Nakosa cha kuongea na mpenzi

Huyo ni mtarajiwa wako wa baadae lakin kwa sasa sio mpenzi wako, au ni mtarajiwa na mpenzi wako wa sasa? Kikubwa wewe mfanye rafiki yako kama rafiki zako wengine wa chuo.

Share nae mambo mbalimbali ya kimaisha kama unavyoshea na masela wako wengine wa kitaa au chuo. Ukimuweka kundi hilo hutokosa cha kuongea.
 
Ahaaaaaa njo nikufundishe loh hivi utaanzaje kukosa la kushema kwa mfano? Hata mambo ya siasa, mabadiliko na ukawa, mpira, mambo ya kijamii,mahusiano hujui? Acha utoto basi kuwa unashutukiza unamwambia shikamoo basi ataona aibu acheke ndo story zinaanza.

Au develope vitu ambavyo ni vya kipekee kiasi kwamba akiona ishara anajua ni wewe. basi kama kuna sehemu mnakutanaga au unajua lazima binti huyo apite, kila ukipita hapi dondosha ka ua (sio la dukani) na liwe the same colour basi kila akipita analikuta mbona ataanza naongezi mwenyewe??

Au develop jina la kichekesho ukimuita tuu lazima acheke mfano my...... Malizia
 
fanya hivi mkuu; weka mazingira awe mtani wako! yaani isiwe kama ni mama mkwe wako. weka mazingira ya utani nae yaani mnataniana sana kucheka, kufanyiana vituko vya kutosha, mnataniana muweke mazingira ya utani we utakuaje na mpenzi wako afu muwe serious kama ni mwalimu wako mkuu bhana. ila usipofanya hilo basi jua akipata mtu wa kumtaniatania kumfanya acheke vituko vya hapa na pale basi jua ataondoka mazima. maana ya mpenzi ni kimbilio lake kwa faraja sa anakuja kwako mnakosa la kuongea then nyie ni wapenzi au kitu gani
 
dakika 5*5=25 umri wa jamaa,...unashindwa kumsifia? kamwambie baby unajua unahips kama tofali za kuchoma,.stori zitaanza
 
Namshangaa.
Hivi mnakosaje ya kuongea kwa mfano?
Hawana hata jirani wa kumuongelea?
Enzi zangu kama tumekosa kabisa story tunafungua MAHAKAMA ,tunasomeana mashtaka.... Ugomvi unaibuka tu.
Baada ya miezi kadhaa nayo inakua story.


umenichekesha sana mkuu
 
Back
Top Bottom