Najiuliza tu, Rais Magufuli atafanyaje Kampeni 2020?!

Najiuliza tu, Rais Magufuli atafanyaje Kampeni 2020?!

Keshapita hana haja ya kampeni kuna makundi matatu upinzani( mambubmbu kabisa),ccm(mambumbumbu kdg)na kundi la tatu ni watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri hawa ndo watakao mpa nchi kwa awamu ya pili maana hawa ndo wana macho ya kujua lipi anafanya sahihi lipi anakosea bila kuingiza siasa na upuuzi wa wanasiasa na hapo tupo wengi..
 
Sioni watatokea wapi maana mchimba kisima kaingia mwenyewe.
 
Hivi 2020 ikifika, kile kipindi cha kampeni

Najiuliza tuu hivi mheshimiwa president atakapokuwa anaomba kura zetu atatumia aina gani ya maneno yatakayotushawishi tumpe kura?

Je atasema kuwa pakitokea njaa hatotoa chakula kwa vile serikali haina shamba?

Kwamba pakitokea maafa tusitegemee msaada toka serikalini, na hata watu wakichanga misaada itapelekwa kwenye mambo ya maendeleo

Kwamba atahakikusha wote wenye vyeti feki wanaondoka kwenye ajira japo yeye haangalii kama mtu anajua kusoma A ila anayechapa kazi?

Kuwa hatoongeza mishahara wala kupandisha madaraja mpaka uzalishaji uongezeke

Mengine naomba mnisaidie kuyaongezea....

Je hizo kauli atazitoa kweli?
atakuwa na kampeni ngumu sana, labda alazimishe ushindi kwa nguvu kama walivyozoea. kwasababu, yeye ameamini anapambana na watu wa mijini hasa wale wenye uwezo mzuri, wafanyakazi, wafanya biashara ili abaki na wapiga kura wa vijijini, matokeo yake wamjini walipokosa hela, wa vijijini hawatumiwi hata ya kununua mafuta ya taa, maisha vijijini ni magumu kuliko kabla na wakituuliza wa mjini tunawaambia magu kabana....wafanyakazi ndio kabisaaaa jana ametoa ujumbe wake kwao, wafanya biashara hakuna hata anayemtaka, sasa sijui nani anamhitaji tena 2020. hakuna rais aliyeumiza mioyo ya watz kama jamaa.
 
tumeondoa watumishi hewa, tumeyashughulikia mafisadi yaliyokuwa yanakura hera za serikali na yale yaliyokuwa yanatorosha madini hasa Tanzanite
 
Huwa trend iko hivi, ikifika mwaka 2019 ataanza kujibaraguza na kubadili staili na maneno yake pia yatajawa na asali.

Kwa mfano atasema (nasisitiza ni mfano) "....hali ya uchumi baada ya kuwathibiti wale wezi wa rasilimali zetu na kukusanya kodi nk nk .............Serikali yangu sasa ina uwezo mkubwa wa kujiendesha .......na sasa hali ya uzalishaji imeimarika....hali ya viwanda ni .............. kwa hiyo nimemuagiza Waziri ....apandishe mishahara yote kuanzia mwezi ujao......."

".......kwa wale wenye njaa Serikali yenu haiwezi kuwaangusha.....sasa hivi tunazo tani.....za chakula...... hizo sio za kulishia ng'ombe au punda .....hizo ni za kwenu......... zitasambazwa na vikosi......."

"....Sasa hivi zile milioni 50 kwa kila kijiji tumepeleka......kuna vijiji tayari tumeanza kulipa.......na vilivyobaki mgao utawafikia....sitawaangusha..." Ataserebuka kidogo na ngoma za akina mama......kisha atapiga kilugha .....halafu atawachamba watani zake(?)........

"...Mnaona ndugu zangu jinsi nilivyowatumikia......naombeni kura zenu, sitawaangusha jamani.....(ataongea kilugha weee) ........na kukamilisha ......sitawaangusha jamani...na ...."
 
Atafanya na magari ya maji ya kuwasha, fanya fujo uchapwe, makarani watakuwa wajeda, marufuku kwenda kwenye kampeni za vyama pinzani mnahatarisha amani,Wapinzani ni wachochezi watawekwa under house arrest.nk nk
Atafanya kirwandarwa
 
atakuwa na kampeni ngumu sana, labda alazimishe ushindi kwa nguvu kama walivyozoea. kwasababu, yeye ameamini anapambana na watu wa mijini hasa wale wenye uwezo mzuri, wafanyakazi, wafanya biashara ili abaki na wapiga kura wa vijijini, matokeo yake wamjini walipokosa hela, wa vijijini hawatumiwi hata ya kununua mafuta ya taa, maisha vijijini ni magumu kuliko kabla na wakituuliza wa mjini tunawaambia magu kabana....wafanyakazi ndio kabisaaaa jana ametoa ujumbe wake kwao, wafanya biashara hakuna hata anayemtaka, sasa sijui nani anamhitaji tena 2020. hakuna rais aliyeumiza mioyo ya watz kama jamaa.


Point sana kaka
 
Atasema yeye ni raisi wa "wanyonge" na atawapandishia mshahara wafanyakazi.
Ataleta wawekezaji.

Ataongeza Bombardier!

Atajenga hostel!

Atapambana na rushwa ndogo kama zile za madiwani Arusha!

Atapambana na walevi kama wale wakurugenzi wanne !

Atahakikisha Taa za barabarani zinakuwa mikoani hata kama punda ndio wanapita
 
Nimekuwa discouraged sana na kazi ila sina ujanja maana siwezi kushindana naye aniongeze mshahara. Sijui kama wenzangu mna machungu kama mimi.
 
Eeh! Kwani ile hoja ya miaka 7 si ndiyo tunategemea ipite. So hapo kwenye heading badilisha weka 2022
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom