Najuta kuoa mwanamke mlokole

Najuta kuoa mwanamke mlokole

Dah! Walokole weengi n kama wameshikiwa akili zao, manake wayafanyayo n tofaut na akili ya kawaida ya kufikiri, jamaa yangu flani pamoja na kupata zero form 6 pale kibaha baada ya kujaza vitu vya ajabu kwenye paper mpaka leo bado mlokole
Yaan kama vile wamemuazima mtu akili

yaani mtu baada ya maisha kumpiga ndo anajifanya mlokole, muda wote kanisani unafanya nini kama sio kudata, makanisa yenyewe haya ya kina lus.eke.lo
 
yaani mtu baada ya maisha kumpiga ndo anajifanya mlokole, muda wote kanisani unafanya nini kama sio kudata, makanisa yenyewe haya ya kina lus.eke.lo

Mkuu huwapend sasa walokole..dah
 
Kwa maelezo yako na uwelewa wangu nianze na jinsi ninavyo kuona:
  • Mosi, unaelekeakuwa una wivu wa kupindukia kiasi kuwa hupendi mkeo atoke nyumbani hata kwa kwenda kanisani.
  • Pili una udikiteta fulani, ndani mwako ni amri tu hakuna mjadala (negotiation), Unalotaka ndilo linakuwa.
  • Una mapenzi ya kizamani ya kikurya ambayo yanahusisha kupigana pigana.
Ulipaswa kabla ya kuoa, uchunguze kwanza: Unataka mke wa kushinda kwenye baa au saloon ama kitchen party, maana hawa nao wapo ni wewe tu na upendeleo wako. Si rahisi kumbadilisha mtu mlevi akawa mlokole na mlokole akawa mlevi hivyo ulipaswa upate ready made kuliko kutransform. Mkeo, licha ya mapenzi yako ya kizamani ya kupigana pigana, amekusamehe, anataka mrudiane wewe hutaki. Maana yake huna roho ya msamaha. Waswahili husema 'Asiye samehe haliwezi penzi.' Kumbe wewe huwezi penzi ingawa unaweza kupanda.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa uhuru wa kila mtu kuabudu imani aitakayo, lakini wewe unataka mkeo aabudu namna unavyotaka wewe, hivyo bila kujua, unataka kuwa juu ya Katiba ambayo ndiyo sheria mama ya sheria zote nchini. Masikini nduyu yangu hata hujui kuwa kuvunja Katiba ni kosa. Unaishi katika jamii ya watu wasiostarabika, wastaarabu huheshimu sheria zilizowekwa. Ni wanyama wa porini ndiyo wanaoishi kama unavyotaka wewe na mkeo muishi.
Sijazungumzia upande wa mkeo wala wazazi wake kwa sababu sijawasikia, lakini kubwa ni wewe uliyeomba ushauri na wao hawajaomba chochote. Ndoa ni taasisi inapaswa iheshimiwe na watu wote ukiwemo wewe mwenye ndoa. Mtu yeyote aliyemo kwenye ndoa hushawishiwa wakati wote na mtu mmoja mmoja vikundi vya watu marafiki mbalimbali wakike kwa wakiume, lakini wewe mwenye ndoa unapaswa kuwa na ushawishi mkubwa kushinda makundi yote. Tunapomshawishi mke hatumshawishi kwa mabavu, tunamshawishi kwa hoja huku ukinyunyiza juu yake UPENDO usiopatikana mahala pengine popote isipokuwa kwako tu

Umesema vema mkuu
Lakin umehalalisha tabia ya mwanamke..
Ila kimsing jamaa hapingani na iman ya mwanamke ila ratiba iliyo kisiri
 
Mkuu huwapend sasa walokole..dah

sio siwapendi bali nawajua a-z wengi ni wanafiki, nimekuwa nikihudumu kanisani kwa muda kiasi Mungu amlaze pema mchungaji wangu Samwel Chumu alinifundisha vitu vingi sana kuhusu hawa wanaojiita walokole na wachungaji wao wachumia tumbo
 
Mkuu unanikumbusha..mimi nlimfatilia msichana tulikuwa tunasali nae, alikuwa na tabia kama za huyu ila yeye hta smartphone alikuwa hataki et inawatsup so itamtia dhambin

Mwisho akawa anadate na mlez wa kikund church..
Paka leo sina ham naooooo
 
Makanisa mengine ni shida kwerikweri, ila mtu wangu usimuache wife kwa kosa linalowezarekebishika, cha kufanya ni kumweleza maisha yanavyotakiwa kwenda na akionyesha kukubaliana na matakwa yako ndoa na idumu. Ila shukuru umepata aliyepagawa na kanisa, siku ukipata aliyepagawa na waganga utakiona cha moto. Na hilo kanisa wanalosali ni lakilaghai, huwezi kusali bila kupumzika eti mnamtafuta Mungu! Ingekuwa hivyo basi wakae humohumo kanisani na wala wasifanye kazi na sadaka wasitoe ili hao wachungaji waombe kwa Mungu wao awashushie hizo hela.
 
Mkuu unanikumbusha..mimi nlimfatilia msichana tulikuwa tunasali nae, alikuwa na tabia kama za huyu ila yeye hta smartphone alikuwa hataki et inawatsup so itamtia dhambin

Mwisho akawa anadate na mlez wa kikund church..
Paka leo sina ham naooooo

ukweli lazima usemwe, kuna mmoja nilikutana naye tulipishana kama hatujuani, alivaa soksi imembana hatari wakati mwanzo alikuwa anazipiga vvita na kupondea, shame on them walokole!
 
Nimependa tu pale ulipomtengua dada wa mkeo mbavu...sikushauri chochote!
 
Haya makanisa yasiyokuwa na kichwa wala miguu ni hatari,kumbuka kwa sasa kwao ni kamali.
Achana naye lasivyo maendeleo kwako itakuwa sifuri.
Bora niendelee kusali lutherani aisee
 
Hata sijui unaomba ushauri wa nini kila kitu kipo wazi ulitakiwa uweke misimamo yako kabla ya ndoa achana na mke wako focus kwa Rachel kuna rafiki yangu yalimkuta mpaka akafikia mtoto wake kufariki mtoto anaumwa malaria mke wake anampeleka mtoto kanisani kuombewa mpaka mtoto akavuta achana kabisa na hiyo ndoa itapoteza mwelekeo wako wa maisha kabisaa.
 
Siku zote too much is harmful, katika hilo huyo mwanamke anafanya makosa makubwa. Unachotakiwa kukifanya ni kumtengeneza mkeo bila yeye kujijua kwanza mpe masharti kabla ya kumrudisha halafu muweke chini uongee nae friendly usiongee nae kama vile ni adui yako maana huwezi jua kwenye maombi pengine anakuombea mazuri. Ulivyokuwa unampiga na kumkaripia hiyo ilichochea yeye kuongeza nguvu ya kwenda kanisani kwa kujua kuwa ndoa yake inapita kwenye moto. Hicho ni kitu kidogo sana kudeal nacho kama mwanaume
 
But life is a very interesting game, MTU akioa mke anayetulia home analalamika oo mywifewangu golikipaflan ivi, kujibwetekea sake home, akioa mcharuko basi kila siku analalama kaibiwa, akioa chapombe basi ndo usiseme, akioa mfanyakazi analalamika all time yuko ofisini, wengi humu vihoro juu wakihofia wake zao kuchepukia kwa mabosi wao.

Basi Dunia vurugu, ukioa mpenda Dini ndo hivi Tena. Kwanini mnaoa si mkae tu msioe.?

Too much is harmful. Lazima kila jambo liwe kwa kiac. Umesoma vizuri huo uzi? Mtu anayeachisha kunyonya hata mtoto wake wa miezi mitatu kunyonya huyo hana hekima hata kidogo. Na mleta uzi hakatai mke kusali na kwenda kazini anachohitaji ni kutumia muda vizuri
 
dah! haya makanisa ya kilokole cjui wanawalogaga wa2 au ndo kucheza na akili zao tuu,,unadaiwa hadi salary slip??? kwel wajinga ndo waliwao
 
Kanisa linaomba pay slip?
damn it ....hii sio crime kabisa?

mkeo ni jukumu lako kumsaidia
mwambie mhame kanisa ndo sharti la kurudiana
 
Sijahalalisha, ila kinachotakiwa mume amshawishi mkewe kwa upendo. Mimi binafsi mke wangu alikuwa akisali kanisa fulani sitaki kulitaja, lilikuwa na ratiba kama ya mke wa mtoa uzi. Nilimwacha mke wangu akiendelea kusali kama kawaida huku nikimshawishi kujali familia yake kwa kutumia biblia ileile. Mungu ndiye mwanzilishi wa ndoa soma mwanzo. Mke anapaswa kumtii mumewe na mume anapaswa kumpenda mkewe kama mwili wake. Mtu amwenye upendo hawezi kuupiga mwili wake hadi kuutengua ubavu. Biblia inatuasa ' mke anayeishi na mume asiyeamini asimwache kwa maana mume aweza kuokoka kwa kuangalia matendo ya mkewe. Mke mwema ana wajibu wa kutunza familia yake kwa umahiri mkubwa.
Mwisho, kwa kuwa nilikuwa natumia pia mafundisho ya biblia, mke wangu akaona ni kweli. Dini inapswa iwe ile iletayo upendo katikati ya chuki, ilete faraja miungoni mwa wenye ndoa, ilete gundi ya kuwaunganisha badala ya kuwatenganisha, kwa maana imeandikwa 'alichokiunganisha Mungu mwanadamu asitenganishe. Biblia inasema tuonyane kwa upendo siyo kwa kutenguana mbavu. Shughuli nzima ya mapenzi ni ya kubembelezana, kama huwezi kubembeleza na kubembelezwa hakika huwezi mapenzi. Acha fanya kazi nyingine, lakini hakuna kazi nyingine mbala wa mapenzi
Umesema vema mkuu
Lakin umehalalisha tabia ya mwanamke..
Ila kimsing jamaa hapingani na iman ya mwanamke ila ratiba iliyo kisiri
 
makubwa madogo ya na nafuu kweli unampiga mtoto wa watu kisa nini jamani
si ungemwacha tu kwani yeye kaamua hivyo

si busara kuingilia uhuru wa mtu mwache afanye atakavyo yaani wewe unarushia ngumi utadhani
unapiga gunia kumbe mtu mwenye moyo na nyama kwanini wanaume mmekuwa mafisadiwa utu wa mtu?
 
haya maneno yako yamenipa motisha na yamenifanya nione kuwa kumbe wako watu mwenye busara kama wewe thanks mkuu
Sijahalalisha, ila kinachotakiwa mume amshawishi mkewe kwa upendo. Mimi binafsi mke wangu alikuwa akisali kanisa fulani sitaki kulitaja, lilikuwa na ratiba kama ya mke wa mtoa uzi. Nilimwacha mke wangu akiendelea kusali kama kawaida huku nikimshawishi kujali familia yake kwa kutumia biblia ileile. Mungu ndiye mwanzilishi wa ndoa soma mwanzo. Mke anapaswa kumtii mumewe na mume anapaswa kumpenda mkewe kama mwili wake. Mtu amwenye upendo hawezi kuupiga mwili wake hadi kuutengua ubavu. Biblia inatuasa ' mke anayeishi na mume asiyeamini asimwache kwa maana mume aweza kuokoka kwa kuangalia matendo ya mkewe. Mke mwema ana wajibu wa kutunza familia yake kwa umahiri mkubwa.
Mwisho, kwa kuwa nilikuwa natumia pia mafundisho ya biblia, mke wangu akaona ni kweli. Dini inapswa iwe ile iletayo upendo katikati ya chuki, ilete faraja miungoni mwa wenye ndoa, ilete gundi ya kuwaunganisha badala ya kuwatenganisha, kwa maana imeandikwa 'alichokiunganisha Mungu mwanadamu asitenganishe. Biblia inasema tuonyane kwa upendo siyo kwa kutenguana mbavu. Shughuli nzima ya mapenzi ni ya kubembelezana, kama huwezi kubembeleza na kubembelezwa hakika huwezi mapenzi. Acha fanya kazi nyingine, lakini hakuna kazi nyingine mbala wa mapenzi
 
Ndugu pole sana ila nakushauli kabla hujachukua maamuzi ya kuoa mwingne take time kwanza msome mwenzio yuko vip,anapendelea nini,tabia gan na hata ikibid ijue vyema ratiba yake. Maana unaweza kuta unaoa mwingine kumbe bora hata huyu wa kanisani. Yeye akawa anakesha bar,na night clubs maana kilaki2 ni mazoea.
 
Wewe ni tatizo kubwa. Unasema mkeo anatoka kazini saa kumi na moja jioni, halafu tena unasema anashinda kanisani 24/7....! Umeelewa ulichokiandika kweli?! Sijui unaishi mji gani, lakini wenzako wa dar unatoka kazini mda huo, unafika home kwenye saa mbili saa tatu, kutegemeana na unakoishi. Si afadhali huyo wako anapata muda wa kupita sehemu ya kusali kama ni kweli? Umekiri mwenyewe umekuwa ukimpiga mkeo mara kwa mara! Hadi umefikia kumpiga na kumtegua mbavu dada wa mkeo ambaye pia ni mke wa mtu! Unajitambua kweli? Wewe wa wapi??? Unajisifia hapa kwa kuwapiga wanawake! Una maadili gani wewe? Au dini yako ni bangi na pombe? Ingefaa pamoja na shutuma zako kwa mkeo, ungetaja hilo dhehebu unaloshutumu pia. Maana unaonekana kwa uongo pia hujambo. Pole.
 
Back
Top Bottom