Chaguzi mbili kuu pale unapogundua mkeo anakusaliti

Kambi ya Fisi

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
13,563
22,096
1. ACHANA NAYE na ulee watoto wako uliowapata ukiwa na mkeo. Unaweza kuamua kuoa mwanamke mwingine ama kubaki mseja daima.

Kumbuka ukiamua kuoa tena hutapata malaika mwingine bali utapata mke mwenye moyo kama wa yule utakayemuacha.

2. MSAMEHE mkeo kisha tafuta mtaalam wa kukusaidia kushughulika kuponya maumivu yako.

Weka mkakati wa namna bora ya kukusaidia usiingie katika mahusiano mapya.

Leeni watoto wenu pamoja hata kama mu wanandoa mliochana.

Vile utakavyo amua ni chaguo, huyo mwanamke ni mkeo ulimpenda ukamuoa, ni chaguo lako.

Kwa upande wangu binafsi ningechagua njia ya MSAMAHA kwa sababu mimi ni zao la msamaha. Yesu mwenyewe alisisitiza MSAMAHA 7×70 na wala hakusisitiza talaka, hivyo mie ninaishi ndani ya msamaha.

Pamoja na kumsamehe lakini ikitokea akaendeleza - maisha ya uzinzi - udanganyifu wa kudumu - hapo nitamwangusha kama kizazi cha moto. Lakini sitavunja ndoa yangu kwa sababu ya wingu linalopita.

Tafadhali usiue wala usijiue kwa sababu ya mkeo kukucheat bali chagua hatua mojawapo kati ya hizo mbili nilizozitaja.

Ubarikiwe.
 
1. ACHANA NAYE na ulee watoto wako uliowapata ukiwa na mkeo. Unaweza kuamua kuoa mwanamke mwingine ama kubaki mseja daima...
Ukifanya mazoezi ya kutosha ya kuwa mstahumilivu, basi utatoa msamaha wa kweli na kusahau kabisa mistakes za sio tu mkeo kwenye ndoa, bali pia katika mambo mengine katika maisha...

usipokua mstahimilivu, utasamehe lakini hutosahau mistakes ulotendewa.....

samehe na usahau, mbingu si hasira wataingia waTakatifu....
 
Ukifanya mazoezi ya kutosha ya kuwa mstahumilivu, basi utatoa msamaha wa kweli na kusahau kabisa mistakes za sio tu mkeo kwenye ndoa, bali pia katika mambo mengine katika maisha...

usipokua mstahimilivu, utasamehe lakini hutosahau mistakes ulotendewa.....

samehe na usahau, mbingu si hasira wataingia waTakatifu....
Ngedere yuko wapi? Tumemzoea
 
Imeandikwa wapi kwamba ukimuacha mwanamke mzinzi huwezi kupata mwanamke mwingine mwaminifu?
Naona Hujanielewa, nimeshauri ukiweza kubaki mseja fanya hivyo, Ila ikijifariji kuwa utapata mwingine mpya hiyo ni sawa na kucheza bahati nasibu, usishangae kupata mzinzi kwa mara nyingine.

Hakuna mwanamke malaika katika kuwaka tamaa
 
Yeye aachanaye na mke wake isipokua kwa sababu ya kuzin.........;

Nukuu manenohaya kuzin ni mtu kufanya mapenzi kabla ya ndoa au mwanandoa kuchepuka. Sasa bas kumbe hata Biblia imeandika kua isipo kua kuzini... Nukuuu neno isipo kua kwahiyo makosa yooote waweza samehe mkeo ndoa iendelee ila sio kuzini. Mkeo akikuchit jua tayar wewe nafas yako ndogo kumbuka mke hubebwa na performance yako katika tendo je unajua utam alio pewa?. Unajua alianza lin had umewafuma?

Ikiwa hujawai kumfumania mkeo usijipe maamuz kua nikimfumania ntakua hiv au ntachukua maamuz haya. Ila mwombe sana Mungu isikutokee na kama ikikutokea uchukue maamuz ya busara maana kamwe hakuna mwenye maamuz sahih kabla yatukio

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom