Najitolea bure kufanya matibabu kwa watu watakaokuwa tayari

Daktari wa Meno

JF-Expert Member
Sep 5, 2019
509
1,610
Baada ya kusoma juu ya utabibu kwenye mtandao wa YouTube kwa sasa nimeiva na ninataka kufanya majaribio ya kile nilichosoma kwa miaka zaidi ya 5 huko mtandaoni. Nilisoma kuhusu kufanya operesheni na kutibu magonjwa mbalimbali kupitia video za mtandaoni.

Japo napungukiwa na uhaba wa vitendea kazi kama visu, nyuzi za kushonea, mikasi mikubwa, gloves, nyembe na vitanda vya kufanyia upasuaji ila naamini nitaweza kufanya huduma nzuri kadri nilivyosoma.

Naomba ushirikiano wako kama mdau na kama unahitaji kufanyiwa operesheni naweza kujaribu kufanya nione kama nitakuwa na mafanikio makubwa.

Karibuni wadau
 
Baada ya kusoma juu ya utabibu kwenye mtandao wa YouTube kwa sasa nimeiva na ninataka kufanya majaribio ya kile nilichosoma kwa miaka zaidi ya 5 huko mtandaoni. Nilisoma kuhusu kufanya operesheni na kutibu magonjwa mbalimbali kupitia video za mtandaoni. Japo napungukiwa na uhaba wa vitendea kazi kama visu, nyuzi za kushonea, mikasi mikubwa, gloves, nyembe na vitanda vya kufanyia upasuaji ila naamini nitaweza kufanya huduma nzuri kadri nilivyosoma.
Naomba ushirikiano wako kama mdau na kama unahitaji kufanyiwa operesheni naweza kujaribu kufanya nione kama nitakuwa na mafanikio makubwa.
Karibuni wadau
 
Sisi kabila letu;

Mtu akisema ameshajua kufanya tohara basi inampasa aanze kuwafanyia watoto wake mwenyewe kwa ufanisi ili watu wakuamini. Ukikosea umewaharibu wanao mwenyewe. Hivyo na wewe kafanye majaribio kwa nduguzo kama huna watoto.

Kwenye mwili wa binadamu hakuna majaribio. Ndiyo maana madaktari wenzako wakitaka kuanzisha tiba, basi majaribio yake hufanywa kwa wanyama. Hii ni kwa sababu hakuna majaribio kwenye mwili wa binadamu.
 
Asilimia kubwa mnaonekana kunivunja moyo ila naamini nitafikia malengo yangu na kuwa mbobezi wa upasuaji.
Hapana Mkuu, hujakatishwa tamaa.

Kila kitu kina gharama yake. Ndiyo maana wenzako wanasoma darasani kwa miaka mitano au mitatu kwa ngazi ya diploma ili waweze kupata hadhi ya kuwa madaktari. Hii inaambatana na mafunzo kwa vitendo na siyo kwenye video za YouTube.

Nenda darasani kasome uhalalishwe. Kwa kuwa umeshasoma sana, utapasua na itakuwa rahisi kwako.
 
Sisi kabila letu;

Mtu akisema ameshajua kufanya tohara basi inampasa aanze kuwafanyia watoto wake mwenyewe kwa ufanisi ili watu wakuamini. Ukikosea umewaharibu wanao mwenyewe. Hivyo na wewe kafanye majaribio kwa nduguzo kama huna watoto.

Kwenye mwili wa binadamu hakuna majaribio. Ndiyo maana madaktari wenzako wakitaka kuanzisha tiba, basi majaribio yake hufanywa kwa wanyama. Hii ni kwa sababu hakuna majaribio kwenye mwili wa binadamu.
Sijajua ni aina gani za wanyama wa kufanyia majaribio mdau pia ni ngumu mtu kunipa mnyama wake nimfanyie majaribio kwa jinsi navyojua watu na tabia zao.
 
Na vile humu hatujuani unakuta wewe ndo ndugu yake
Hhhhh
Labda huyu anayesoma udaktari mtandaoni bila vitendo sidhani kama nina ndg mwenye akili hizi.
Akaanze na panya, kuna wale panya wanafugwa iringa wanaitwa simbils nasikiaga ndio huwa wanaanzia madaktari wa fani ya upasuaji
 
Back
Top Bottom