Kile kipindi cha chuo nimetoka zangu likizo nipo kwa mjomba huku nyanda za juu kusini.
Kwa ancle hapo kulikuwa na wapangaji wawili wamama wa makamo,wana mtoto mmoja mmoja.
Kakuwa maji yalikuwa ya shida mtaani,ancle alijenga tank kubwa maji yakitoka anatunza halafu anauza kipindi maji hayatoki. Alikuwa anajua kucheza na meter za kizamani maji yalikuwa yanatoka usiku tu,lakini bill ya mwezi inakuja elf3😀
Kukawa kuna binti mmoja mrembo akawa anakuja mara kwa mara kuteka maji pale,mpaka akanifanya niwe nashinda bombani namsubiria. Akawa kazoeana sana na mama mmoja mpangaji. Nikaona isiwe case,nikampanga yule mama aniungishe kwa mtoto,kwa mbwembwe zote jirani akasema hatachomoa!
Siku zinapita namuulizia,vipi mtoto? Anasema alikuja mchana[muda ambao mimi sipo] anakuwa ananilaumu mimi kutokuwepo. Wekeend moja nikaamua kutokutoka ili nipate kuongea na mrembo,mama akasema kampanga jioni saa kumi na moja tukutane maeneo.. Nikajiandaa vocal fresh,saa kumi na moja simu ikapigwa njoo sehemu fulani- nilienda nikamkuta mama mtu jirani,mtoto mkali hayupo; "yuko wapi sasa?",mama mtu anasema tusubiri kidogo anakuja! Subiri subiri,mpaka giza linaingia hakuna mtu! Baadaye yule mama anasema "unajua vibinti visumbufu sana,achana naye huyu atakusumbua!,kwani mimi vipi"?
Kwakweli nlichoka! Yule mama hakuwahi kuongea na binti wala nini. Ilikuwa giza giza linaingia ikabidi nizuge kuwa wewe rudi nyumbani kwanza tutayajenga siku ingine. Nlipaisha😀😀
Lakini shangazi namimi naomba nionje😊