Uchaguzi 2020 Naipenda CCM, Sipendi yanayojiri

Mkirindi

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
6,750
4,958
Ninakipenda sana chama changu cha CCM, lakini sifurahishwi na yanatoendelea:

1. Kwa mara ya kwanza campaigne ya Urais na Wabunge haina muelekeo. Magufuli umefeli sana na kukiharibu chama kwa kuwashirikisha vijana/ watu wasio na ujuzi wa namna kampeni zinavyoendeshwa.

2. Magufuli chukua hatua za haraka sana kubadilisha kampeni team yako.

3. Magufuli dhambi inayokusubiri ni chama kufia mikononi mwako, na dola kuwapa chadema, wanaichukua bila taabu yoyote, kwani mumekiweka chama kiholela.

4. Mmetumia pesa nyingi sana za chama, kuwarubuni na kuwanunua wapinzani, ambao hawana la kutuongezea, na ununuzi wao umeleta mfarakano ndani ya chama.

Mheshimiwa Rais, chukua ushauri, na rekebisha team yako, akina Polepole , Bashiru na wenzao wamefeli.
 
Dah hata wewe umeanza kulalamika lazima kuna jambo huko.

Ndiyo kwa sababu sisi hatuna unafiki na sio bendera. Tukiona kuna kosa ndani ya chama tunakosoa na kushauri, hatufumbii macho kama nyie. Nyie uozo wowote unaofanywa na viongozi wenu mnavimeza na kuvitetea. Not with me
 
Kwanza tuambie Jiwe yuko wapi na anafanya nn huko aliko??

Raisi yupo kazini, yeye anafanya kampeni na pia bado ni raisi wa nchi, na ana majukumu ya kitaifa, sio mtu asiye na kazi na mwenye kungojea akubaliwe maombi yake ya ukimbizi
 
hali hio yako pia ninayo mim kwa upande wangu hapa Mtaa wa ufipa tumekuwa makundi makund.
 
Ni hivi ukijua kweli nayo kweli itakuweka huru twende na Lissu atuvushe kwenye hili ombwe hata malaika wa Mbinguni watafurahi kama Mungu amememponya na kumweka hai mpaka leo na kama Mungu amekuponya na gonjwa la kutisha la Corona na kukuweka hai mpaka leo je wewe ni nani ukose kumpa lissu kura yako na kumrudishia Mungu Utukufu!?

Amini nakwambia lipo kusudi la Mungu juu ya maisha yako mimi na wewe la kutokufa mpaka kusudi la Mungu litimie mpe kura yako Lissu kuweka historia iliyotukuka ya leo na ya vizazi vijavyo.

Sent from my BLL-L22 using JamiiForums mobile app
 
NDIYO KWA SABABU SISI HATUNA UNAFIKI NA SIO BENDERA. TUKIONA KUNA KOSA NDANI YA CHAMA TUNAKOSOA NA KUSHAURI, HATUFUMBII MACHO KAMA NYIE. NYIE UOZO WOWOTE UNAOFANYWA NA VIONGOZI WENU MNAVIMEZA NA KUVITETEA. NOT WITH ME
Chama sio Baba yako au Mama yako useme utashindwa kukiacha kama wewe ni mcha Mungu kweli na una hofu ya Mungu basi kanawe mikono kama alivyonawa Pilato

Sent from my BLL-L22 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom