Nakataa Tanzania haiwezi kuwa Nchi ya Uchumi wa Kati ifikapo 2025

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Habari zenu wakuu ,

Nchi yetu imekuwa ni ya mipango ya muda mrefu bila ukamilishaji kwa muda , na kupanga bila kuangalia mbele,

Ninaangalia nchi nyingi duniani huwa na mipango endelevu amnbayo uongozi urithishana na kama ajenda ya taifa, nina mifano ya mataifa yafuatayo ambayo miaka ya nyuma kidogo walikuwa kama Tanzania lakin kwa muda huu wako mbali sana ,

Naiangalia Malaysia walijiwekea miaka 20 ya kutimiza lengo lao kufikia mwaka 2020 wawe Uchumi wa juu,

Mpango huo si wakuandika kwenye makaratasi tu bali ni mipango endelevu na maono ya mbali kwamba ifikapo mwana 2020 wawe na nguvu zaidi kiuchumi katika ukanda wa Kusini mshariki mwa Asia,

Haiishii hapo hata katika maojiano ya vidoe ya Astro Awani, inaonesha benk ya dunia inaeleza jinsi nchi hiyo ilivyojipanga kipindi kile kimkakati kutekeleza jambo ilo kufikia 2020 na ukuaji wa uchumi wake ulivyo halisi,

Malaysia katika taarifa za uchumi wake ulitegemea zaidi
  • Huduma za Kifedha
  • Utalii
  • mafuta na Gesi
  • sekta ya afya
  • Elimu
  • Biashara
Ukiangalia asilimia kubwa ya mambo ya uzalishaji waliyo nayo malaysia sisi tunayo ya kutosha,

SISI KAMA TANZANIA TUNASHINDWA WAPI
1. Sera ya elimu ni mbovu sana tuwe wawazi hapa, elimu ya Tanzania bado haiendani na mazingira husika na muda husika wa mazingira halisi ya mtanzania, elimu ya Mtanzania haijajikita katika kumuinua mtu kutumia ujuzi wake kwa kulisaidia taifa lake kiuchumi,

2.Ukusanyaji wa kodi wa Nchi zilizotajwa hapo juu uko katika mfumo safi ambao unaeleweka, Taifa letu hatuna hata rekodi ya idadi ya wafanyabiashara, tunakusanya kodi kwa makadirio, TRA ni vurugu sana ,

3. Wapinzani wa maendeleo ndani ya Tanzania ni wengi kuliko wapinzani wa kisiasa, watu wanaotaka kuona Tanzania inafeli ni wengi kuliko wapinzani halisi wa siasa, hao hao ndo wapinga ununuzi wa Nyenzo muhimu za kuleta maendeleo

4. Serikali ya CCM haina consistency , aliyoyadhamiria kikwete hayajaisha uongozi wa mwaka huu una ya kwake pia, ni ngumu na inatufanya tusiendelee kabisa tunategemea sera za vyama badaala ya sera ya taifa, KKwa kifupi hakuna sera maalumu ya Taifa ili,

5. Rushwa bado ipo hasa katika miradi ya maendeleo, hapa ilibidi ipitishwe sheria kali dhidi ya wala Rushwa, lakin serikali ni kama inabagua baadhi wa ku deal; nao na inaacha wengine wakijiachia sana,

6. Siasa inachanganywa na utendaji, nashangaa Tanzania hakuna kiwanda kipya cha maana kimefunguliwa lakini naona idadi tunaambiwa mpaka sasa hivi kuna viwanda 3000??? vipi na vya wapi? hii yote ni kutaka kuwaridhisha watanzania wasioelewa au wasio na uelewa mpana juu ya masuala ya maendeleo,

7. Chama kinachoongoza nchi , kiongozi wake anatukuzwa badala ya kuheshimiwa, hii inapelekea hata ushauri kutolewa na washauri kwenda kwa mkulu kujihami na kuhami nafasi zao, wanamshauri kinafiki na uoga , hii imekuwa Tatizo,

8. Wapumbavu na wajinga bado ni wengi ndani ya raia wa Tanzania, yaan 70% ya watanzania hawana uwezo wa kusimamia ukweli, hasa vijana wengi wamekuwa wa kutumiwa kwenye siasa hata kama anajua ni uongo anaolazimishwa kuhusema, au kuuamini, leo hii utakuta vijana au watu wazima wanahama ajenda muhimu za nchi na kujadili speed ya ndege kutoka Canada, au wanajadili ujinga tu ,hii hapo sijaona kizazi cha kuleta mapinduzi ya viwanda na uchumi wa kati hakika,

9. Jumuiya za kimataifa zimeanza kunusa kitu Tanzania kupitia kakikundi kanakolipwa kuchafua image ya Tanzania, hasa kuna reporter wetu huyu wa BBC na DW, kuna jambo wanapaswa kuangalia wakati wa kutoa taarifa zao juu ya Tanzania, wawekezaji wengi wamepaogopa Tanzani kuwekeza, mpaka wengine wameanza kutukosoa, na wawekezaji wengine wameunguka moja kwa moja,

10. Mzunguko wa fedha na uwekezaji wa ndani kwa ndani umepungua mno hii iko wazi, hakuna mikopo tena, inatolewa kwa masharti makubwa mno, si vibaya kuhakiki lakini hela itengenezewe mfumo halali wa kuwa katika mzunguko,
naona aliyepanga Tanzania ya uchumi wa kati kufikia mwaka 2025 alikurupuka ama hakujua mipango,

11. Takwimu zetu ni za kubuni kwa baadhi ya mambo hata ya msingi, idadi ya raia haijulikani, watanzania tegemezi idadi yao ni ya kubuni, wazalishaji idadi yao ni ya kubuni pia, inakatisha tamaa, hata uhitaji wa taifa nao ni wa kubuni
hapo inabidi mipango iwe 2050 ndo tutaweza fika huko kwa kasi hii na ninavyoona

TUNATAKIWA KUWA NA AJENDA MAALUMU YA MAENDELEO YA TAIFA ILI, SI SIASA

Cc tindo
 
Hii ndio aina ya mijadala inayotakiwa kutawala kwenye majukwaa. Mambo mengi ya muhimu yameguswa kwenye huu uzi.
Muda sio mrefu utajaa siasa. Natamani tungejadili kwa kuweka kando mihemko.

Kwa kuwa mimi ni layman, huwa natamani tungekuwa na mpango wa miaka 30 ulioandaliwa na wataalamuna wabobezi wa kada mbalimbali, ili kila rais au utawalaunaoingia madarakani, lengo lao iwe kutekeleza mpango huo bila kujali chama kilichomuweka madarakani.

Hapo itakua rahisi hata kupima utendaji na kuwawajibisha walioko madarakani, vilevile kila anayetaka nafasi atajitafakari kama kwelie ataweza kutekeleza majukumu yake kwakuwa vitu tunavyovitarajia viko wazi.

Tukiendelea na huu mtindo mwingine akija anafumua kila kitu anaanza upya, kabla hajamaliza kuonyesha vipaji vyake, muda umeisha. Tukumbuke hatuna muda wote wala rasilimali zote za kupoteza kufanyia majaribio.
 
Comrade britanicca
....
Asante.
Nakuunga mkono kwa hisia kadhaa ikiwemo hii hapa...
Kufikia uchumi wa kati kwa nchi kama yetu inakuwa ni vigumu kutokana na mfumo wa siasa yetu kuwa tegemezi. Siasa tegemezi ni hii ya kila kiongozi kuingia madarakani akiwa na plan yake ya maendeleo.

Kwenye chama kuna ilani ya chama lakini kiongozi akikabidhiwa fimbo anaibuka na ilani yake binafsi.

Hali hiyo inapelekea wengine (leaders) wafikilie kuongeza umri wa kujaa madarakani kwa lengo la kutaka kutekeleza ilani yake binafsi na siyo ya chama.
 
Hakika mkuu tuna haribu sana katika mada tunaweka siasa zisizo kuwa na maana, ndo maana mpaka sasa Tanzania yetu hakuna wa kujua mwelekeo wa.nchi,

Kiongizi anaweza kuwa na maono.lakin ukweli ukawa kwamba sera zisizoeleweka na misingi isiyo vema ikamtoa kwenye mstari
 
Comrade britanicca
....
Asante.
Nakuunga mkono kwa hisia kadhaa ikiwemo hii hapa...
Kufikia uchumi wa kati kwa nchi kama yetu inakuwa ni vigumu kutokana na mfumo wa siasa yetu kuwa tegemezi. Siasa tegemezi ni hii ya kila kiongozi kuingia madarakani akiwa na plan yake ya maendeleo.

Kwenye chama kuna ilani ya chama lakini kiongozi akikabidhiwa fimbo anaibuka na ilani yake binafsi.

Hali hiyo inapelekea wengine (leaders) wafikilie kuongeza umri wa kujaa madarakani kwa lengo la kutaka kutekeleza ilani yake binafsi na siyo ya chama.
Ilo ni ukweli, hasa tatizo ili lipo nchi zetu za Swahili
 
Umesema vema sana mkuu
Pointi nyingi nimesepa nazo mfano pointi namba tatu:- Wapinzani wa maendeleo ndani ya Tanzania ni wengi kuliko wapinzani wa kisiasa.
Asante mkuu.
 
Mimi sababu ulizozitoa katika SISI KAMA TANZANIA TUNASHINDWA WAPI nimezielewa kabisa,
Haujataka kupindisha ukweli, umetaja Chama tawala, Rushwa, Takwimu za kubuni, sera mbovu.

Sasa baada ya kuainisha tulipokosea ungemalizia basi tufanyeje ili tutoke hapo. Naona umeachia hewani hewani tu
 
Kabisa uongo umezidi na matumaini hewa mtu unasema viwanda viko 3000 wakat havipo hiyo ni kuandaa watu ili update kura wakat kihalisia hamna kinachofanyika
 
Comrade britanicca
....
Asante.
Nakuunga mkono kwa hisia kadhaa ikiwemo hii hapa...
Kufikia uchumi wa kati kwa nchi kama yetu inakuwa ni vigumu kutokana na mfumo wa siasa yetu kuwa tegemezi. Siasa tegemezi ni hii ya kila kiongozi kuingia madarakani akiwa na plan yake ya maendeleo.

Kwenye chama kuna ilani ya chama lakini kiongozi akikabidhiwa fimbo anaibuka na ilani yake binafsi.

Hali hiyo inapelekea wengine (leaders) wafikilie kuongeza umri wa kujaa madarakani kwa lengo la kutaka kutekeleza ilani yake binafsi na siyo ya chama.
Ilani za chama ni za kisiasa mno zimetengenezwa kufurahisha watu wenye uelewa mdogo. Mfumo wake ni kama kadi ya harusi, imepambwa kwa mambo mengi mazuri watakayofanya pasipo kutumia watalamu wa uchumi wala kuangalia pato la Taifa. Mwisho haitekelezeki, baada ya muhula kwisha wanatoa ilani nyingime tena!!
 
Mimi sababu ulizozitoa katika SISI KAMA TANZANIA TUNASHINDWA WAPI nimezielewa kabisa,
Haujataka kupindisha ukweli, umetaja Chama tawala, Rushwa, Takwimu za kubuni, sera mbovu.

Sasa baada ya kuainisha tulipokosea ungemalizia basi tufanyeje ili tutoke hapo. Naona umeachia hewani hewani tu
Kusimama kwenye ukweli na mipango sahihi, kuwe navipaumbele vya kitaifa, sheria kali juu ya rushwaa, tuache kuichezea elimu kupandisha grade kila siku wala sio suluhu
 
Back
Top Bottom