Ninahitaji watu wenye idea na video production watakaokuwa tayari kujitolea kufanya project free ila kwa malengo

Idrisajr

Member
Jan 15, 2018
7
7
Nadhani kwa wale wenye idea na mambo ya movie making wanaelewa ila lengo la kuanzisha hii thread ni kukutanisha watu wenye mawazo tofauti ya idea moja.

Na sio mawazo tu hata nyenzo(vitendea kazi) naamini tupo vijana wengi ambao tuna idea ila jinsi ya kuzifikisha kuna vitu vinatukwamisha kama mitaji ya kufanya hivyo vitu hivyo ukiwa na idea yoyote inayozunguka hii thread itakuw vizuri ukichangia au ukiwa mmoja wetu.

Ukiwa na uelewa wa hivi vitu utatufaa pia mtunzi wa stori, location manager, camera man, vfx &matte painter, sound designer na mtu mwenye idea na program zifuatazo pia atahitajika AE, PP, PS, nuke, fusion na zozote ambazo zinahusika na hizi mambo.

(IKUMBUKWE-tunahitaji watu ambao watajitoa sababu hakuna ambae atalipwa kupitia hili malipo yetu ni kufanya kitu kizuri ili kije kutulipa baadae nmeandika hii sababu hata mm nina idea za hii kitu ila sina mtaji wa kufanya peke yangu lakini naamini tukiwa wengi tunaouwezo wa kulifanikisha hili jambo) ukiwa interested just nicheki 0684842325
 
Tuanze kwanza na wewe. Umesema una idea, vitendea kazi gani unavyo?
Ninavyo ila havijakamilika kufanya kitu kinachoeleweka bado maana nina camera, pc ambayo inauwezo kiasi chake na ninaijua vizuri Premiere pro hivyo ndio nilivyo navyo mm ndugu najua sio vingi ndio maan nikaandika hii post.
 
Hivi kwa mfano movie production za Bongo wanazingatia haya yote na wana wataalam? Mbona kazi zao ni za kiwango cha chini mno? Mimi sina ujuzi wowote lakini nikiamua kwa mfano kutengeneza documentary naweza kufanya vizuri kuliko kazi nyingi zilizo sokoni.
 
Mkuu hizo ni genre mbili tofauti, ofcourse documentary inategemea zaidi na unachoongelea na washiriki husika, documentary ni factual movies una wigo mpana just creativity yako sky is the limit.

Kazi nyingi zilizo sokoni zinapikwa haraka haraka na kupakuliwa (investment ya time na pesa haipo) swali linakuja, unaweza ukapika na kupakua haraka haraka kama wao na kutoa kitu mujarabu?
 
Hivi kwa mfano movie production za Bongo wanazingatia haya yote na wana wataalam? Mbona kazi zao ni za kiwango cha chini mno? Mimi sina ujuzi wowote lakini nikiamua kwa mfano kutengeneza documentary naweza kufanya vizuri kuliko kazi nyingi zilizo sokoni.
Ongera kwa kuwa na huo ujuzi ila kinachowashinda ma director wa bongo ni kuwekeza mda na pesa sbb kazi ya vfx na cgi inakula mda na pia mfanyaji anahitaj mpunga uliochangamka hata hivyo tunajaribu tu ila kiukwel bado hata hatuja karibia
 
Mkuu una camera aina gani na una idea gani? Kama una camera kubwa nzuri huo ndo mtaji mama, ebu njoo PM tunaweza kufanya jambo.
 
Mkuu hizo ni genre mbili tofauti, ofcourse documentary inategemea zaidi na unachoongelea na washiriki husika, documentary ni factual movies una wigo mpana just creativity yako sky is the limit.

Kazi nyingi zilizo sokoni zinapikwa haraka haraka na kupakuliwa (investment ya time na pesa haipo) swali linakuja.., unaweza ukapika na kupakua haraka haraka kama wao na kutoa kitu mujarabu?
Naona hujaelewa nilichozungumzia. Mimi nazungumzia vitu kama quality ya picha, sauti etc... technical side. Unapotengeneza documentary na movie quality ya hivyo vitu ni ile ile. Sijazungumzia ule uigizaji na waigizaji, nyanja ambayo ni hovyo mno kwa Tanzania. Unakuta mtu anasema ana-act comedy ukiangalia alicho-act unakasirika nusu ya kuvunja TV badala ya kucheka.
 
Hivi kwa mfano movie production za Bongo wanazingatia haya yote na wana wataalam? Mbona kazi zao ni za kiwango cha chini mno? Mimi sina ujuzi wowote lakini nikiamua kwa mfano kutengeneza documentary naweza kufanya vizuri kuliko kazi nyingi zilizo sokoni.
If you can imagine it, it doesn't mean you can make it. If you can render it, it does not mean you can invent it.

Kuabadilisha story kuwa script, na kuiibadilisha script kuwa movie ni jambo linalohitaji utaalam sana, nahisi director inabdi awe vizuri sana maana kuna wakati hata waigizaji wanakuwa hawajui mwisho wa wanachocheza. Kuna muda hata waigizaji wenyewe wanahisi wanacheza mvoie ya kilofa.

Mfano Pirates of the carribeans dead men tell no tales yule bidada alikuwa anaona anaigiza mvoie ya kifara kiasi kwamba alikuwa anaona aibu hata kuwambia rafiki zake kuwa kashiriki, ila alipokuja kuiona movie yenyewe alishangaa sana.

Terminator ile ya kwanza ya anorld, alidiriki kusema anaigiza movie ya kiboya ambayo itafail kwasababu alikuwa anaona ile script ya kidwanzi, ila director James Cameroon yeye alijua mwisho wa final product utakwuaje.
 
If you can imagine it, it doesn't mean you can make it. If you can render it, it does not mean you can invent it.

Kuabadilisha story kuwa script, na kuiibadilisha script kuwa movie ni jambo linalohitaji utaalam sana, nahisi director inabdi awe vizuri sana maana kuna wakati hata waigizaji wanakuwa hawajui mwisho wa wanachocheza. Kuna muda hata waigizaji wenyewe wanahisi wanacheza mvoie ya kilofa. Mfano Pirates of the carribeans dead men tell no tales yule bidada alikuwa anaona anaigiza mvoie ya kifara kiasi kwamba alikuwa anaona aibu hata kuwambia rafiki zake kuwa kashiriki, ila alipokuja kuiona movie yenyewe alishangaa sana.
Terminator ile ya kwanza ya anorld, alidiriki kusema anaigiza movie ya kiboya ambayo itafail kwasababu alikuwa anaona ile script ya kidwanzi, ila director James Cameroon yeye alijua mwisho wa final product utakwuaje.
Haya. Mdandia treni kwa mbele mwingine huyu. Hajajua nilichozungumzia anajibu. I am talking about technical side! Vifaa vinavyotumika na ujuzi wa kuvitumia. Nazungumzia vitu kama mambo ya lighting, sound etc. Haya unayoleta ya mambo ya uigizaji na waigizaji pia ma-directors sijui kwa Bongo kiwango chake kiko chini mno mno. Zaidi naweza kusema kuwa maelezo mengine uliyotoa yanaakisi ile ile hulka za ki-bongo bongo. Mtu anaelezea kitu ambacho hajaulizwa kwa sababu tu alikikariri ili aonekane bonge la mjanja.
 
Shida siyo vifaa shida ni kujua kutumia vifaa vyenyewe. Kuna movie moja imeshootiwa kwa iPhone 5s na ni movie ya mbele lakini quality yake huwezi kuiringanisha na movie zetu hata kidogo. Kuwa na vifaa high end bila uwezo haviwezi kukusaidia. Na muda mwingine kuna technology zinakuwa invented wakati wakitatua changamoto ya kushoot movie.
Naona unajisifu, nikuulize ushawahi kutengeneza documentary au unafikiria kuwa unaweza kutengeneza documentary nzuri tu?
 
Yeh. Vifaa ofcourse bila kujua kuvitumia ni kazi bure wala sikatai. Ndipo hapo hoja yangu ilipo haswa na mwanzisha thread alikuwa na nia ya kukutanisha wenye ujuzi na wenye vifaa au walio na vyote. Kutengeneza documentary nzuri ni kazi kubwa na ni ya kitaalam. Mimi nilijigamba kwa kujilinganisha na hizi Bongo movie nikasema pamoja na ukilaza wangu lakini naweza kuja na kitu kizuri zaidi.
 
Dada yangu anafanya kazi TBC anasema wao wana vifaa vingi na vizuri ila sasa tazama quality ya vipindi vyao na channel ya juzijuzi tu hapa ya Wasafi
 
sio vipindi vyote huandaliwa na tv husika
Hilo suala nalijua. Tunataka ulinganishe kipindi gani cha TBC 1 chenye quality ya picha na sauti kuliko Wasafi TV au Clouds TV? Linganisha hata vipindi vilivyofanyika mazingira ya kawaida kama 5 Gear vinafanyika gereji ila quality nzuri, tazama Tunatekeleza wakienda hata kwenye kituo cha kufua umeme low quality.

Linganisha sauti ya TBC Taifa na sauti ya vituo kama EFM utajua namaanisha nini.
 
Yeh. Vifaa ofcourse bila kujua kuvitumia ni kazi bure wala sikatai. Ndipo hapo hoja yangu ilipo haswa na mwanzisha thread alikuwa na nia ya kukutanisha wenye ujuzi na wenye vifaa au walio na vyote. Kutengeneza documentary nzuri ni kazi kubwa na ni ya kitaalam. Mimi nilijigamba kwa kujilinganisha na hizi Bongo movie nikasema pamoja na ukilaza wangu lakini naweza kuja na kitu kizuri zaidi.
kumbe unaweza kwa kuongea sasa kama kwa kuongea na kwakuimagine Mimi naweza kupigana na Antony Joshua na nikampiga.

usiwe keyboard warrior.
 
Back
Top Bottom