Kwa ile nyomi ya jana pale Tanganyika Packers, naiona dhahiri CCM ikitawala kwa zaidi ya karne moja tena.
Kwanini?
CCM ina wanachama wengi, zaidi ya milioni 13 na ndio chama chenye wafuasi wengi zaidi waliosajiliwa Barani Afrika na kimo kumi 10 ya vyama vyenye wafuasi wengi duniani.
CCM ina rasilimali zote za msingi kukifanya kuendelea kusalia madarakani kwa miongo mingi zaidi. Assets zake zinakadiriwa kufikia zaidi ya Tsh. Trilioni 1.5, ina midogi, viwanja vya mipira, kumbi na rasilimali nyingine za msingi.
CCM ina watu bwana, kuna aliyedhani kwamba Mama Asha Rose Migiro angerudi kubwa Katibu Mkuu wa chama? watu walishamsahau, lakini amerudi na kurudi kwake, ni ujumbe kwamba CCM ina hazina ya watu, tena watu wa maana ambao inaweza kuwatumia kwenye kuboresha shughuli za chama.
CCM ina connection ndani na nje ya nchi kama China, Cuba, Urusi na maeneo mengine nje ya nchi ambazo, zinazidi kuipa nguvu zaidi kuendelea kusalia madarakani.
Mwisho zaidi, CCM ina mikakati, tayari ina plan ya kuongoza 2030, 2040 na kuendelea hadi mwisho. Ukitazama kwa jicho la kawaida sana, utagundua kwamba hakuna chama kingine cha siasa hapa Tanzania, chenye msuli wa kushindana na CCM, hakipo.