Naitangaza harusi

Barubaru

JF-Expert Member
Apr 6, 2009
7,161
2,323
Amani iwe juu yenu.

Nimepokea simu kutoka kwa aliyekuwa member wa barza hii Bw Hossam Mohammed Hafif Al Miskry ( HM Hafif) ambaye kitaaluma ni Civil Engineer wa Kalafiy Construction ya Saud Arabia kuwa panapo majaaliwa taarih 8 July 2011 ataozesha mtoto wake Hajjat Dr Rufeeda Hossam Mohd Al Maskry kwa Engineer Fareed Fahad Abdullah Al Walad .

Harusi hiyo itafungwa Huko Zanzibar katika msikiti mkuu wa Malindi baada ya Swalat al Jumaa na baadae Chakula cha mchana Serena Hotel Zanzibar.

Bwana na Bibi harusi wote wanaishi na kufanya kazi Muscat Oman. Mama Daktari hospitali kuu ya Jeshi Oman na baba ni Mhandisi wa kampuni ya mafuta Oman (PDO)

Amewaomba woooote nduge zake muhudhurie bila kukosa. Hata mimi InshAllah nitakuja na mke wangu.

Shime alaykum, karibuni kwani sherehe ni watu na watu ndio nyie.

Nitatoa ufafanuzi zaidi mara atakapo nijulisha.
 
kila la kheri kwa hao maharusi watarajiwa!


Ila wana majina magumu hao!

Ni majina ya kiarabu na mimi labda nimeaandika kwa yanavyotamkika kwa kiarabu.

Lakini kwa Kiswahili ni Dr RUFIDA na Bw Harusi mtarajiwa ni Fahadi.
 
Kweli sherehe ni watu na watu ndio sisi! Safi sana na hongera kwa maharusi hao.
 
Unajuwa JF ina members wangapi? ila ninachofahamu mimi Hm Haffif ni wewe mwenyewe,........... very interesting!
 
Hahahaaa, Dr., hiyo Frida huwa inatamkwa Frida na siyo Firida.

Umenikumbusha kuna picha niliona imechorwa na mtoto kwenye picha kuna TV na mtoto kaandika SKIRINI (Screen). Mwingine alikuwa na kigugumizi na akawa anajitahidi kurudia neno alilosikia na alisikika akisema "fu.... fu..... fu...... fulashi" (flash).

Nifikishie hongera kwa ndugu, jamaa na marafiki na niwatakie sherehe njema . Salimia familia na mpe Seif hi.
Ni majina ya kiarabu na mimi labda nimeaandika kwa yanavyotamkika kwa kiarabu.

Lakini kwa Kiswahili ni Dr RIFIDA na Bw Harusi mtarajiwa ni Fahadi.
 
Dr.Manyaunyau naona umeweka picha yako kwene avatar..Haidhuru sana tutakaribia kusherehesha shughli insh'allah mradi tu kuombeana uhai.
 
Hongera sana HM Haffif kwa kuozesha...
Kila la heri kwa maharusi.
 
Dr.Manyaunyau naona umeweka picha yako kwene avatar..Haidhuru sana tutakaribia kusherehesha shughli insh'allah mradi tu kuombeana uhai.

Siku nyingi ahali yangu Labda nikupe picha yangu kamili na vazi langu la kila siku kazini. Nakukaribisha sana na nitakutafuta Ijumaa tano nitakapo fika dar es salaam
 

Attachments

  • Hamza.jpg
    Hamza.jpg
    9.7 KB · Views: 25
Unajuwa JF ina members wangapi? ila ninachofahamu mimi Hm Haffif ni wewe mwenyewe,........... very interesting!
karibu sana kwenye harusi ili uweze kuhakikisha hayo uyanenayo. karib bila kukosa
 
Back
Top Bottom