Nakaribia kuhitimu chuo ila sijui kuhusu chochote nilichosomea

Nakaribia kuhitimu chuo ila sijui kuhusu chochote nilichosomea

Rudi uanze first year labda utaelewa mkuu..Elimu ya Tanzania ndio iko hivyo kariri kafanye mtihani pata GPA kubwa na nzuri nenda zako..
 
sio wewe tu, wanasema hata huko marekani kati ya wahamiaji wote, watu weusi wenye asili ya afrika ndio wamesoma (shahada etc) kuliko watu wenye asili ya china, india etc lkn hawana impact yoyote...

we maliza tu utafanikiwa...
ila baada ya chuo, amini ndio unaanza elimu
Asilimia kubwa ya watu wa Marekani ni wahamiaji. Watu wa asili wa nchi hiyo ni Wahindi Wekundu, wazungu walihamia huko na kuwaua hao Wahindi ili kupata maeneo ya kuishi. Kwa mantiki hiyo basi, kati ya wahamiaji wote, ni wale wenye asili ya wazungu ndo wamesoma sana hizo degree.
 
Nipo mwaka wa tatu naenda wanne lakini sijui chochote kile ninachokisomea yani mi ni mtu wa kukariri kwa kwenda mbele pepa ikiisha nasahau vyote.

Na semester ikiisha ndo kabisa nasahau kabisa nilichojifunza semester nzima.

Mbaya zaidi hata vitu nilivyosoma advance navyo kama nilipita patupu yani nipo mweupe peee kama karatasi.

Sasa naona kabisa nikiajiriwa nitaaribu kazi za watu tu.

Sasa nipeni ushauri nifanyeje kuacha chuo siwezi naona nitakosa title mtaani , lakini nachokisoma sikielewi nashindwa hata ambao hawakwenda shule kabisa angalau wao wana mwangaza kuliko mimi.

Kama utaajiriwa fuata maelekezo ya kazi. Pia jisomee mwenyewe vile ambavyo utahisi unavihitaji katika kazi yako. Tafuta maandiko ambayo ni maalum kwa profeasionals, watu ambao wako kazini, maandiko ambayo yako simple.
Yaani ukiwa kazini usisome tu andiko eti kwa sababu ni la field yako maana utakutana na maandiko ambayo yaliandaliwa kwa ajili ya watu ambao wako chuoni, hapo utarudi kule kule kwenye complication.

Kama utataka kujiajiri (hutaki kuajiriwa), ukijua kusoma English na ukaielewa utakuwa una nyenzo nzuri sana. Soma vitabu, jichanganye na watu unaohisi wamekuzidi kimafanikio katika kile unachokitafuta. Ila huku kwenye kujiajiri unatakaiwa usiwe na mihemko, maana si kwamba utakachokifanya mara moja utafanikiwa. Unaweza kufeli mara nyingi tu ila unachotakiwa ni kujifunza kutokana na kufeli kwako. Hali hii itakujenga na kadri siku zinavyokwenda utajihisi ni mtu tofauti sana.

Pamoja na haya yote niliyoeleza, maisha yako yatatokana na wewe unataka uwe NANI.

Kwanza jiulize, "NATAKA KUWA NANI", Kisha fuata njia itakayokufanya kuwa huyo mtu.

Hayo ni kwa uchache tu.
 
Vyuo vilipokaribisha maswali mengi ya 'select and choose' na kuondoa maswali mengi ya 'why, explain, define, proove etc' kwenye ue, matokeo ndio hayo.
 
Nipo mwaka wa tatu naenda wanne lakini sijui chochote kile ninachokisomea yani mi ni mtu wa kukariri kwa kwenda mbele pepa ikiisha nasahau vyote.

Na semester ikiisha ndo kabisa nasahau kabisa nilichojifunza semester nzima.

Mbaya zaidi hata vitu nilivyosoma advance navyo kama nilipita patupu yani nipo mweupe peee kama karatasi.

Sasa naona kabisa nikiajiriwa nitaaribu kazi za watu tu.

Sasa nipeni ushauri nifanyeje kuacha chuo siwezi naona nitakosa title mtaani , lakini nachokisoma sikielewi nashindwa hata ambao hawakwenda shule kabisa angalau wao wana mwangaza kuliko mimi.
Dah pole sana mdogo wangu. Nahisi you have been psychological tortured na hili jambo kwa mida mrefu. Inawezekana kipindi cha nyuma ulikuwa vizuri na ulikuwa na vision ya what kind of man you wanna be hapo baadae ika kuna jambo linakusumbua linalokukatisha tamaa ya maisha yako academically. Nakushauri uende kwa kiongozi wako wa imani I mean kama ni mchungaji au shekhe nenda mueleze nae atakupa angalizo.
Pole sana
 
TATIZO KUBWA SANA HILI NCHINI.

LAKINI SIDHAN KAMA UPO EMPTY
KABISA... MALIZA CHUO WALA USIACHE ... UKIFIKA MDA WA AJIRA NDIO UTAJUA KAMA KWELI WEWE HUJI KITU.... KAZANA KUSOMA ..

KWAHERI
wanafunz wengisana waliohitimu f4 f6 kuanzia 2000 mwaka huo had I sasa wako hivyo...

kama nitaeleweka baada ya kufanya mabadiliko mwaka huo hata marking scheme zilibadilika...wahitimu wakaanza jufaulu Sana...kabla ya miaka hiyo around 2000. 2001 ufaulu ukaimarika chemistry kupata C History A Lev kupata D sio lelemama.

hata product zilianza kutoka vimeo. walimu vimeo
 
Nipo mwaka wa tatu naenda wanne lakini sijui chochote kile ninachokisomea yani mi ni mtu wa kukariri kwa kwenda mbele pepa ikiisha nasahau vyote.

Na semester ikiisha ndo kabisa nasahau kabisa nilichojifunza semester nzima.

Mbaya zaidi hata vitu nilivyosoma advance navyo kama nilipita patupu yani nipo mweupe peee kama karatasi.

Sasa naona kabisa nikiajiriwa nitaaribu kazi za watu tu.

Sasa nipeni ushauri nifanyeje kuacha chuo siwezi naona nitakosa title mtaani , lakini nachokisoma sikielewi nashindwa hata ambao hawakwenda shule kabisa angalau wao wana mwangaza kuliko mimi.
Post zako Jf ni kielelezo tosha cha wewe ni nani
 
Nakuhakikishia hauko peke yako sema wewe ni honest tu umeusema ukweli
 
wewe si bure,utakuwa umechezewa na wabaya mtaani kwenu,
kwanza fanya juhudi uhame ulikokuwa unaishi au unapoishi tika ukiwa advance,pili nenda ukakemewe madudu yapotee
 
Acha woga Dogo hata maprofesa wetu wapo kama wewe chamsingi jifunze ujue English tu tayari utakuwa bonge la msomi kila MTU atakusujudia
Baada ya kujua English, soma vitabu vya aina nyingi na vihusuvyo mambo unayopenda. Vitakufungua kwenye suala zimaa elimu.
 
Wewe ni huna tatizo lolote. Mbona unakumbuka kuwa ulisoma hadi advance. Kama kichwa kingekuwa sio kinzuri ungesahau. Tatizo kubwa ni mfumo wa elimu Tz Ndio unalazimisha mwanafunzi ajali mitihani kuliko kuelewa.
 
TATIZO KUBWA SANA HILI NCHINI.

LAKINI SIDHAN KAMA UPO EMPTY
KABISA... MALIZA CHUO WALA USIACHE ... UKIFIKA MDA WA AJIRA NDIO UTAJUA KAMA KWELI WEWE HUJI KITU.... KAZANA KUSOMA ..

KWAHERI
Unawaza ajira eti
 
umesoma pharmacy tena chuo kikubwa namna hiyo na haujui ulichosomea, utawapaje watu dawa sasa? basi upelekwe milembe unaweza kuwa hujui kama wewe ni chizi.
Aisee hata me nimeshangaa...au hayuko makini
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom