Hivi kwanini watu wanaamini kuwa Mungu yupo?

Hivi kwanini watu wanaamini kuwa Mungu yupo?

Sun is Sun

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2024
Posts
1,250
Reaction score
1,999
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nataka niwaulize tu, Kwanini mnaamini kuwa kuna Mungu?

Nawatakia wakati mwema.
 
Ni issue complex sana, lakini unaamini kuwa Dunia hii na ulimwengu huu wote uliyojaa ma trillion ya nyota na galaxies kwamba vilitokea tu Kwa tukio la ajali? Au mifumo ya kimaisha ya mimea na wanyama ilitokea tu Kwa ajali au kulikuwa na nguvu isiyoonekana Kwa macho iliyosababisha hayo kutokea? Kama unaamini Kuna nguvu fulani isiyoonekana Kwa macho ilisababisha hayo basi hiyo nguvu ndiyo Mungu
 
Tuko kwenye mudi na tafakuri ya mambo yanayotokea nchini halafu we unatuletea habari za uwepo au kutokuwepo kwa Mungu, unataka tukujibuje? kama we huamini uwepo wa Mungu usitusumbue, baki na upagani wako au nenda kanisani ukamjue Mungu na nguvu zake
 
Ngoja nimjibu,
Mimi naamini Mungu yupo kwa sababu tangu aumbe viumbe vyote vipo jinsi hiyohiyo kama alivyoviumba.
Mfano mwanadamu.
Tunaaminishwa kuwa binadamu alitokana na nyani/sokwe, haya, hebu nikubali sawa, kisha niulize swali je huyo sokwe/nyani aliumbwa na nani!? Au alitokeaje?
Kwanini haendelei kutokea na kuendelea kubadilika?

MUNGU YUPO BANA!!
 
Mimi naongezea swali kwamba;
1. Kwanini watu wanaamini stori za kwenye biblia, kurani, Torati, Talmud n.k ni maneno ya Mungu?

2. Mmeshawishikaje kuamini kwamba waandishi zaidi ya 40 walioandika vitabu na story za biblia walikuwa wanaandika kwa niaba ya Mungu?
 
Kwa sababu nikiona jua na ule mwanga wake naamini kuna super being ambae ni God ndio ka create sun is sun.....
 
Utakuwa bado kinda sana.

Ngoja kwanza ukuwe.

Na kukuwa ni kupata Changamoto za maisha.
 
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nataka niwaulize tu, Kwanini mnaamini kuwa kuna Mungu?

Nawatakia wakati mwema.
Kwa kuamini kwao Mungu yupo wewe unapata hasara gani faida gani au kwa wewe kutokuamini kama Mungu yupo unadhani wao wanapata hasara gani au aida gani?

Ujinga tu,unapenda mpira sipendi mpira unapenda pombe sipendi pombe kwani haitoshi kuishi kwenye codes ulizojipangia mwenyewe hata utake kuingia kwenye anga za wengine?
 
Hii mada tata, ila nimewahi ulizwa hili swali kwa style tofauti,

Kama Ukifa unaenda peponi au motoni..je kuna mtu aliwahi enda akaleta feedback?
 
Ni issue complex sana, lakini unaamini kuwa Dunia hii na ulimwengu huu wote uliyojaa ma trillion ya nyota na galaxies kwamba vilitokea tu Kwa tukio la ajali? Au mifumo ya kimaisha ya mimea na wanyama ilitokea tu Kwa ajali au kulikuwa na nguvu isiyoonekana Kwa macho iliyosababisha hayo kutokea? Kama unaamini Kuna nguvu fulani isiyoonekana Kwa macho ilisababisha hayo basi hiyo nguvu ndiyo Mungu
Kwanini hiyo Nguvu ndio Mungu na si kitu kingine??
 
Ngoja nimjibu,
Mimi naamini Mungu yupo kwa sababu tangu aumbe viumbe vyote vipo jinsi hiyohiyo kama alivyoviumba.
Mfano mwanadamu.
Tunaaminishwa kuwa binadamu alitokana na nyani/sokwe, haya, hebu nikubali sawa, kisha niulize swali je huyo sokwe/nyani aliumbwa na nani!? Au alitokeaje?
Kwanini haendelei kutokea na kuendelea kubadilika?

MUNGU YUPO BANA!!
Umewqza kitoto sana ,nani aliyekwambia alivyoumba ndio vimebaki hivyohivyo?? Hujui maama ya evolution?? Hilo swali la nyani aliumbwa na nani aliyokeaje?? Hata wewe ukiulizwa huyo mungu aliumbwa na nani aliyokeaje huwezo kujibu .
Hilo swali la kwanini haendelei kubadilika pia ni la kitoto,evolution ni mchakato wa mamilioni ya miaka kwahiyo hata ewe ishi miaka milioni utaona wakibadilika
 
Back
Top Bottom