ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 25,009
- 61,260
Mosi, nashindwa kufikiri sawasawa. Mungu mwenye upendo aumbe binadamu mfano mtoto huko Sudan kwenye vita amezaliwa kwenye vita kisha katika maisha yake anakutana na janga la njaa halafu baadae anakuja kufa akiwa na malaria. Kwanini Mungu aruhusu mazingira ya namna hii?
Pili, mtu anazaliwa kwenye umaskini kisha anatenda dhambi kwa ajili ya umaskini wake. Mwisho akachomwe moto. Mungu angetuumba bila umaskini na shida kisha akatuacha tufikiri na tuenende katika mawazo yetu wenyewe ili ukifanya dhambi uwe umejitakia mwenyewe. Kama ni kweli kuwa shetani ndo chanzo cha vifo na dhambi basi atakuwa anatutengenezea mazingira ya dhambi ili tukifanya tu anatusababishia kifo tukachomwe naye moto moja kwa moja.
Tatu napenda kujua hili suala. Tunaamini kwamba hapo nyuma kabla ya ukoloni dini hazikuwepo Africa sasa ina maana wale mababu zetu waliofuata imani za miungu yao kutokana tu na tamaduni walizokuta je wenyewe watahukumiwa kivipi maana wao ndo wako wengi kuliko tulio hai sasa hivi. Kwa lugha nyepesi ni kwamba nauliza wale ambao hawakupata neema ya kusikia habari za Mungu kama sisi dini zimesema watahukumiwaje?