Najuta kujenga kibanda changu uswahilini. Mswahili ni mtu duni sana

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,113
27,099
Baada ya kujibanabana hatimae nikajenga kibanda changu uswahilini.

Jirani yangu ana mpangaji wake. Huyo mpangaji wake ana mtoto mdogo (4yrs). Mimi nina watoto watatu mmoja la Saba wa kike wawili wakiume (5) and (3).

Sio kwamba Mimi ni mchoyo na mbinafsi, la hasha! Ila hakuna kitu nakichukia katika maisha yangu kama vikwazo. Hii familia ya huyu mtoto mdogo inashindwa kumdhibiti mtoto wao wa kike (4yrs).

Msosi umeiva huyo kaibuka. Tatizo sio chakula. Anakuta watoto wangu wanakula nimewawekea nyama kila mtu na vipande vyake Kwa bajeti yeye huyo mtoto doezi anafika anachukua plate ya chakula anan'gan'gania kisha anaanza kulia eti hataki watoto wangu wale. Hapo mama ake yupo nje.

Siku nyingine anatoka huko kwao anakuja kunywa maji kwangu. Akiwa anakula na wanangu wakitaka kunywa maji analia anataka yeye ndio awe wa kwanza kunywa.

Kero kero zipo nyingi sana. Mimi nilikuwa sina habari hizo cause sishindi home. Last week nimerudi home mapema nakuta madogo ndio wametoka shule halafu eti huyo mtoto analia hataki wao wale chakula walicho andaliwa na dada kazi kwamba kidogo apewe yeye tu.

Na analia kwa nguvu kama kachomwa na mkuki vile. Hapo mama ake yupo nje. Huwa naambiwaga upuuzi huu but sikuwahi kushuhudia. Nikasema hawa wanafanya huu ujinga kwasababu wananiona nimekaa Kikristo sana.

Basi nilimchukua huyo mtoto nikamnyanganya hiyo plate nikamshika nje hadi kwa mama ake nikaanza kumchana mama ake.

"Wewe Mwanamke msiniletee maswala ya ki...nge. Kwangu sio kituo cha kulelea watoto. Mtoto wako anafanya us..nge humkanyi.." Kuanzia leo sitaki kumuona mtoto wako nyumbani kwangu.

It was a surprise for her kwasababu nadhani alikuwa ananiona nimekaa kisomi kisomi na anavyosikiaga naweka ngoma za gospel kwangu basi anajua huyo Mtakatifu Matayo.

Basi kuanzia siku hiyo adabu imekuwepo. Mazoea hakuna tena. On top of that nimeanza kuwa napiga kwa nguvu nyimbo za kigumu.

Ngoma kama Hit 'Em Up na nyimbo nyingine za kigumu gumu ili at least wajue huyu jamaa msela hataki mambo ya kidwanzi.

Majirani kushirikiana kwenye mambo mengine sio kukerana kerana kiasi hicho. Kama una njaa njoo ukope hela umpikie mtoto wako sio kumuacha aje awakere watoto wangu.

Toto lako kula kwangu halafu siku likipata tatizo si ndio mwanzo wa kushikana uchawi huo. Sisi ngozi chafu huwaga sio wastaarabu kabisa

Ngoja nitafute hela nipige Mwanaukome. Ndio maana matajiri wakijenga nyumba zao huwa wanazipiga stop nonsense

#Walayhi nimeona umuhimu wa kuoa. Ukiwa na mke majirani hawawezi kufanya upuuzi kwa sababu wanajua mama mwenye nyumba Hawezi kukubali. Ila wakiwa wanakuona kibachela bachela hivyo wanakuchukulia ki-gentleman sana.
 
Mjukuu wa mwenye nyumba. 2 yrs old. Mimi naangalia sana katuni. First time nashangaa dogo huyo, nikamuuliza wewe nani akawa anataja jina ila simuelewi nikamtoa nje babu yake ndiyo akamtaja jina.

Naongea na babu yake yeye kasharudi ndani kwangu.

Sikuona tatizo. Balaa likaja kulilia remote, ukitaka kutoka anakuzuia, babu yake anasema niache funguo kwamba akimaliza kuangalia wafunge wanishikie funguo.

Nimelala nasikia hodi ya kugonga mlango kwa nguvu nafungua ni yeye, kaingia kafikia kujilaza kwenye kochi anasubiri tv. Namuambia mi nalala rudi baadaye ananijibu "Sitaki" hii wiki ya pili sijarudi nyumbani.
 
Msosi umeiva huyo kaibuka. Tatizo sio chakula. Anakuta watoto wangu wanakula nimewawekea nyama kila mtu na vipande vyake Kwa bajeti yeye huyo mtoto doezi anafika anachukua plate ya chakula anan'gan'gania kisha anaanza kulia eti hataki watoto wangu wale. Hapo mama ake yupo nje .
Jomba LIKUD,

Kama unaweka nyama kwa kuhesabu vipande, wewe kwako ni Uswahilini manake huko kwingine, wenzako wananunua nyama kilo 2 na kuwapa mbwa wale!!!

Karibu Uswahilini jombaa!!
 
Nilichogundua wewe ni (Mchumi ) Ila ungeweza hata kumjumulisha kwenye bajeti yako ya msosi lakini kwasababu huna bajeti naye,; Nikushauri weka uzio hata wa mabati chakavu funga kabisa ubakize mlango ambao utakuwa unaufunga mida ya msosi!

Pia zingatia Kama Watoto wako wanapenda kwa watu Basi na kwako watakuja wa watu, Zuia watoto wako kuzurula! Lakini mwisho wa siku Kero ni sehemu ya jamii! njia nyingine ya kuondoa kero ni kuivumilia.
 
Nilichogundua wewe ni (Mchumi ) Ila ungeweza hata kumjumulisha kwenye bajeti yako ya msosi lakini kwasababu huna bajeti naye,; Nikushauri weka uzio hata wa mabati chakavu funga kabisa ubakize mlango ambao utakuwa unaufunga mida ya msosi!

pia zingatia Kama Watoto wako wanapenda kwa watu Basi na kwako watakuja wa watu, Zuia watoto wako kuzurula!

Lakini mwisho wa siku Kero ni sehemu ya jamii! njia nyingine ya kuondoa kero Ni kuivumilia
Nope sio uchumi. Mimi sitaki watoto wangu wasumbuliwe. My family is a nuclear family. Nataka nikiwa nakula niwe nimekaa kwenye meza moja Mimi na watoto wangu damu yangu.. sitaki allien nyumbani kwangu.. wanawafundisha watoto wangu tabia mbaya na kuwakwaza.

Imagine toto linakuja linakuta watoto wangu wanakula halafu linashikilia plate linaanza kulia. That's amount to child abuse.
 
Hizo kesi ungewaachia mama zao mkuu.

Mambo ya vyakula wewe jitahidi tu usifatilie sana,Fuatilia yale Mambo Magumu Magumu ya kiume yale au vp bro!
Sina MKE bro Mimi ni msela. Hawa watoto kila mtu na mama Yao. Sipendi tu watoto wangu kufanyiwa kero. Toto linakuja na mikono yake michafu huko halijaogeshwa linanuka mikojo linakuja kusumbua watoto wangu.
 
Back
Top Bottom