Najiuliza tu, Rais Magufuli atafanyaje Kampeni 2020?!

Hivi 2020 ikifika, kile kipindi cha kampeni

Najiuliza tuu hivi mheshimiwa president atakapokuwa anaomba kura zetu atatumia aina gani ya maneno yatakayotushawishi tumpe kura?

Je atasema kuwa pakitokea njaa hatotoa chakula kwa vile serikali haina shamba?

Kwamba pakitokea maafa tusitegemee msaada toka serikalini, na hata watu wakichanga misaada itapelekwa kwenye mambo ya maendeleo

Kwamba atahakikusha wote wenye vyeti feki wanaondoka kwenye ajira japo yeye haangalii kama mtu anajua kusoma A ila anayechapa kazi?

Kuwa hatoongeza mishahara wala kupandisha madaraja mpaka uzalishaji uongezeke

Mengine naomba mnisaidie kuyaongezea....

Je hizo kauli atazitoa kweli?

Nani kakwambia President anawazia kugombea 2020?
Be smart kwani kwa anayofanya kwa mroho hata asingejaribu.
So relax sio sio wana-politics.
Thanks
 
Muongo huyu Mkuu atatumia uongo wake kuudanganya umma wa Watanzania na ipo misukule itamwamini kumbuka hizi kauli ambazo zote ni uongo mtupu! "Nilipoingia kilo ya sukari ilikuwa 5,000" "Bashite kakamata wenye madawa" na huu uongo wa mshahara, na misukule inaamini kwamba ni kweli tupu.

Hivi 2020 ikifika, kile kipindi cha kampeni

Najiuliza tuu hivi mheshimiwa president atakapokuwa anaomba kura zetu atatumia aina gani ya maneno yatakayotushawishi tumpe kura?

Je atasema kuwa pakitokea njaa hatotoa chakula kwa vile serikali haina shamba?

Kwamba pakitokea maafa tusitegemee msaada toka serikalini, na hata watu wakichanga misaada itapelekwa kwenye mambo ya maendeleo

Kwamba atahakikusha wote wenye vyeti feki wanaondoka kwenye ajira japo yeye haangalii kama mtu anajua kusoma A ila anayechapa kazi?

Kuwa hatoongeza mishahara wala kupandisha madaraja mpaka uzalishaji uongezeke

Mengine naomba mnisaidie kuyaongezea....

Je hizo kauli atazitoa kweli?
 
Atacheza Wimbo wa TMK, atapiga push up atakimbia, Atazindua mrad mmoja mmoja mara 3, Atasema sijawahi kwenda Ulaya toka niwe rahisi, elimu ni bure kweli kweli, then atapeta.N.B km la mkaa 100 halitajadiliwa other factors remain costant
 
Hivi 2020 ikifika, kile kipindi cha kampeni

Najiuliza tuu hivi mheshimiwa president atakapokuwa anaomba kura zetu atatumia aina gani ya maneno yatakayotushawishi tumpe kura?

Je atasema kuwa pakitokea njaa hatotoa chakula kwa vile serikali haina shamba?

Kwamba pakitokea maafa tusitegemee msaada toka serikalini, na hata watu wakichanga misaada itapelekwa kwenye mambo ya maendeleo

Kwamba atahakikusha wote wenye vyeti feki wanaondoka kwenye ajira japo yeye haangalii kama mtu anajua kusoma A ila anayechapa kazi?

Kuwa hatoongeza mishahara wala kupandisha madaraja mpaka uzalishaji uongezeke

Mengine naomba mnisaidie kuyaongezea....

Je hizo kauli atazitoa kweli?
Ataiba kura mkuu
 
Mleta mada angekua anajua watanzania ukisema neno mungu na ukalialia kidogo basi una kura 90%. Ndiyo gia atatumia. Lazika ashinde tena 2020 maana CDM walivyo na akili ya ovyo badala ya kumuweka Lissu agombee watamuweka Lowassa.
 
Hivi 2020 ikifika, kile kipindi cha kampeni

Najiuliza tuu hivi mheshimiwa president atakapokuwa anaomba kura zetu atatumia aina gani ya maneno yatakayotushawishi tumpe kura?

Je atasema kuwa pakitokea njaa hatotoa chakula kwa vile serikali haina shamba?

Kwamba pakitokea maafa tusitegemee msaada toka serikalini, na hata watu wakichanga misaada itapelekwa kwenye mambo ya maendeleo

Kwamba atahakikusha wote wenye vyeti feki wanaondoka kwenye ajira japo yeye haangalii kama mtu anajua kusoma A ila anayechapa kazi?

Kuwa hatoongeza mishahara wala kupandisha madaraja mpaka uzalishaji uongezeke

Mengine naomba mnisaidie kuyaongezea....

Je hizo kauli atazitoa kweli?
SWALI LA KIJINGA NA KILOFA SANA. KWANI 2015 ALIFANYAJE KAMPENI? RUBBISH
 
Mungu atupe uzima ili tushuhudie, Amina [emoji1431][emoji1431]
Ila bado tunasubiri utabiri wa mbuge wa Arachuga [emoji111]️[emoji111]️
 
Cccm wasivyo na aibu anaweza kuja akasema tena kuwa atapandisha mishahara na madaraja.....pia hapatokua na bomoabomoa
 
Hivi 2020 ikifika, kile kipindi cha kampeni

Najiuliza tuu hivi mheshimiwa president atakapokuwa anaomba kura zetu atatumia aina gani ya maneno yatakayotushawishi tumpe kura?

Je atasema kuwa pakitokea njaa hatotoa chakula kwa vile serikali haina shamba?

Kwamba pakitokea maafa tusitegemee msaada toka serikalini, na hata watu wakichanga misaada itapelekwa kwenye mambo ya maendeleo

Kwamba atahakikusha wote wenye vyeti feki wanaondoka kwenye ajira japo yeye haangalii kama mtu anajua kusoma A ila anayechapa kazi?

Kuwa hatoongeza mishahara wala kupandisha madaraja mpaka uzalishaji uongezeke

Mengine naomba mnisaidie kuyaongezea....

Je hizo kauli atazitoa kweli?

Kuna ma ccm mkuu hao Ndo adui zetu namba moja ktk nchi hii.wao hawafikirii chochote muda ukifika watavaa kijani na kulinda maslahi ya chama watasahau yote.
Wasio na akili ni mzigo kwa wenye akili.
 
2015 nilikuwa namhurumia sana jinsi alivyokuwa akipigwa na jua huku akipata shida sana kuwashawishi watz huku ccm yake ikiwa haiaminiki hata kidogo, ni wazi silaha iliyombeba ni jina lake tu, ambalo leo ukilitaja mbele za watu unashuhudia nyuso za watz zikikutizama kwa huzuni iliyochanganyika na kukata tamaa...

Nilipata shida sana kumtetea huku nikipata changamoto kubwa sana ya upinzani kutoka kwa vijana wenzangu waliodai ccm imeoza na haitokaa iweze kutuletea maendeleo, zaidi itatunyonya tu hadi mwisho wake...

Point yangu niliyoisimamia ni kwamba naamini katika magufuli si ccm, lakini bado nilishambuliwa kwamba urais ni taasisi na inaundwa kwa mfumo mkubwa ambao nao ni mchafu (ndani ya ccm), pia tuhuma zake pia nilitajiwa. Nilielewa lakini sikutaka kubadili msimamo na kusema nampa nafasi, akichemka basi sitomuamini yeyote atokaye ccm...

Nilifanikiwa kushawishi wanyonge kadhaa wakamchagua japo mimi sikupiga kura, ila leo hii wananilaumu sana. Magufuli alifanikiwa kuukwaa urais. Alishinda kihalali au NEC walifanya yao? Mimi sijui. Ila leo hii najuta sana kutumia energy yangu kubwa kumsapoti mtu ambaye leo hii anatuona kama mbuzi wake tu!

Mheshimiwa hata kama unapita huku, uone malalamiko ya raia wako. Ukiona wengi wanapiga kelele ujue kweli kuna tatizo, badilika ndugu yangu ubabe hausaidii. 2020 imekaribia utahangaika sana!

Kumbuka yaliyokukuta kwenye maeneo ya watu waliokuwa tayari wanajielewa kama Arusha, Tanga, Mbeya na Dar es Salaam, ulitaabika sana na kwenye sanduku uliona walichokufanyia. Bongo ya 2020 si kama ya 2015, wengi watakuwa tayari wanajielewa. Mimi yangu macho tu........

UmeongeA kwa hisia ndugu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom