Nakiri nimemkosea mwanaume mwenzangu

Na mimi kuna msichana(mwanafunzi) anasoma boarding yule mtoto akifunga shule geto kwangu hakauki na mamaake ni single mother kila mda yuko geto anavizia mda wa mother kurudi mida ya saa 20-21 ndo anatoka na hata jamaa anaye mgonga namjua lakini itakuaje siku yule mtoto amepata mimba??? na wapangagaji pale wote wanajua kwamba mtoto geto kwangu hatoki!! na sijawahi hata kumtongoza!!
 
Jamaa basi atakuwa inferior labda kwa hali yake.lkn ni vzr ukianza kujiepusha na huyo binti na umueleze hilo alielewe.Anapaswa kujiheshimu hasa ukizingatiwa kwamba katolewa mahali ni kwa mila nyingi ni kama ameshaolewa.utajisiej ww una mtu umemtolea mahali halafu anashinda kwa mchizi mwingi.hili jambo ni elementaru kabisa hukuhitaji kuomba ushauri.unatuchosha tu

sawa mkuu lakini huyu dada sio kwamba hajiheshimu ila alikuwa hajajua kama ni kosa kuja kwangu na pia sikuwahi kumuona akionyesha dalili dalili zozote za mapenzi kwangu hata mara moja kwa kweli.
 
Na mimi kuna msichana(mwanafunzi) anasoma boarding yule mtoto akifunga shule geto kwangu hakauki na mamaake ni single mother kila mda yuko geto anavizia mda wa mother kurudi mida ya saa 20-21 ndo anatoka na hata jamaa anaye mgonga namjua lakini itakuaje siku yule mtoto amepata mimba??? na wapangagaji pale wote wanajua kwamba mtoto geto kwangu hatoki!! na sijawahi hata kumtongoza!!


mzee mkimbie mapema bomu hilo.
 
Hizi scenario huwa zinatokea sana, watu wengi wametiwa hatiani kwasababu ya ushahidi wa kimazingira ambao kimsingi hautoshi kuthitibisha kosa. Mambo ya namna hii ni kumuomba Mwenyezi MUNGU aingilie kati kwa kuithibitisha haki na kuifuta batli inayoamiwa na wengi kuwa ni kweli kumbe si kweli. Nilishawahi kutiwa hatiani mm na mwenzangu kwa ushahidi wa kimazingira lkn ukweli ni kuwa sisi hatukufanya lile kosa hakika!!

Pamoja na yote hayo, ww pia unamakosa, kushinda ndani mwako na mwanamke asiye wako ni makosa sana!! Hata ungekuwa ww ndio huyo mlemavu unadhani ingekuwa rahisi kuelewa??? Mkuu tubu dhambi hiyo kwanza, kisha anza utaratibu wa kurejesha amani kwa uchumba huo unaoelekea kuvunjika.

kweli nimekosea sana kumkalibisha nyumbani.
 
Onana nae ongea nae man to man, tell him the truth and let him know the effects of not taking his responsibility..whether to believe you or not is not up to u. Ishu ya ulemavu isikufanye uji-feel guilt. Everyone is mlemavu anyways.
 
Onana nae ongea nae man to man, tell him the truth and let him know the effects of not taking his responsibility..whether to believe you or not is not up to u. Ishu ya ulemavu isikufanye uji-feel guilt. Everyone is mlemavu anyways.

Nimekupata mkuu
 
kwani kuna ubaya mkuu???mie nakushauri uhame huo mtaa nenda mbali ,huyo mwanamke asijue unapokaa,wakikutafuta wakikupata waambie huyo si mwanao,nendeni polisi wakufungulie mashtaka au waende ustawi wa jamii,hapo ndipo haki itatendeka maana watahitaji uthibitisho wa DNA.

ahsante nimekuelewa vizuri
 
Habari wanajamii, poleni kwa majukumu ya kutwa nzima ya leo.

Jamani naombeni mnisaidie nini cha kufanya nana roho inaniuma sana kwa jambo hili. Kuna ndugu yangu naishi nae mtaa mmoja ila yeye ameo na ana watoto wawili. Mara nyingi huwa nakwenda kwake nahasa shemeji yeye huwa anata niende kula chakula kwake pindi ninapotoka kazini kwa kuwa mimi bado sijaoa so ananionea huruma kujipikia mwenyewe.

Sasa pale kwa huyu ndugu yangu kuna mpangaji ambaye anawatoto wawili mmoja ni binti mkuwa wa miaka 21 na mwingine ana miaka 13 kiujumla maisha yao si mazuri kila kitu wanamtegemea mama yao. Huyu binti mdogo anasoma form one pamoja na mtoto wa ndugu yangu.

Hawa watoto wamenizoea sana. Nikajikuta namhurumia sana huyu mtoto wa jirani wakati mwingine anakosa hata vifaa vya shule kutokana na hali yao ya kimaisha basi nikaamua kumnunulia baadhi ya vitu pia na hata pesa za tution namlipia mimi. Mama yake pamoja na dada yake wakanishukuru sana.

Sasa ikawa kila siku dadayake akaanza kuwa karibu na mimi na hatimaye tukawa marafiki wakubwa tu hadi kwangu akawa anakuja kilichokuwa kikimleta ni CD huwa anapenda sana kuangalia seasons kama mimi so anakuja kuchukuaga kwangu. Ila hatukuwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi hata siku moja Mungu wangu ni shahidi.

Kumbe huyu dada alitolewa mahari na bwana mmoja hapa mtaani mimi sikufahamu hilo na wala yeye hakunambia. Mara nikamuona huyu dada akiwa mjamzito sikuhoji kitu na sikuwa na sababu ya kuhoji kwa hilo.

Kumbe likawa kosa kubwa sana mchumba wake akawa analalamika kuwa mimi natembea na mchumba wake mimi sikuwa na habari kwasababu mimi si mkaaji wa vijiweni mimi nikiingia nimeingia nikitoka nimetoka ukibahatika basi utanikuta kwa shemeji yangu so story za mitaani zikawa zinanipita.

Imefika wakati huyu dada kajifungua tena kwa oparetion na siku chache kabla ya kujifungua alikuja kwangu tuliongea sana kama kawaida yetu. Kilichotokea jamaa kamkataa mtoto anadai sio wake ni wangu mimi na hii leo ni siku ya 6 tangu ajifungue jamaa hajaenda kumuona mwanae. Dada wa watu analia anaomba nimsaidie kumwambia ukweli huyo jamaa. Shemeji ndo amenambia kila kitu kuhusu huyu jamaa.

Kinacho niuma zaidi mtu mwenyewe ni mlemavu masikini naumia sana moyoni sikutembea nae mimi hata mara moja jamini. Nitafanya nini ili niaminike wakati watu walikuwa wanamuona akija nyumbani kwangu?

NITAELEZA NINI MIMI WAPENDWA. NAJIONA MKOSAJI HASA MTU MWENYEWE KILEMA NITAANZIA WAPI KUMWAMBIA UKWELI .
NISAIDIENI MAWAZO YENU NDUGU ZANGU NIMEKWAMA HAPA.


siku nyingine usiwe na ukaribu uliopitiliza na mwanamke mkubwa coz ana mtu wake,hata mm ningekuwa jamaa nisingekubali mtoto kirahisi
 
Mambo ya kawaida haya mkuu.........lkn naamini umejifunza kitu....sio wa kuwachekea hawa.........
 
Uliendekeza ukaribu na mwanamke ambaye huna mahusiano naye ya nini? mpaka unamruhusu kuja kwako hata wakati ana ujauzito? huyo jamaa hawezi kuamini kuwa hujala mzigo hata mimi nisingeamini kwani ww hudindishi aweze tu kukuamini kirahisi? kalee mwanao acha kutuzuga hapa.
 
hofu yangu ni 1,,,,, kweli wewe ni rijali?????? huna demu wako???? kweli mwanaume mwenye urijali na mkomavu anaweza kusumbuliwa na kitu kama hiki???....duh eti alikuwa anakuja kuchukua CD.......acha wakusingizie tuu...wamekuona bwimbi.....
 
DNA laki tatu tu ,poteza laki tatu kapime nyie wote.na kama anakataa huyo mwanaume.nenda polisi huko unafuata utaratibu mwingine maana unaweza kufikiria hivi naye kumbe anakufikiria mabaya.,kuwa makini mkuu
 
Uliendekeza ukaribu na mwanamke ambaye huna mahusiano naye ya nini? mpaka unamruhusu kuja kwako hata wakati ana ujauzito? huyo jamaa hawezi kuamini kuwa hujala mzigo hata mimi nisingeamini kwani ww hudindishi aweze tu kukuamini kirahisi? kalee mwanao acha kutuzuga hapa.

Mkuu huwezi kula kila anae pita mbele yako kisa we nimwanaume.
ni kweli alikuja kwangu lakini sikuwahi kutembea nae.
 
Back
Top Bottom