..
tembea na mada mda mrefu huku ukiibasilisha taratibu kurudi kuongelea mapenzi kuona kama mnaendana interests
 
Back
Top Bottom