Nakaribia kuhitimu chuo ila sijui kuhusu chochote nilichosomea

Yeezy 666

Member
Dec 11, 2017
38
74
Nipo mwaka wa tatu naenda wanne lakini sijui chochote kile ninachokisomea yani mi ni mtu wa kukariri kwa kwenda mbele pepa ikiisha nasahau vyote.

Na semester ikiisha ndo kabisa nasahau kabisa nilichojifunza semester nzima.

Mbaya zaidi hata vitu nilivyosoma advance navyo kama nilipita patupu yani nipo mweupe peee kama karatasi.

Sasa naona kabisa nikiajiriwa nitaaribu kazi za watu tu.

Sasa nipeni ushauri nifanyeje kuacha chuo siwezi naona nitakosa title mtaani , lakini nachokisoma sikielewi nashindwa hata ambao hawakwenda shule kabisa angalau wao wana mwangaza kuliko mimi.
 
Nipo mwaka wa tatu naenda wanne lakini sijui chochote kile ninachokisomea yani mi ni mtu wa kukariri kwa kwenda mbele pepa ikiisha nasahau vyote

Na semester ikiisha ndo kabisa nasahau kabisa nilichojifunza semester nzima .

Mbaya zaidi hata vitu nilivyosoma advance navyo kama nilipita patupu yani nipo mweupe peee kama karatasi.

Sasa naona kabisa nikiajiriwa nitaaribu kazi za watu tu .

Sasa nipeni ushauri nifanyeje kuacha chuo siwezi naona nitakosa title mtaani ,lakini nachokisoma sikielewi nashindwa hata ambao hawakwenda shule kabisa angalau wau wana mwangaza kuliko mimi.
Usijali haupo peke yako hata unaowaoona makazini na hospitalini hawakujua pia wanapambana na hali zao hivyo hivyo ili mradi tonge liingie mdomoni.Umesahau wazee wa EXPANSION JOINT nao ni kama wewe tu na hata baadhi ya walimu wako hapo chuoni hawajui wanachofundisha!
 
Usijali haupo peke yako hata unaowaoona makazini na hospitalini hawakujua pia wanapambana na hali zao hivyo hivyo ili mradi tonge liingie mdomoni.Umesahau wazee wa EXPANSION JOINT nao ni kama wewe tu
nashukuru kwa kunipa faraja
 
Nipo mwaka wa tatu naenda wanne lakini sijui chochote kile ninachokisomea yani mi ni mtu wa kukariri kwa kwenda mbele pepa ikiisha nasahau vyote

Na semester ikiisha ndo kabisa nasahau kabisa nilichojifunza semester nzima .

Mbaya zaidi hata vitu nilivyosoma advance navyo kama nilipita patupu yani nipo mweupe peee kama karatasi.

Sasa naona kabisa nikiajiriwa nitaaribu kazi za watu tu .

Sasa nipeni ushauri nifanyeje kuacha chuo siwezi naona nitakosa title mtaani ,lakini nachokisoma sikielewi nashindwa hata ambao hawakwenda shule kabisa angalau wau wana mwangaza kuliko mimi.

Hakuna anayejuaga, wanajuaga wakiwa kazini, elimu ya Tanzania ndivyo ilivyo, ndio maana wenye vyeti feki wamefanya kazi vizuri over 30 years, usiwe na wasiwasi kabisa, hautaharibu, na ukienda kuwa mjasiri!
 
Mkuu unatania au ndio unajaribu kuwa mkweli wa nafsi yako?

Bila kujali lengo la kuweka bandiko lako hapa JF. Lakini ukweli ni kuwa wapo watanzania wengi sana wenye hali kama uliyoelezea. Mfano jamaa yangu mmoja wa karibu alikuwa hivyo. Hata sasa miaka kadhaa bado anapiga simu kuniuliza vitu vidogo sana ambavyo tulijifunza chuo na sasa anashindwa kuvifanya na hajiamini kabisa kiasi kwamba haombi kazi zenye interview anatafuta kubebwa na mtu yani ile connection kupitia shemeji au rafiki n.k.

Huyo jamaa alifaulu vizuri sana bachelor degree yake kuliko mimi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom