Najuta kuoa mwanamke mlokole

Kwa kuwa amekuomba msamaha - msamehe na umpe mashart
Usirudie kumpiga - maana utaua
Nakupa pole kwa kuoa mashuka lakini ni uvivu wako - Hg yupo
Mtafute Rachel mpe ukweli ili unapotingwa - Ukajipooze
Usiachane nae maana utakuwa masikini - kugawana mali
Usipende kuwahusisha watu na kuwapa siri zako za ndani maana - wengi wanashida kubwa kuliko hizo upatazo
Tumia mtungi/bia zitakuongezea maarifa - ma biamed wapo na sio wasumbufu
Nakutakia maisha mema yenye uvumilivu - MAISHA NI VITA
 
Hahaha pole sana ndio mambo ya church hayo chakula cha paster
 
Kweli ushahuri mzuri mnooo, hii ni hekima ya kipekee kwa kizazi hiki cha nyoka!
 
Dear Brother.Divorce is not solution for a marriage.
 
katika umri wangu nilioishi mpaka sasa,nimegundua kitu kimoja...katika mapenzi nothing wrong nothing right.uamuzi wowote utakaofanya unaweza kuleta matokeo yeyote!umemchagua mlokole yametokea haya,pengine ungemchagua rachel nae angekutenda kwa style nyingine...labda yeye angekuletea mtoto sio wako kabisa!katika mapenzi we furahia tu matokeo yeyote utakayokutana nao..yawe mabaya au mazuri songa mbele as long as you are still breathing
 

Naomba niseme haya kama ushauri wangu kwako:

1. Siku zote thamani ya mtu hujulikana pale asipokuwapo. Lkn wakati ule akiwapo, aweza kudharauliwa, kukejeliwa, kupuuzwa, kubezwa na hata kutendwa kwa namna yoyote yenye kuonesha kama si kitu, lkn huwa si kwa wakati ule anapokuwa mbali au anapofariki. Tafakari!

2. Biblia inashauri kuooana watu wenye imani moja na si vinginevyo (2Korintho 6:14-18). Mungu alikusudia kuepusha migongano isiyo ya lazima kama iliyokupata.

3. Ndoa ya Kikristo haitanguliwi labda kwa kifo tu. Na hata ikitokea mmeachana, mnashauriwa kurudiana tena. (1Korintho 7:10-11)

4. Ninakuomba sasa wewe pamoja nà familia yako, mtafute kumwabudu Mungu ktk njia kwa iliyo ya kweli na inayotambuliwa na Mungu mwenyewe maana madhehebu yaliyojazana kila pembe hata duniani, mengi ni ya kuwapoteza watu. Kumbuka, miruzi mingi humpoteza mbwa. Mungu akusaidie kuitafuta njia ya kweli.

Ubarikiwe!
 
Mkuu kipigo kimemtosha mrudishe maana mpaka amerudi kuomba msamaha ujue kuna kitu amejifunza, sasa wee mwambie akija home ajue mume ni nani na mke ni nan na ajue kuwa biblia inatutaka kuabudu mara moja kwa juma
 
Ha ha ha hicho kipigo kwa mtu na dadake ni balaa
 

Kila kitu kinahitaji kiasi. La sivyo basi watu tungelala makanisani! Ni vema pia kuwa waanglifu na haya makanisa anayochipukia watu mpaka wanfilisika Watu wnauwa brainwashed Tuwe makini! Mfano kumuachisa motto kunyonya miezi 3!?!?
 
shida si ulokole , shida ni hilo dhehebu analosali, kunamadhehebu mengi sana ya kipepo siku hizi yanayotumia nguvu za giza,huwezi kuamini jinsi wanavyocheza na akili za watu.
Jua kwamba ufahamu wa mkeo ulishatekwa siku nyingi, cha msingi ni wewe ungepiga goti umlilie Mungu ufahamu wake urudi.

na rafiki yangu alitekwa kwa staili hiyo hiyo, uzuri mama yake alibaini mapema akaamua kuingia kwenye maombi, akazinduka akajua akaacha kwenda kwenye hilo kanisa, ndio ilikua pona yake.

tatizo watu wamekua wavivu wa kiroho wanataka tu kuombewa na kubandikiwa mikono na watumishi hata wasiowajua, badala ya kumtafuta mungu wenyewe na kulisoma neno la Mungu.



 
hm...pole kaka...kuna wanawake ambao wameokoka wanasahau kabisa kwamba yeye ni mke na ni mama pia..pole sana
 
Hivyo eeh? Haya basi hongera!

Ukienda kwa Joshua mwambie nampa hi.

Ulikuwa unampiga Yesu kijana. Tubu na kumuomba msamaha la sivyo ni nini kitakutokea. Mke anaenda kukuombea baraka kanisani wew unapiga? Wengine wake zao wana michepuko na wengine wanaenda kwa waganga ila wew unapata mvha Mungu unapiga. Nakusikitikia
 
Kanisa gani hilo wanataka hadi pyslip.? Jina la wachungaji?mshawishi ahame na kwa kifupi mshirikiane matumizi ndio utakuwa mwanzo wa maelewano,kwani makanisa ya kilokole siku hizi yameingiliwa na wasaka fedha,
 

Giza na Mwanga haviwezi katu kukaa pamoj. Kuna mistake hapo ilitokea tangu awali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…