Naibu Waziri wa TEHAMA, Kundo Andrea ashauri TCRA kuanzisha mitandao yetu ya kijamii tuachane na Twitter, FB, YouTube n.k

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,309
24,204
Kuelekea uchumi wa kidigitali Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeitaka mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA kufikiri namna ya kutoa fursa kwa waTanzania wenye uwezo wa kuanzisha mitandao ya kijamii ya ndani ya nchi ili kukuza uchumi na usalama wa nchi.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari mhandisi Kundo Andrea amesema kuwa sehemu kubwa ya uchumi wa makampuni ya mawasiliano unaendeshwa na mitandao ya kijamii na inachangia kiwango kikubwa cha uchumi wa nchi kupitia vifurushi kwa mitandao ya kijamii "Facebook, Instagram, whatsapp zikiwa shutdown leo makampuni ya simu yatalia na uchumi wetu ukashuka.

Sasa tuhakikishe tunapromote local content siku moja tuwe na Facebook, Instagram, twitter yetu itafanya uchumi wetu kuwa stable na tutakuwa tumeimarisha usalama wa nchi yetu" Eng. Kundo

Source: millard ayo
 
Nikisoma between the lines kama kuna kitu anataka sema...

Ngoja niunge doti..

China mpaka leo whatsapp imepigwa ban, google na fb nadhan hazipo pia!!

Je tunataka fwata nyayo za china?

Ke haya yote yanawezekana vipi kwenye huu mfumo mbovu wa elimu ambao injinia wa kompyuta hawezi hata kuunda website?

Huyu mtu sio wa kumdharau... kuna kitu kipo!!

NB: JamiiForums ni mtandao wa kitanzania na mpaka sasa una kesi mhakamani iliyo funguliwa na serikali.
 
Waibadilishe JamiiForums iwe fesibuku ya huku. Ila tuendelee na utaratibu huu huu wa kuficha majina japo taarifa za zikihitajika kwenye mamlaka sijui itakuwaje
 
Naibu Waziri hajui majukumu ya TCRA kwa mujibu wa Act ya bunge ya kuanzishwa kwake , fedheha sana
Tatizo la Mkuu hateui huko buku 7 fc , laiti angewateua kutokana na uzoefu wenu humu jf mngeweza kumsaidia kuliko hawa wengine anaowaokota kusikojulikana
 
Back
Top Bottom