Nakiri nimemkosea mwanaume mwenzangu

hofu yangu ni 1,,,,, kweli wewe ni rijali?????? huna demu wako???? kweli mwanaume mwenye urijali na mkomavu anaweza kusumbuliwa na kitu kama hiki???....duh eti alikuwa anakuja kuchukua CD.......acha wakusingizie tuu...wamekuona bwimbi.....


Sawa tu hayo ni maoni yako sina namnay ya kukuaminisha mkuu.
 
Na mimi kuna msichana(mwanafunzi) anasoma boarding yule mtoto akifunga shule geto kwangu hakauki na mamaake ni single mother kila mda yuko geto anavizia mda wa mother kurudi mida ya saa 20-21 ndo anatoka na hata jamaa anaye mgonga namjua lakini itakuaje siku yule mtoto amepata mimba??? na wapangagaji pale wote wanajua kwamba mtoto geto kwangu hatoki!! na sijawahi hata kumtongoza!!
natumai hujazaliwa 1961..This is a bomb, microsecond away from being detonated.
 
Pole sana jikusanye na ndg yako na shemeji muende kwa jamaa mkamueleze kila kitu
 
tatizo lenu mnapenda sana mazoea ya kipuuzi unaanzaje kubadilishana CD na mabinti, me huwa sipendi mazoea ya ajabu ajabu kama haya
 
Sioni kama wewe ni mkosaji (kama ni kweli hukuwahi kudandia mahusiano yao kama ulivyoeleza). LA muhimu kwa sasa, kama walivyoeleza wengine wenye mapenzi mema, ni kujiamini na kutafuta namna ya kukutana na huyo jamaa ili kumweleza ukweli uliopo. Akikataa rudi, tafuta ndugu wachache, nenda tena mzungumze.

Akiendelea kukataa na kukutuhumu achana naye maana atakuwa anatafutiza visababu vya kumwacha huyo binti. Lakini wewe utakuwa umeshafanya yaliyokupasa, nawe utakuwa mtu huru. Zaidi ya yote kwamba wewe, binti na Mungu tu ndio mnaoujua ukweli wa jambo hili.
 
sasa unalia lia nini ndugu, hapo ni kuchukua hatua tu...na kama hukusex nae ini shida...binti pia ndio anajua ukweli...nani mlemavu pia ..kama ni huyo mwanaume pia itakuwa inferior situation .....kingine maamauzi ni yake ya kutotembela hospital sio wewe...isiwe ulilala nae af unasema huku do....pamoja na yote we endelea na utaratibu wako wa maisha kwa kuwa sio wewe.....kilakitu itakuwa wazi....na mkapime basi DNA ila sio mapema baada ya wao kutoelewa au huyo jamaa kutoelewa....
 
I can see Mkuu. big up sasa naona unasikilizia umeitiwa nini
Najaribu kuzingatia mkuu, huu uzee inanipasa kua msikivu sana aiseeee......
Bila ya kua msikivu, vijana hawachelewi kujaza kingi
 
sasa umekosea wapi unakiri nini? au ulifanya naye? mbona mwandiko wako unaonesha kukiri unachokikana nafsini mwako
 
Mimba za Bluetooth hizo. Pole sana ila nadhani jamaa mwenye aloweka mimba Kwa huyo dada alikuwa anatafuta sababu tu ya kuruka majukumu nawe ushaingia kwenye sababu zake umemsaidia kutoroka sindimba ya malezi.

Mimba zinazokataliwa miaka Hii Ni nyingi kuliko zinazoishia kwenye condom

Me naona hujakosa na huna kosa kabisaa ila huyo jamaa ndio ana makosa ya kuleta duniani mtoto ambae baadae ataitwa " mtoto anayeishi kwenye mazingira magumu' Mungu amsaidie mama wa mtoto
 
Back
Top Bottom