Najikuta nina stress kupindukia

Najikuta nina stress kupindukia

cutelove

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2017
Posts
3,586
Reaction score
8,386
Siku za hivi karibuni najiona ovyo, sina amani ndani ya moyo, muda mwingine najiuliza kwanini nilizaliwa hapa duniani.

Kuna muda machozi yananitoka ndo najihisi angalau mtu.

Nimekuwa mnyonge, hata kazini huwa akili yangu haipo serious, muda mwingine najihisi kuondoa uhai wangu.

Nimekuwa na hasira, muda mwingine huwa natumia lugha mbaya kwa wanaume wanao ni-aproach.

Naombeni ushauri tafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app

TAFADHALI cutelove SOMA HAPA
Sonona (Depression): Jinsi ya kupambana nayo na kumsaidia mwathirika


Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako
 
Time heals all wounds

Waliosema huo usemi hawajakosea..
Mimi nimewahi pitia hiyo leo ukiniambia nikwambie kilichokuwa kinanisumbua hata sikikumbuki, imagine that.

Itapita miaka utasahau hata nini kilikuwa kinakupa stress.

Shida zingine tunapitia ili tuweze kuthamini hata kidogo tunachokipata.

Huwezi thamini kuwa na TV kama kila siku unayo, au kulala nyumba haivuji kama hujawahi ona watu wamehama nyumba mvua ikinyesha.
 
Hata sijui nini tatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
Doh, ina maana unskosa amani pasi na kuwepo na chanzo chochote cha moja kwa moja?

Hapo ni shida sasa.

Ila unaposhikwa na hisia za kuchoka maisha ni lazima kuna kitu kibaya au cha kuumiza unachodhani utakiepuka wewe ukiondoka, ni kipi hicho? Kuanzia hapo watu wanaweza kupata pa kuanzia.
 
Mimi naona ndo utu uzima wenyewe.
Baadhi ya siku unaona mambo poa tu, some days unajiona loser hakuna cha maana kwenye maisha. Mm nishazoea when I feel worthless nasikiliza music nameza sleeping pills nalala. When i feel good na enjoy maisha. It's life it has ups and downs you just have to handle both situations with class otherwise utakua kituko duniani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom