Mwana wa pori
Member
- Aug 13, 2022
- 12
- 12
Habari wakuu,kabla ya kuanza Uzi huu napenda kuwapa tahadhari kwamba story hii Haina chembe ya utunzi hata kidogo,
Miaka kadhaa nyuma baada ya kuzaliwa nikajikuta nikiwa naishi Mimi,mama yangu mzazi pamoja na baba wa kambo...katika kuishi huko sikua najua kwamba yule baba alikua ni baba wa kambo....maisha yakaenda hatimae nkaanza darasa la kwanza katika shule iliyopo hapo jiji la raha (dar es salaam) maeneo ya mikocheni A,
Sikufanikiwa kusoma hapo Kwa muda mrefu maana kulikua na utoro ambao mara nyingi uliletwa na mzazi wangu(mama) hivyo bibi yangu baada ya kupata taarifa hizo ikabidi anichukue na kwenda alipokua anakaa yeye huko dodoma mjini,nikafanikiwa kuendelea na elimu ya msingi mpaka miaka kadhaa nikawa nimemaliza elimu ya msingi shule ya chamwino B iliyopo hapo mkoani dodoma....baada ya kuhitimu elimu ya msingi nikafanikiwa kuendelea na elimu ya upili yaani sekondari,hapo sasa ndo nikaanza kuona mauzauza ya kuishi Kwa bibi....😭😭😭😭😭😭
Tukio la kwanza nilikua nimelala mida ya saa Tisa kasoro nikahisi jina langu linaitwa Kwa dirishani,nikawa nahisi kama naota mpaka nikajaribu kujifinya ngozi ndo nikagundua sio ndoto ni uhalisia,nikapiga kelele sana ila Cha ajabu hakuna mtu ambae aliweza kusikia ila baada ya muda akaingia bibi yangu akiwa anacheka Kisha akaniambia unaogopa nini?
Nilipatwa na hofu zaidi kuona anacheka,nakumbuka akaniambia funga mdomo wako usimwambie mtu kama Kuna kitu kimetokea,
Asubuhi nimeamka kama kawaida yangu ili nijiandae kwenda shule Ile naamka natoa mguu kitandani nashangaa kitanda chote kimelowa damu...😭😭😭😭
Nini kitaendelea fuatana nami za