Serikali haraka fungeni mipaka chakula kisiuzwe nje, machafuko na migogoro ya kivita viwape ari hiyo

Arovera

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
11,233
29,452
Wakuu,

Dunia ya leo ni migogoro na vita sehemu mbalimbali, hivo wakati huu wa mavuno mazao kama mchele, mahindi, maharagwe na nafaka nyingine haraka sana yazuiwe maana sio muda tutaanza kulia njaa.

Nchi nyingi kwa sasa wamefunga mipaka yao hakuna chakula kutoka kwani usalama na utulivu wa kwanza kwa mwananchi ni chakula.
 
Wakuu
Dunia ya leo ni migogoro na vita sehemu mbalimbali, hivo wakati huu wa mavuno mazao kama mchele, mahindi, maharagwe na nafaka nyingine haraka sana yazuiwe maana sio muda tutaanza kulia njaa,
Nchi nyingi Kwa sasa wamefunga mipaka yao hakuna chakula kutoka kwani usalama na utulivu wa kwanza Kwa mwananchi ni chakula,
Kalime kama umahofia njaa. Yaani mkulima aache kuuza sehemu yenye bei nzuri kwa sababu ya njaa? Nitakubalina na wewe kama utasema mishahara ya wafanyakazi nayo ikatwe kidogo ili kuilinda serikali na matumizi. Pia kodi za biashara ziongezwe kidogo ili kuongeza akiba ya serikali
 
utomaso huu
 
Tzn hakuna shida ya chakula,Huwa tunaagiza vyakula vya chapati ngano ambayo sio lazima.

Huu ni wakati wa kuuza chakula sio Kuzuia.

Mwisho shida inaweza kuwa kwenye Mafuta na sio vinginevyo
 
Kalime kama umahofia njaa. Yaani mkulima aache kuuza sehemu yenye bei nzuri kwa sababu ya njaa? Nitakubalina na wewe kama utasema mishahara ya wafanyakazi nayo ikatwe kidogo ili kuilinda serikali na matumizi. Pia kodi za biashara ziongezwe kidogo ili kuongeza akiba ya serikali
Unachoongea hukijui!! Anayeuza nje ya nchi sio mkulima ni mfanyabihashara. Wakulima wanaouza gunia elfu 30 leo ndo watakuja kununua debe elfu 30 mwezi wa 10
 
Wakuu
Dunia ya leo ni migogoro na vita sehemu mbalimbali, hivo wakati huu wa mavuno mazao kama mchele, mahindi, maharagwe na nafaka nyingine haraka sana yazuiwe maana sio muda tutaanza kulia njaa,
Nchi nyingi Kwa sasa wamefunga mipaka yao hakuna chakula kutoka kwani usalama na utulivu wa kwanza Kwa mwananchi ni chakula,
Hayo maghala ya kuhifadhi chakula yameshajaa, utakiweka wapi? Halafu kilimo ni biashara, mtu kalima kwa gharama zake, hiwezi kumpangia mahali na muda wa kuuza wakati anadaiwa Benki. serikali ianze kulima wenyewe ndio wajipangia pa kuuzza.
 
Kalime kama umahofia njaa. Yaani mkulima aache kuuza sehemu yenye bei nzuri kwa sababu ya njaa? Nitakubalina na wewe kama utasema mishahara ya wafanyakazi nayo ikatwe kidogo ili kuilinda serikali na matumizi. Pia kodi za biashara ziongezwe kidogo ili kuongeza akiba ya serikali
Hawa watu hawajawahi kumhurumia kabisa mkulima
 
Wakuu
Dunia ya leo ni migogoro na vita sehemu mbalimbali, hivo wakati huu wa mavuno mazao kama mchele, mahindi, maharagwe na nafaka nyingine haraka sana yazuiwe maana sio muda tutaanza kulia njaa,
Nchi nyingi Kwa sasa wamefunga mipaka yao hakuna chakula kutoka kwani usalama na utulivu wa kwanza Kwa mwananchi ni chakula,
Mwaka huu chakula kingi mnoo kinaweza kulisha nchi 5
 
Unachoongea hukijui!! Anayeuza nje ya nchi sio mkulima ni mfanyabihashara. Wakulima wanaouza gunia elfu 30 leo ndo watakuja kununua debe elfu 30 mwezi wa 10
Na wewe unachoongea hukijui. Huyo mfanyabiashara anayeuza nje anafanya mazao yawe yana uhitaji mkubwa na unajua demand ikiwa kubwa na bei inapanda.
Sasa mipaka ikifungwa wahitaji sio wengi hivyo chakula kinashuka bei.

Mfano ulioutoa gunia la elfu 30 mkulima atakuja kununua debe elfu 30.

Nikuambie,mmulima naye ana matatizo yake mengi tu yanayohitaji fedha. Ikiwa mazao yatakosa soko kwa vyovyote vile atauza hayo mazao bila kujali ni kwa bei ndogo kiasi gani.
Mfano serikali imefunga mipaka na imetokea mazao ni mengi kwa mfano mahindi,unakuta mipaka ikifungwa debe 1 linauzwa 5,000/= hadi 8,000/= na mkulima anashida ya 100,000/= itabidi auze madebe mengi ya mahindi ili kuipata laki 1 na hivyo kumletea njaa mlangoni tofauti na mipaka ingekuwa wazi mkulima angeuza kiasi kidogo cha mahindi ili kuipata laki 1 maana mipaka ikiwa wazi debe 1 linaweza kuanzia 15,000/= hadi 25,000/=

Sasa wewe elezea mipaka ikifungwa inavyoweza kuzuia njaa kwa mkulima.
 
Kwa kiasi kikubwa nakubalina na wewe. Lakini huoni kwamba ukiwanyima hao wafanyabiashara kuuza nje, bei ya mkulima itaporomoka zaidi? The higher the demand, the higher the price. Ukikataza wafanyabiashara kuuza nje, mahindi yatakuwa mengi na yatadodea wakulima ambao itabidi wauze bei ya chini zaidi. BTW hata hili la wafanyabiashara kufaidika na uuzaji nje ya nchi nalo ni tatizo serikali. Tungekuwa na serikali inayojali wakulima ingewasaidia kwenye kuuza mazao yao nje, na hii angalao inge-justify katazo la uuzaji wa chakula nje ya nchi panapokuwa na tishio la upungufu wa chakula.
 
Na wewe unachoongea hukijui. Huyo mfanyabiashara anayeuza nje anafanya mazao yawe yana uhitaji mkubwa na unajua demand ikiwa kubwa na bei inapanda.
Sasa mipaka ikifungwa wahitaji sio wengi hivyo chakula kinashuka bei.

Mfano ulioutoa gunia la elfu 30 mkulima atakuja kununua debe elfu 30.

Nikuambie,mmulima naye ana matatizo yake mengi tu yanayohitaji fedha. Ikiwa mazao yatakosa soko kwa vyovyote vile atauza hayo mazao bila kujali ni kwa bei ndogo kiasi gani.
Mfano serikali imefunga mipaka na imetokea mazao ni mengi kwa mfano mahindi,unakuta mipaka ikifungwa debe 1 linauzwa 5,000/= hadi 8,000/= na mkulima anashida ya 100,000/= itabidi auze madebe mengi ya mahindi ili kuipata laki 1 na hivyo kumletea njaa mlangoni tofauti na mipaka ingekuwa wazi mkulima angeuza kiasi kidogo cha mahindi ili kuipata laki 1 maana mipaka ikiwa wazi debe 1 linaweza kuanzia 15,000/= hadi 25,000/=

Sasa wewe elezea mipaka ikifungwa inavyoweza kuzuia njaa kwa mkulima.
Uko sahihi kabisa. Njia nzuri ya serikali kuweka ''katazo'' ni serikali kununua hayo mahindi kwa bei ile ile wanayouzia nje ya nchi au zaidi. Wakifanya hivyo, hakutakuwa tena na umuhimu wa kuweka katazo kwani wakulima watakilimbilia kuiuzia serikali.
 
Serikali ikishanunua itayaweka wapi? Au turudishe mambo ya serikali kufanya biashara? Mliona JPM alichowafanya wakulima wa korosho?

Tanzania hakuna vita, mazao yauzwe nje, anaehisi njaa nyumbani kwake akalime mashambani
 
Back
Top Bottom