Naipenda DAR,my City

dar ntakuja kupata mahitaji kama ambavyo naweza kwenda moshi, arusha, na hata kagera lakn yawezekana ni sababu ya kutotembea miji mbalimbali ukauona utofauti ndio maana unaiyona dar ni mbingu ndogo

Majiji ya Tz, sijafika Tanga tu, na nimekaa mikoa 5 ya bara na kutembea angalau kukaa kwa siku 3 au 4 hivi mikoa 4 ya Tz bara. 9 ya Tz bara. Mwanza nimeipenda, na pia Kahama nilipapenda ila siziweki mbele ya Dar!
 
Kama ni mkazi wa Dar naomba utuweke na mtaa unaoishi na nyumba unayoishi kwa nje!!!
 
huko sina picha zake.....nimeweka picha zinazonifanya niipende dar....

umeona eeh... kupenda kitu ni relative term unapenda kulingana na kile unachoona, au unachokijua. umenikumbusha hekaya ya vipofu saba waliopapasa tembo alieuawa. Alieshika sikio akasema 'ah kumbe yuko kama ungo!' aliegusa mguu akasema 'ah kumbe yuko kama mti!' laiti wangechukua hatua zaidi ya kumpapasa kila mahali wangalifahamu tembo angalau anafananaje. Umegusa posta na kariakoo... papasa dar yote uijue vema mkuu... kama kuna picha zilizokufanya uipende Dar ukiona picha nyingine zitakufanya uichukie.
 

kazi kweli kweli......naijua DAR kuliko unavyofikiri. hivi msichoelewa nini? naipenda dar ndio my city. thats it...
 
jamani nimesema naipenda DAR. my city sasa sioni sababu ya watu kuchukulia too personal na kuanza kuniuliza naishi sehemu gani dar. mwingine anataka nimuwekee picha ya ninapoishi! hata nikiwa naishi jangwani pale bondeni nitaendelea kupenda DAR my city
 
Nimekuelewa - kupenda ni subjective i.e. the beauty is in the eye of beholder!
 
Kama ni mkazi wa Dar naomba utuweke na mtaa unaoishi na nyumba unayoishi kwa nje!!!

hahahaa! Umeua mkuu!. Ni rahisi kukuwekea picha zilizopigwa maeneo ya posta na osterbay lakn kamera haitoi picha za nyumban anapoishi
 
hahahaa! Umeua mkuu!. Ni rahisi kukuwekea picha zilizopigwa maeneo ya posta na osterbay lakn kamera haitoi picha za nyumban anapoishi

hivi wewe na akili yako timamu unaweza kuweka nyumba yako unapoishi humu? thread hii sio kuhusu mimi ninapoishi hebu acha utoto hapa tunajadili uzuri wa DAR CITY na ndio maana naipenda dar
 
hahahaa! Umeua mkuu!. Ni rahisi kukuwekea picha zilizopigwa maeneo ya posta na osterbay lakn kamera haitoi picha za nyumban anapoishi

Ni suala la privacy, wewe unaweza piga picha unapokaa na kui-post kwenye mtandao kwa ajili ya watu ambao hujawahi kuwaona wapaone??
Kama miji mingine, Dar kuna Uswazi, matawi ya kati na matawi ya juu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…