Nakimbia ndoa-Naogopa kuua

Nakimbia ndoa-Naogopa kuua

Kaka kwanza pole sana!

Unapitia kipindi kigumu. Katika maisha unapokuwa umempenda mtu na kujitoa kwa kila kitu juu yake na kisha mtu huyo akafanya mambo ambayo unaona ni tofauti ni lazima nafsi yako itaumia. Jambo ninaloliona kwako ni hili; inawezekana mwanamke huyo hakuwa amekupenda tangu mwanzo. Mtu huyo alikubali kuwa na wewe na kukuonyesha kuwa anakupenda kutokana na hali yake ya kimaisha na wewe ulimpenda kutokana na unyonge wake na kujitolea kila kitu. Hili si jambo baya-kumpenda mtu na kumsaidia. Lakini, kwa upande mwingine upo uwezekano kuwa mwanamke huyo alikupenda kweli ila kama unavyojua hulka za binadamu za kubadilika; mazingira ya kufanikiwa na uwezo wa kifedha na matamanio yamemfanya abadilike; upo uwezekano anakuona humvutii tena kuwa kuna watu kwa mtazamo wake anawaona wanamfaa kuliko yeye na amekuchoka. Mapenzi yameonesha tabia hiyo kihistoria, unaweza ukapendana na mtu leo, mkapendana kwa kiasi kikubwa kiasi cha kwamba mkaona hamuwezi kuachana daima, lakini inatokea bila kujua wala kupenda mnachokana au mmoja anamchoka mwenzake. Aidha, inaweza ikawa ni ulimbukeni, kuna watu huwa hawakui anabadilika miaka tu lakini akili za kishamba; na anajikuta anachezewa na kila mtu kirahisi.

Uamuzi wa kuachana nae si mbaya ila usiufanye kwa hasira, wala usiumize kichwa kufikiria gharama ulizotumia; haya ndiyo maisha, na hizo ndio changamoto.Tulia, mshukuru MUNGU kuwa uhai. Ongea naye kwa utulivu mwambie kwa namna mnavyoenda unaona ni vyema mkatengana kwa amani hiii ni kwaajili ya afya yako. Fanya mambo yako na bado naamini utampata mtu mwingine wa kuishi naye kwa amani. Kuhusu watoto pangeni utaratibu.

Kaka katika maisha tumezaliwa watupu tutaondoka watupu; nakuhakikishia kuwa hata siku yakufa huwezi kuzikwa na mtoto wala hela wala mali ulizozichuma so the game is kupata na kupoteza ulimpata, ukampenda mapenzi yameisha, iruhusu nafsi yako kukubaliana na hali halisi.

GININGI
 
duh kuoa nao kazi jaman hv nntaoa kwel mana me sipendi hizo stres zinikute
 
Wana jf....mi nimeoa na nina watoto wa3. Huyu binti nilimtoa kwao nikawaahidi wazazi wake kua nitamsomesha mpaka elimu yeyote. Nikafanya hivyo mpaka sasa yupo na kazi. Ila kwa bahati mbaya mimi karibu mwaka sasa sina kazi ila pesa za kula hazinikosi.

Huyu binti wakati naenda kumtambulisha kwetu alinifanya nikosane na ndugu zangu wote. Lakin kwa kua nampenda nilisimamia show mpaka wakanielewa. Maisha yetu mimi na yeye yamekua ya magomvi sana kwa takriban miaka 7 sasa. Hakuna tulichofanya cha mafanikio mpaka muda huu.

Magomvi yetu mengi yamekua ni tabia za unafki,uzinzi,uongo,dharau,majibu mabaya ya kutia hasira na kutojali wala kumthamini mtu. Ni mzuri sana wa kuomba msamaha ambapo baada ya kuomba msamaha hurudia kitu kile kile alichofanya baada ya muda mfupi.

Sasa maisha yamebadilika sana....baada ya yeye kua na kibiashara ambacho kinamuingizia pesa licha ya anazopata kwenye mshahara. Unachomweleza hakusikii hata kidogo. Anajifanya yeye ndio yeye...misheni town...kugawa namba ovyo kwa wanamme...kua na namba tofautitofauti ambazo hata mimi sizijui ambazo huzitumia kuwasiliana na wanamme zake wa nje.

Kiukweli mpaka time hii....nimewahi kumfuma akicheat zaidi ya mara 7. Akiwasiliana na wanamme wapya au ma X zake. Ni mtu wa iringa. Anakiburi sana na dharau ya hali ya juu. Hajali kama tunawatoto au la.

Hutoa majibu ambayo hunifanya nipate hasira sana na ikafikia mahala nikampiga kama mara 3 ivi. Na jana ilikua mara ya nne. So nimefikiria sana na nimeona ngoja nikimbie mji nimwachie kila kitu niende ninakokujua.

Kwa hasira nilizokua nazo jana....nimemwambia...hata akisikia nimekufa...asije kuniona...wala mimi sitakuja kumuona. Koz kama ni kunipotezea muda kanipotezea muda mwingi sana na gharama nyingi sana. Lakin zaidi ya yote ni kuhusu watoto wangu ambao sikutaka kabisa waishi ktk malezi mabovu kwasababu yake.

Nawashauri wanawake wenye tabia hizi waache. Malipo ni hapa hapa. Mtu akikutoa ujinga usimdharau.

Pole sana mkuu...ushauri wangu ni kwanza achana na huyo mwanamke atakuletea matatizo makubwa sana katika maisha yako potelea mbali sahau yote yaliyopita i.e. gharama na muda uliopoteza...and focus on providing for ur 3 wonderful kids (mtapanga utaratibu). Kama utapenda na uwezo wa kifedha unaruhusu waweza tafuta mwanamke mwingine atakae kufaa mkaanza maisha upya, ukiongeza watoto wa 2 wengine sio dhambi. Best of luck.
 
mmhh.. sisi ambao hatujaoa bado tujifunze vitu kama hivi kutoka kwa rafiki zetu..

4 years to come.... ntaweka mke ndani na mimi!
 
Mmmmmmmmh! *Covers face from shame!*

Huyo dawa yake wala si kukibia na kumuachia jiji ajitanue! Dawa yake ndogo sanaaa! We tafuta nyumba ndogo hapo hapo jirani utiize ule usemi ULIKIONA CHA NINI, WENZIO WASEMA WATAKIPATA LINI? Atanyooka kama nguo mbichi iliyopigwa pasi!

I realy do feel mercy for the kids! Wataisoma namba, chezea baba wa kambo na mama wa kambo!

Huu ndio ushauri wa kufuata! komaa nae maka kieleweke, kama uliweza kufanya yote utaweza tu! Dawa ya Bishoo ni kuwa bishooo zaidi yake!
 
Kaka kwanza pole sana!

Unapitia kipindi kigumu. Katika maisha unapokuwa umempenda mtu na kujitoa kwa kila kitu juu yake na kisha mtu huyo akafanya mambo ambayo unaona ni tofauti ni lazima nafsi yako itaumia. Jambo ninaloliona kwako ni hili; inawezekana mwanamke huyo hakuwa amekupenda tangu mwanzo. Mtu huyo alikubali kuwa na wewe na kukuonyesha kuwa anakupenda kutokana na hali yake ya kimaisha na wewe ulimpenda kutokana na unyonge wake na kujitolea kila kitu. Hili si jambo baya-kumpenda mtu na kumsaidia. Lakini, kwa upande mwingine upo uwezekano kuwa mwanamke huyo alikupenda kweli ila kama unavyojua hulka za binadamu za kubadilika; mazingira ya kufanikiwa na uwezo wa kifedha na matamanio yamemfanya abadilike; upo uwezekano anakuona humvutii tena kuwa kuna watu kwa mtazamo wake anawaona wanamfaa kuliko yeye na amekuchoka. Mapenzi yameonesha tabia hiyo kihistoria, unaweza ukapendana na mtu leo, mkapendana kwa kiasi kikubwa kiasi cha kwamba mkaona hamuwezi kuachana daima, lakini inatokea bila kujua wala kupenda mnachokana au mmoja anamchoka mwenzake. Aidha, inaweza ikawa ni ulimbukeni, kuna watu huwa hawakui anabadilika miaka tu lakini akili za kishamba; na anajikuta anachezewa na kila mtu kirahisi.

Uamuzi wa kuachana nae si mbaya ila usiufanye kwa hasira, wala usiumize kichwa kufikiria gharama ulizotumia; haya ndiyo maisha, na hizo ndio changamoto.Tulia, mshukuru MUNGU kuwa uhai. Ongea naye kwa utulivu mwambie kwa namna mnavyoenda unaona ni vyema mkatengana kwa amani hiii ni kwaajili ya afya yako. Fanya mambo yako na bado naamini utampata mtu mwingine wa kuishi naye kwa amani. Kuhusu watoto pangeni utaratibu.

Kaka katika maisha tumezaliwa watupu tutaondoka watupu; nakuhakikishia kuwa hata siku yakufa huwezi kuzikwa na mtoto wala hela wala mali ulizozichuma so the game is kupata na kupoteza ulimpata, ukampenda mapenzi yameisha, iruhusu nafsi yako kukubaliana na hali halisi.

GININGI

Mkuu fuata ushauri wa @lara1 , Tulizaa akili jipange tu kila kitu kitakwenda sawa! ukihadithiwa yaliyowakuta wenzako unaweza sema ww, una nafuuu! so komaa tu!
 
mkuu pole,jambo la busara ni kumuacha huyo mwanamke coz atakuletea magonjwa,angalia ni vp utalea watoto wako.
 
Mkuu.hili ni tatizo ulilolitengeneza mwenyewe ,tabia njema uzipendazo mwalimu wake mkuu ni wewe. Harufu mbaya ya uozo ulianza kuisikia zamani na wewe hukutaka kuchunguza ili kubaini harufu inatokea wapi.pole Sana tafuta njia nzuri na sio kukimbia tatizo. Maana hata ukiki
Bia anaweza kukufata huko huko akidai wewe ni mume Wake. Kuhusu ushauri wa kuwa na nyumba ndo
 
mh! mkuu, kuachana sio suluhu nzuri. usimwache au kukimbia. kama mmeshindwa kufanya suluhu ushauri wangu tafuta nyumba ndogo jirani au hapo mtaani. na ikiwezekana hata rafiki yake. hiyo itamuuma sana, na ataomba mfanye suluhu.
 
jf ni zaidi ya google !
abbas-hassan yaani ulivyoongea tu hapo, ninakufahamu, ulimsomesha chuo kikuu, unakaa jetrumo dsm, yeye anafanya kazi afisa mambo ya elimu, anasafiri sana mikoani, wewe ulikuwa unafanya kazi zamani katika ubalozi fulani hivi hapa dsm, uliachishwa kazi, na una kisukari, dada ana hela za kutosha tu na mmejenga nyumba yenu nzuri sana huko jet. yeye mtu wa iringa, wewe ni mngoni. hadi nakuonea huruma.

kumfumania mwanamke mara 7 yahitaji ujasiri. mwombe Mungu usiingie majaribuni ukaja kujutia maisha yako yaliyobaki, usichukue uamuzi mbaya kwani utakugarimu.
 
Mama kawachagulia watoto maisha mapya, sasa unataka kuteseka kwa sababu gani. Mwachie watoto, na wewe anza maisha yako. Kwani watoto watakuwa wa kwanza kuishi maisha ya namna hiyo? Mkuu achana na zana za mpaka kufa wakati kuna shoruba kibao. Mimi hakuna ya mpaka kifo, mwanamke akileta za kuleta hata kama tunawatoto kumi, napiga chini. Maisha haya ni mafupi sana, yanashoruba za kiasili na ukileta hizi za kutengezwa na binadamu si ndo inakuwa balaa. Chukua hatua mkuu ila usiue.
 
pole sana kaka inaonekana pesa zako zilikosa kazi ukaamuwa kwenda kusomesha mwanamke,nyie mbona mko wengi sema wengine wanakufa na tai zao shingoni.
 
Umeambiwa na nani ulete historia ya abbas-hassan hapa, kama unamjua kihivyo siumpe ushauri afanye nini, kuanza kusema mwenzio mara aliachishwa kazi, ana kisukari ni nini? mbona mwenyewe hajasema hayo?
uzuri wake ni kwamba, jamaa hilo jina la abas hassan ni bandia, sio jina lake hasili. na wala sijamtaja jina makusudi kwasababu watu wachache sana wanamfahamu. hana kazi yeye kwa sana anaishi kwenye nyumba ya huyo mwanamke aliyojenga, kazi yake yeye ni kutunza tu mifugo ya kuku wa kisasa home kwani kibarua kilishaisha ubalozini kama dereva. mwanamke huyo alimwokota kabisa hopeless hana mbele wala nyuma akamsomesha, chuo kikuu udsm alimsomesha, alisoma education akafundisha pugu, akaacha na kuingia wizara ya elimu. mwanamke anagawa ile mbaya ana kiburi ajabu na ni mara chache anakuwepo home anasafiri sana mikoani anaweza kukaa wiki,miezi etc kikazi. pesa ipo, ila ndo hivyo mwanamke amesahau kuwa usomi na hela alizonazo mme wake alijinyima akamsomesha. tena wazazi wa mwanaume walimsema sana kwamba anamsomesha mwanamke gani huyo, mwanaume alikuwa faithful kwake, ila sasa naona upendo haupo..(kama ni yeye, manake sina uhakika kama kweli ninayemfikiria ni yeye).
 
Ningekuwa mimi kaburi lingekuwa limeishaota nyasi.
 
abbas-hassan Ulifanya nini mpaka ukawa uko nje ya kazi abbas-hassan? kama kuna kaufisadi kalichopelekea wewe kuondolewa kazini matunda ya huo ufisadi ulitumia na familia yako au na rafiki zako?
Hii sidhani kama ni muhimu mkuu...kazi za kuajiriwa yeyote anaweza kupoteza muda wowote....muhimu nadhani ni ushauri alotoa Lara 1 kutafuta msichana mwngne maeneo si mbali na kwako ili nae ajue...mbinu hii kaka yangu aliitumia na sasa ana wake wawili ila mke mkubwa ujinga ulishamuisha kwa kiasi kikubwa japo kuna matatizo ya hapa na pale...ila it worked out na kwa kweli yeye binafsi kaka imemsaidia haumii kwa maudhi alokuan anafanyiwa... jaribu hiyo uendelee kula maisha bhana hata kama si hulka yako
 
Mweee!! Mi naua under the defence of provocation s. 202 of the penal code! Punguza upole mtoe mmojawapo wa anaocheat nao sadaka ya kuteketezwa wengine watajifunza.
 
Pole sana mkuu,aisee!anyway familia yako(watoto) ni jambo la mhimu sana ila dharau ni jambo lingine,tena kubwa,kua mwanaume.
 
Back
Top Bottom