Nakiri leo kuwa Mungu yupo!

Nakiri leo kuwa Mungu yupo!

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,793
Reaction score
5,042
Katika watu ambao walikuwa wabishi kuhusu uwepo wa Mungu mimi wa kwanza na nilikuwa na sababu zangu

Sababu hasa ilikuwa matatizo ambayo nilikuwa nayo:

Nilikuwa na matatizo ya ugonjwa wa ini. Niliteseka saana. Nilikwenda hospitali mbalimbali bila mafanikio yoyote yale. Nilikwenda kwenye Makanisa mbalimbali kutafuta msaada bila mafaniko nilikwenda kwa waganga wa asili bila mafanikio.

Familia na ndugu zangu walikuwa wanasubiri tu siku nitoweke duniani. Na mimi nilikuwa nimeshakata tamaa ya kuishi kabisa maana. Tumbo ilikuwa imeanza kujaa maji na miguu kuvimba.

Kuna siku ilikuwa mchana nilikuwa nimepumzika ndani. Sijui nini kilitokea mpaka sasa hivi sijuagi kama nilikuwa nipo kwenye ndoto au nilikuwa vipi. Nilijikuta nimechukuliwa mpaka makaburini na mzee mmoja ambaye huyo mzee alikuwa tayari ameshakufa alikuwa naishi mtaani kwetu pale. Ndo nilijikuta nipo naye akawa ananiambia unajua dawa ya ugonjwa wako ni nini.

Nikajibu sijui mzee wangu nateseka saana na ugonjwa huu mimi ni wakufa tu akajibu apana wewe sio wakufa
Dawa ya ugonjwa wako ni jiwe ili akanipa jiwe fulani hivi jeusi akaniambia nimeze jiwe ilo nitapona. Nilimeza jiwe hilo halafu baada ya hapo nikajikuta nimeamka.

Kufika jioni nilianza kutapika damu kuharisha damu walinikimbizi hospitalini watu walikuwa wameanza kulia nyumbani kwetu maana walijua mwisho wangu umefika. Nilipelekwa huko hospitalini. Nilifanya siku 4 sijui mchana ni upi au usiku ni upi nilikuwa nimezimia.

Madokta nao walikuwa wanasubiri moyo usimame tu maana wazee wangu walikuwa hawana pesa za matibabu ambayo walikuwa wanaomba. Baada ya wiki hali yangu ilianza kurudi polepole mpaka nikapona kabisa. Sasa hivi mimi ni mzima wa afya kabisa.

Ila mpaka sasa hivi najiulizaga maswali mengi kuhusu ndoto hile yule alikuwa Mungu alikuja kwa sura ya yule mzee au ni mambo tu wazee wetu.
 
Story kama hizi ngumu kumeza maana tumesikia nyingi sana, ungekuwa na cheti/vipimo kabla hujapona na baada ya kupona kutoka katika mamlaka inayoaminika ningeweza kuamini, na hongera sana kwa kuwa mzima wa afya tena baada ya kuteseka boss
 
Pole na hongera kwa kupona.

Mwishoni unakiri mwenyewe huna uhakika yule ni Mungu au lah ila kichwa cha Uzi unasema ni Mungu.

Bado unalo Hilo Jiwe uwaponye na wengine au Mungu anakupenda wewe tu wengine sio watoto wake? Itapendeza kama utaenda nalo Muhimbili pale kuwaponya na wengine waache kuteseka na madaktari waache kupoteza muda wao.
 
Katika watu ambao walikuwa wabishi kuhusu uwepo wa Mungu mimi wa kwanza na nilikuwa na sababu zangu

Ila mpaka sasa hivi najiulizaga maswali mengi kuhusu ndoto hile yule alikuwa Mungu alikuja kwa sura ya yule mzee au ni mambo tu wazee wetu.
Mkuu kwisha , kwanza pole kwa changamoto ulizipitia, na hongera kwa kupona. Ukiisha amini kuwa Mungu yupo na umepona kwa uwezo wa Mungu, kuwa na imani thabiti kuwa ni Mungu na usiendelee kujiuliza maswali maswali huyo babu ni nani, ulilishwa nini etc, maadam you are cured from your illness, then be firm mponyaji ni mmoja tuu, The One and Only HIM!.

Uponyaji wako ni kupitia mizimu ya mababu zako, ndio wenye mambo ya kupelekana makaburini na kulishana vitu!, ingekuwa ni Mungu, then ungetokewa na Mwanga tuu, kushtuka ungejikuta umetakasika na kupona instantly!.

Kitu usichokijua ni kilichokuponya sio huyo babu, sio safari ya makaburini wala hilo jiwe!, its you, wewe mwenyewe!. Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo? pia tembelea "Will Powers!", "Faith Healing!"-Nguvu za Kufanya Miujiza ya Uponyaji kwa Imani. Kila Mtu Anazo!

Ubarikiwe sana.
P
 
Ila si unaona mtu ukiwa mtu wa mizimu unaonekana mchawi na mtu asiyeelimika..somehow Inasaidia watu fulani kumbe.
 
Unatuchanganya. Umesema umeamini mungu yupo ila mwoshoni unajiuliza kama aliyekuponya ni mungu au mambo ya kiswahili. Kifupi bado hujaamini km mungu yupo.
 
Unatuchanganya. Umesema umeamini Mungu yupo ila mwoshoni unajiuliza kama aliyekuponya ni Mungu au mambo ya kiswahili. Kifupi bado hujaamini km Mungu yupo.
Kuna Mungu na mungu!, Japo umeandika mungu, najua ulimaanisha Mungu!. Kuliandika jina la Mungu kwa capital M ni somo la darasa la 3!, majina yote huanza na capital letter!. Hapo ukute wewe Mkuu The Nugget ni graduate wa LL.B mwenye 1st Class alafu umejoin LST!.
P
 
Bado hili halithibitishi uwepo wa Mungu. Kuendelea vzur baada ya kuumwa haihusiani na Mungu. Lazima kuna dawa ulitukuwa unatumia ndo zimekutibu. Ila ukweli unabaki pale pale Mungu hayupo. Ni Imani tu tulidanganywa na wakoloni. Ndo maana hujawahi kumuona Wala kumsikia akiongea, kwa sababa hayupo.
 
Back
Top Bottom