Nakimbia ndoa-Naogopa kuua

Nakimbia ndoa-Naogopa kuua

Kaka hayo nimapito na mungu atamlipa Sawa na ujira wke,cha msingi kaza buti wewe siwakwnza wala hutakua wa mwisho ,mdharau jbu zuri Ningumu ila jitahidi usimuulize aingiapo wala atokapo siku unakifaa lala,nilishamwambiaga shangazi angu narudi nyumbni ndoa imenishinda nikamwmbia mbna Ww umepata mume mzuri hvyo anakusaidia mpka kazi akasema mwnangu kua uyaone nikikwmbia yng utafunga mdomo ,yalitokea wap manake alinilea akasema mjomba ako alikua akiingiza mwanamke ndani mukiwa mumelala mimi nalala sebuleni alfajiri naenda kumuamsha ili amtoe watoto wasijue ndni ya miezi 8 nasikuwahi kusema leo nakwmbia ili ukavumilie yte mwanangu nimengi nikisema utamchukia mjomba ako ,ila ninavyosema hv nibaba 1mzuri mno anaempenda mkewe vbaya naniwa Lutheran masalia kwa sasa ,mshirikishe mungu Hamna gumu kwake usimpe shetani ushindi ,
 
ni kati ya nyuzi zilizonigusa sana,fuata ushauri wa Kipimapembe ni mzuri kulingana na hali uliyomo ya kutokuwa na kazi kwa sasa,Pole sana mkuu Mungu akusaidie sana ktk wakati huu,ntakuombea pia,duh laiti tungejua wenzetu watatugeukaje mbeleni....
 
lara 1 unaufahamu wimbo mmoja sikumbuki jina la kwaya ila wanasema

........watoto wa nyumba zote njooni tuungane
tuwalilie wazazi chozi la damu...........
haki ya malezi bora tumepoteza
urithi wa maadili tumepotezaa
ooh duniaaa dunia ooh tumekusea nini

beti ya 3 anasema

..............familia moja baba na mama watano...........

its a sad thing.

Mt.Kizito - Makuburi - Wimbo chozi la damu - Album Mungu yuleee.
 
Last edited by a moderator:
Mmmmmmmmh! *Covers face from shame!*

Huyo dawa yake wala si kukibia na kumuachia jiji ajitanue! Dawa yake ndogo sanaaa! We tafuta nyumba ndogo hapo hapo jirani utiize ule usemi ULIKIONA CHA NINI, WENZIO WASEMA WATAKIPATA LINI? Atanyooka kama nguo mbichi iliyopigwa pasi!

I realy do feel mercy for the kids! Wataisoma namba, chezea baba wa kambo na mama wa kambo!

Aseee!! haya ndio maneno sasa.
 
abbas-hassan yaani ulivyoongea tu hapo, ninakufahamu, ulimsomesha chuo kikuu, unakaa jetrumo dsm, yeye anafanya kazi afisa mambo ya elimu, anasafiri sana mikoani, wewe ulikuwa unafanya kazi zamani katika ubalozi fulani hivi hapa dsm, uliachishwa kazi, na una kisukari, dada ana hela za kutosha tu na mmejenga nyumba yenu nzuri sana huko jet. yeye mtu wa iringa, wewe ni mngoni. hadi nakuonea huruma.

kumfumania mwanamke mara 7 yahitaji ujasiri. mwombe Mungu usiingie majaribuni ukaja kujutia maisha yako yaliyobaki, usichukue uamuzi mbaya kwani utakugarimu.

Mkuu chukua hatua mtafute ukawasuluhishe, maana hili janga nimemwonea huruma sana jamaa, kama vipi nimwazime pistol.
 
Wadau nawaelewa sana. Ujue mpaka sasa akili imestack....sijui pa kwenda....sijui cha kufanya. Na roho ya mauti inaniwinda sana....bora nife...nyingine nenda hata Lindi ukaanze upya. Mara. ..we vumilia tu kidogo umuone ujinga wake.....kila jaribu lina mlango wake....kwamba soon nitapata ahuheni nitaondoka kuendelea na mambo yangu upya. Kama ni watoto ipo siku wakitaka kumjua baba yao watanitafuta.



Maskini watoto wanguuuuuu........Mungu waupushe na mabaya yote. Sikua na nia mbaya na huyu mwanamke. Kwa wema wote niliotenda mpaka kumtafutia kazi leo naonekana mburula.....ananidharau na kunijibu kunya??..NSSF nilimpa zaidi ya 80% ili afungulie biashara zake. Leo sina kazi ananiona mjinga kweli.........nipeni bastola wadau....nipeni tafadhali. Pls

Listen, kuwa karibu na Mungu wako, punguza ukaribu na mkeo kuminimize chances za mauzi. Epuka kushinda nyumbani wakati yupo. Tafuta shughuli yoyote ya maendeleo ya jamii ushiriki. Usiue, utawatesa watoto bila sababu za
msingi na pia dhambi za huyo umuuaye zitakuwa juu yako.

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 
kwanin ndoa nying (sio zote) ndugu walizotia mdomo huwa znakuja kuwa mbaya.......? Usiachane na mkeo, tengana nae. Mpe muda na jipe muda wa kujitathmini.

Sababu walishaona gap kubwa ya tabia na hulka kati ya wawili hao.

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 

kwa hiyo akimbie nyumba kisa mwanamke?
hayajakukuta wewe!!

Kisa mwanamke....! Yes kisa mwanamke...unataka afanye nini analea nini hapa kama si kuendelea kunyanyasika tu. Kaka tafuta room 2 sehemu tulia huko weka vizuri mipango yako tengeneza bond nzuri na wanao kama ni wakubwa waeleze kila kitu....achana na huyo limbukeni atakuambukiza ukimwi bure
 
Kaka kwanza pole sana!

Unapitia kipindi kigumu. Katika maisha unapokuwa umempenda mtu na kujitoa kwa kila kitu juu yake na kisha mtu huyo akafanya mambo ambayo unaona ni tofauti ni lazima nafsi yako itaumia. Jambo ninaloliona kwako ni hili; inawezekana mwanamke huyo hakuwa amekupenda tangu mwanzo. Mtu huyo alikubali kuwa na wewe na kukuonyesha kuwa anakupenda kutokana na hali yake ya kimaisha na wewe ulimpenda kutokana na unyonge wake na kujitolea kila kitu. Hili si jambo baya-kumpenda mtu na kumsaidia. Lakini, kwa upande mwingine upo uwezekano kuwa mwanamke huyo alikupenda kweli ila kama unavyojua hulka za binadamu za kubadilika; mazingira ya kufanikiwa na uwezo wa kifedha na matamanio yamemfanya abadilike; upo uwezekano anakuona humvutii tena kuwa kuna watu kwa mtazamo wake anawaona wanamfaa kuliko yeye na amekuchoka. Mapenzi yameonesha tabia hiyo kihistoria, unaweza ukapendana na mtu leo, mkapendana kwa kiasi kikubwa kiasi cha kwamba mkaona hamuwezi kuachana daima, lakini inatokea bila kujua wala kupenda mnachokana au mmoja anamchoka mwenzake. Aidha, inaweza ikawa ni ulimbukeni, kuna watu huwa hawakui anabadilika miaka tu lakini akili za kishamba; na anajikuta anachezewa na kila mtu kirahisi.

Uamuzi wa kuachana nae si mbaya ila usiufanye kwa hasira, wala usiumize kichwa kufikiria gharama ulizotumia; haya ndiyo maisha, na hizo ndio changamoto.Tulia, mshukuru MUNGU kuwa uhai. Ongea naye kwa utulivu mwambie kwa namna mnavyoenda unaona ni vyema mkatengana kwa amani hiii ni kwaajili ya afya yako. Fanya mambo yako na bado naamini utampata mtu mwingine wa kuishi naye kwa amani. Kuhusu watoto pangeni utaratibu.

Kaka katika maisha tumezaliwa watupu tutaondoka watupu; nakuhakikishia kuwa hata siku yakufa huwezi kuzikwa na mtoto wala hela wala mali ulizozichuma so the game is kupata na kupoteza ulimpata, ukampenda mapenzi yameisha, iruhusu nafsi yako kukubaliana na hali halisi.

GININGI
 
gfsonwin huo wimbo mara ya kwanza nlpouskiliza machozi yalinishuka bila hata kujua...
 
Last edited by a moderator:
Kwa jinsi ulivyohadithia nakushauri tu chapa lapa kaanze maisha upyaaaaa
 
Pole sana kaka, hawa viumbe ni balaa. Mwombe sana Mungu akuongoze pia usiwaache watoto kwani ni hatari kulelewa bila wazazi wote.
 
Wanawake wa Iringa ni kwanini hasa wanakua hivi?? Ni pepo?? Ulimbukeni?? Najiskia vibaya sana

Pole sana Mkuu ni mapito tu
 
ushauri wa kumwambia atafte nyumba ndogo sahv ni kutaka kumuua na kuwapoteza watoto wake wapendwa. Kwanza watakuwa wanashndana kwenda kwa "mahawara" watoto muda huo watabaki na nani? Pili nyumba ndogo kama mjuavyo hawalambi mikono mitupu, yeye hata kazi hana.
 
Inauma sana .we ndo ulimpandisha awe juu kama vp we mloge afilisike awe kama ulivomkuta heshima itarudi mahala pake
 
Kisa mwanamke....! Yes kisa mwanamke...unataka afanye nini analea nini hapa kama si kuendelea kunyanyasika tu. Kaka tafuta room 2 sehemu tulia huko weka vizuri mipango yako tengeneza bond nzuri na wanao kama ni wakubwa waeleze kila kitu....achana na huyo limbukeni atakuambukiza ukimwi bure

kwani akiishi na mwanamke nyumba moja
lazima ashiriki nae tendo?mpango wa kando
muhimu,na mkumbuke hiyo ni ndoa na watt kulelewa
na mama wa hivyo ni janga,akae kwa ajili ya wtt
ila mapenzi no
 
fact kwamba mpaka sasa hujamuua wala hujahama nyumba ni suala la kukupongeza sana..
 
Wana jf....mi nimeoa na nina watoto wa3. Huyu binti nilimtoa kwao nikawaahidi wazazi wake kua nitamsomesha mpaka elimu yeyote. Nikafanya hivyo mpaka sasa yupo na kazi. Ila kwa bahati mbaya mimi karibu mwaka sasa sina kazi ila pesa za kula hazinikosi.


Huyu binti wakati naenda kumtambulisha kwetu alinifanya nikosane na ndugu zangu wote. Lakin kwa kua nampenda nilisimamia show mpaka wakanielewa. Maisha yetu mimi na yeye yamekua ya magomvi sana kwa takriban miaka 7 sasa. Hakuna tulichofanya cha mafanikio mpaka muda huu.


Magomvi yetu mengi yamekua ni tabia za unafki,uzinzi,uongo,dharau,majibu mabaya ya kutia hasira na kutojali wala kumthamini mtu. Ni mzuri sana wa kuomba msamaha ambapo baada ya kuomba msamaha hurudia kitu kile kile alichofanya baada ya muda mfupi.


Sasa maisha yamebadilika sana....baada ya yeye kua na kibiashara ambacho kinamuingizia pesa licha ya anazopata kwenye mshahara. Unachomweleza hakusikii hata kidogo. Anajifanya yeye ndio yeye...misheni town...kugawa namba ovyo kwa wanamme...kua na namba tofautitofauti ambazo hata mimi sizijui ambazo huzitumia kuwasiliana na wanamme zake wa nje.



Kiukweli mpaka time hii....nimewahi kumfuma akicheat zaidi ya mara 7. Akiwasiliana na wanamme wapya au ma X zake. Ni mtu wa iringa. Anakiburi sana na dharau ya hali ya juu. Hajali kama tunawatoto au la.



Hutoa majibu ambayo hunifanya nipate hasira sana na ikafikia mahala nikampiga kama mara 3 ivi. Na jana ilikua mara ya nne. So nimefikiria sana na nimeona ngoja nikimbie mji nimwachie kila kitu niende ninakokujua.



Kwa hasira nilizokua nazo jana....nimemwambia...hata akisikia nimekufa...asije kuniona...wala mimi sitakuja kumuona. Koz kama ni kunipotezea muda kanipotezea muda mwingi sana na gharama nyingi sana. Lakin zaidi ya yote ni kuhusu watoto wangu ambao sikutaka kabisa waishi ktk malezi mabovu kwasababu yake.




Nawashauri wanawake wenye tabia hizi waache. Malipo ni hapa hapa. Mtu akikutoa ujinga usimdharau.

ndoa ndoano
 
Back
Top Bottom