Naingiaje payroll mpya ya Serikali?

Naingiaje payroll mpya ya Serikali?

Nimesema nimeajiriwa mwezi wa 6 mwaka huu, hivyo mwezi wa saba sitaingia kwa payroll
Hongera kwa kuajiriwa. Siku payroll ikisoma, utukumbuke basi na sisi wenzako tuliokosa ajira kwa mara 5 mfululizo.
 
Mifumo inaendeshwa na watu, hata wakisema sasa hivi ifutwe/isimamishwe inawezekana; muhimu tu, huyo mwenye mamlaka analichukuliaje hilo tatizo.
Nimekuelewa sana, umenikumbusha shida ambazo raia hupata kipindi waingiapo kwenye ofisi za serikali kuhitaji huduma, unakuta mtu anazungushwa hata miezi wakati ni kuhitaji tu saini ya mtu basi

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Wakuu nawasalimu kwa Jina la Jamhuri. Mimi nimebahatika kupata Ajira mpya za sasa hivi. Ila kuna changamoto moja iliyojitokeza ambapo nimeonekana kuwa na cheki namba tayari.

Iko hivi; Hapo kabla niliibiwa cheti changu cha kidato cha NNE na kuzaliwa , hivyo huyo MTU akaajiriwa kada ya afya.

Mimi ni Kada ya Elimu shahada na yeye alikuwa certificate (Afya) mnamo mwaka Jana nililifuatilia suala hili Utumishi, Baraza la mitihani. Ambapo kufikia mwaka huu Feb- April. Aliandikiwa Barua ya kufutwa KAZI kwa sababu ya kughushi vyeti.

Mungu si Athumani mwaka huu mwezi wa sita nami nikapata KAZI. Taarifa zangu zilivyoingizwa Tu ikaonekana tayari Nina cheki Namba.

Afisa Utumish WANGU aliwasiliana na Utumishi wa yule wa mwanzo .Na hivyo kuthibitisha kwamba Mimi siye(aliyekuwa nesi). Basi akasema yeye atawasiliana na makao makuu. Na hili suala litaisha. Japo mwezi wa 7 mshahara sitapata.

Nimekuja hapa kwa ushauri zaidi ndugu zanguni kwa wale mwenye experience.

N.b niombe kwa wale wenye kejeli na matusi wasi komenti.Machungu na matatizo niliyo nayo yananitosha.

AHSANTE
Pole sana, naomba nikuulize, kidato cha nne ulihitimu mwaka gani? Eleza ili watu wakusaide

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom